Wenye medali zao wakishuka kwa kasi 
 
 
 
 
 
 Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza 
Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ 
zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. 
  
 
Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za 
Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza 
 katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na 
Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya Dhahabu. 
  
 
Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius 
Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa 
wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara. 
 
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za 
Kilimanjaro Marathon 2013.  
 |