Lulu
 na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu 
amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni 
mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda 
mrefu sana.
Ama kwa hakika nnje ya mahaka pamegeuka kilio mara muigizaji elizabeth 
michael kuachiwa kwa dhamana leo tarehe 29 lulu amepewa dhama kutokana 
na kesi inayomkabili ya kumuuwa bila kukusudia aliyekuwa star wa bongo 
movie marehemu steven kanumba.
Mara baada ya lulu kumuona mama yake wamejikuta wakiangua kilio hadi 
watu wakaribu wakawa wanashangaa.kazi ilikuwa kwa muigizaji dk cheni 
ambaye kiukweli katika watu wakupongezwa katika hili anachukuwa nafasi 
ya kwanza kwa binadamu ,cheni amekuwa mstari wa mbele kumsimamia lulu 
hadi amepata dhamana.
![]()  | 
| Lulu akiingia kwenye gari huku akisaidiwa na Dk cheni kwa nyuma yake | 
Mama yake lulu aliwahi kukaririwa akisema kwa sasa anamuona cheni ni 
zaidi ya binadamu wa kawaida kwani bila yeye hajui kama ataweza 
kumuokowa mwanae mama huyo amejikuta akilia kwa furaha baada ya kumuona 
tena mwanae huyo.
Dk chen amezungumza na thesuperstarstz na kutuambia anashukuru mungu 
kwakumpa moyo wa ujasiri wa kumsaidia binti huyo kwani wengi walimsusa 
lakini tukumbuke mungu ndiye mlipaji wa yote hatupaswi kumuhukumu mtu 
kwani hata mahakama bado haijamuhukumu lulu sasa sikuona sababu ya 
baadhi ya wasanii kujitenga na lulu na ndio maana nikajitolea kumsaidia 
hadi nijue mwisho wake.
![]()  | 
| Lulu akilia kwa furaha na kushindwa hata kuongea chochote alipokuwa anahojiwa jambo lililofanya cheni amuongelee | 
Cheni ambaye ni mmoja kati ya wadhamini waliotoa milioni 20 za 
kitanzania cheni amekuwa masaada mkubwa sana kwa lulu jambO ambalo 
limefanya lulu kumuona cheni ni zaidi ya baba yake kwa sasa na ndio 
maana mara nyingi hata kabla ya tukio la lulu na kanumba kutokea  bado 
lulu alikuwa anamuita cheni baba japo  haikujulikana kwanini na cheni 
katika familia ya kina lulu anaheshimika sana na ndio maana haikuwa 
rahisi kwake kutojitolea kwa hilo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog


