Taarifa za uhakika zilizopo
 kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la uigizaji 'Lulu' akatoka kwa 
dhamana kesho January 25, 2013. Kutokana na dhamana ambayo inatarajia kusikilizwa kesho Ijumaa.
Uhakika wa Lulu kupata dhamana 
ulikua jana jumatano january 23 lakini ikashindikana kutokana na 
kuahirishwa kwa sababu Jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za 
dhamana kilikua hakijatimia.
Chanzo cha kuaminika 
kilichoongea kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae 
amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.
Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, na baadae mashitaka yake yalibadilishwa na kuwa Ameua bila kukusudia, kitu ambacho kinampa nafasi ya kuweza kupata dhamana. 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog