Kikao cha kamati ya ulinzi na usalama chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa
 Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya kimeridhia kusitishwa kwa Mkataba 
wa Mkandarasi M/S Kalyango Contructoins And Building Company Limited 
aliyekuwa akijenga daraja Nkwasi Wilayani Uvinza.
Mkandarasi
 Kalyango  Construction alikabidhiwa eneo la kazi Julai 5, 2012 na 
kutakiwa kukamilisha ujezi wa daraja la NKWASI   Okitoba 15, 2012, 
lakini pamoja na kuongezewa muda hadi Desemba 30, 2012 mkarandasi huyo 
alishindwa kukamilisha kazi hiyo.
Hadi
 anasimamishwa mkarandasi huyo alikuwa amelipwa zaidi ya milioni 25.7 
ambazo ni kati ya shilingi milioni 97.4 alizostahili kulipwa kama 
angekamilisha ujenzi.
Baada
 ya taarifa ya mkuu wa mkoa safari  ikawa ni kuelekea eneo la ujenzi 
ambapo meneja wa wakala wa barabara mkoani Kigoma Narisi Choma ndiye 
aliyetoa taarifa kwa wafanyakazi wa  mkarandasi Kalyango kuwa hawatakiwi
 kuendelea na kazi.
Muda
 na  kwa nyakati tofauti wajumbe wa kamati ya  ulinzi na usalama, katika
 ziara zao, wamekuwa wakiwaonya wakandarasi wanaofanyakazi chini ya 
kiwango, kauli ambazo zinaungwa mkono na wakazi wa mwambao wa kusini mwa
 ziwa Tanganyika.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog