Pichani kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akipokea 
 Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ulioongozwa 
na  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana uliofika kwenye 
uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot),kuangalia maendeleo ya 
ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategemewa kwa asilimia 
kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.UJumbe huo umewasili mapema 
jana kutoka jijini Dar kwa njia ya Treni ( reli ya kati),ambako wamekuja
 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.
Sehemu ya kuruka na kutua ndege ikiwa katika hutua ya mwisho mwisho,Kwa mujibu wa Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo ameeleza kuwa unatarajiwa kukamilika mnamo juni mwaka huu,ambapo kwa asilimia 80 maeneo mengi yatakuwa yamekwishakamilika.
 Pichani kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa   
Machibya,akimtambulisha  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman 
Kinana kwa baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kwenye uwanja wa Ndege 
wa Kigoma (Kigoma Airpot) kuwapokea,ambapo Mh Kinana na ujumbe wake 
waliwasili mapema jana  jioni kuangalia maendeleo ya ukarabati na 
upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategewa kwa asilimia kubwa na wakazi
 wa Kigoma,ndani na nje. 
 Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. 
Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wakiwemo wanachama wa 
CCM,waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma mapema jana jioni 
walipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.
 Mafundi ujenzi wakipaka rangi sehemu ya barabara ya kurukia na kutua ndege mapema jana jioni.
 Ujenzi ukiendelea.
Meneja uwanja wa Kigoma Elipid Tesha,wa pili kuli akifafanua jambo kwa ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),uliofanya ziara fupi ya kuukagua uwanja huo na kujionea ujenzi wake unavyoendelea kwa kasi,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh Issa Machibya akishuhudia tukio hilo adhimu, na shoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, pamoja na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro

Sehemu ya eneo ambalo linaendelea kupanuliwa ikiwa ni sehemu ya ongezeko ya marekebisho ya kiwanja hicho cha Kigoma
Pichani kati Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa 
Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo akifafanua jambo mbele ya 
ujumbe wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog







