Waziri
 wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wapili 
kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es 
Salaam kuhusu tamko la Serikali juu ya mgogoro wa mpaka wa ziwa Nyasa. 
SERIKALI ya
 Tanzania imeomba  Malawi iache kutapatapa kuhusu mgogoro wa mipaka wa 
ziwa Nyasa kufuatia Rais  wa nchi hiyo, Joyce Banda kutangaza katika  
baadhi ya vyombo vya  habari  kuwa atapeleka  suala hilo kwenye Mahakama
 ya Kimataifa ya Haki(ICJ), badala yake isubiri uamuzi wa jopo la 
usuluhishi lifanye kazi na litoe maamuzi.
Aidha
 serikali  imesema kuwa hata siku moja  haijapelekewa taarifa wala 
nyaraka za siri kutoka kwa Katibu wa jopo hilo, ambalo linahusisha 
marais wastaafu wa zamani wa Afrika na wanasheria  kama ilivyodaiwa  na 
 Rais  Banda katika vyombo hivyo , kuwa kuna Mtanzania anayeitwa Dk. 
John Tesha ambaye wanaamini ametoa  habari na kuiba nyaraka za siri.
Akilitolea
 ufafanuzi   jambo hili, Waziri Membe amesema kuwa  Tanzania na jopo 
hilo   limestushwa juu ya madai hayo na hatua ya Rais Banda kupoteza 
imani.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog