Kamanda
 wa jeshi la polisi mkoa wa Singida (wa kwanza kushoto mwenye fimbo) 
akiangalia daraja lililobomoka la Munung’una lililopo barabara kuu ya 
Singida – Mwanza eneo la  kijiji cha Msisi wilaya ya Singida.
Mhandisi
 wa TANROADS mkoa wa Singida,Yustaki Kangole akiwaelekeza jambo 
wahandisi wa kampuni ya CHICO iliyojenga daraja lililobomokajuzi la 
kijiji cha Msisi wilaya ya Singida.Daraja hilo lililopo kwenye barabara 
kuu ya Singida – Mwanza,limebomoka baada ya kuzidiwa na maji ya mvua 
kubwa iliyonyesha siku moja kabla ya mwaka mpya.
Baadhi
 wa wasafiri waliokwama baada ya daraja la Munung’una lililopo katika 
barabara kuu ya Singida – Mwanza eneo la kijiji cha Msisi wilayani 
Singida, kubomoka juzi kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mkoani Singida.athaniel Limu
Mvua
 kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Singida,zimeendelea kuleta maadhara
 makubwa ikiwemo kuvunja daraja na barabara kuu ya Singida – Mwanza na 
kuua raia moja  wa nchini China.
Juzi
 mvua hizo zilisababisha familia ya watu wanne ya wilaya ya Mkalama mkoa
 wa Singida, kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba ya tembe.
Mvua
 hizo kubwa  zilizonyesha kuanzia  mwaka mpya (1/1/2013) saa nane mchana
 hadi saa 12.30 jioni zilisababisha daraja la Munung’una lililopo katika
 kijiji cha Msisi wilayani Singida, barabara kuu itokayo Singida 
kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Kongo, Burudi, Rwanda 
na Uganda, kubomoka na kusabaisha shimo kubwa.
Kubomoka
 kwa daraja hilo kumechangia foleni kubwa ya magari yanayokadiriwa kuwa 
ni zaidi ya mia tatu. Pia mawasiliano kati ya mikoa mbalimbali ikiwemo  
ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani yamekatika.
Mmoja
 wa madereva walioathirika na kubomoka kwa daraja hilo, George Medadi, 
aliyekuwa akitokea Mwanza akirudi jijini Dar-es-salaam, alisema kubomoka
 kwa daraja hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya 
kiwango.
“Wenyeji
 wa hapa wametueleza kuwa kalvati zilizotumika ni zile za zilizowekwa 
wakati Nalaila Kiula alipokuwa Waziri wa Ujenzi. Kampuni ya CHICO 
iliyojenga barabara hii kwa kiwango cha lami waliyatumia makalivati hayo
 hayo na walichofanya ni kulundika udogo juu tu,” Medadi alisema.
Naye
 dereva Iddi Mussa alisema kuwa barabara nyingi zinazojengwa na kampuni 
za kichina zimekuwa hazisimamiwi ipasavyo kitendo kinachochangia 
kuharibika haraka na kuisababishia serikali kuingia hasara kubwa.
Kwa
 upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi alisema kwa 
kuanzia wameimarisha ulinzi katika eneo hilo pamoja na kufungua kituo 
kidogo cha kutolea huduma ya afya na kudhibiti uwezekano wa kutokea kwa 
magonjwa ya mlipuko.
“Pia
 tumefungua barabara ya Singida-Ndago –Misigiri kwa ajili ya kutumiwa na
 mabasi ya abiria na yale yenye uzito chini ya tani kumi. Vile vile 
tunaangalia uwezekano wa kuangalia ni namna gani watu waliokwama 
wanapata chakula,” alisema.
Meneja
 wa TANROADS Mkoa wa Singida, Mhandisi Yustaki Kangole, ambaye alifika 
na wahandisi wa kampuni ya CHICO, alisema kuwa wamekubaliana na CHICO 
kwamba  wafukie shimo hilo kwa vifusi vya mawe makubwa ili barabara hiyo
 ianze kutumika mapema iwezekanavyo.
“Kwa
 sasa tunafanya kazi hii ya muda na baada ya eneo hili kukauka ndio 
ukarabati mkubwa utafanywa ili kuimarisha barabara hii muhimu kwa uchumi
 wa taifa,” alisema Mhandisi Kangole.
Wakati
 huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Edward Ole Lenga amesema kuwa raia 
moja wa China amefariki dunia baada ya gari lake kusombwa na maji ya mto
 jirani na kijiji cha Gumanga.
Alisema
 Mchina huyo ambaye jina lake bado halijatambuliwa hadi sasa, alisombwa 
na maji ya mto juzi  majira ya jioni wakati akikatisha mto wa kijiji cha
 Gumanga wilaya ya Mkalama. Ndani ya gari hilo alikuwa na mtoto wake 
ambaye alinusurika kufa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa zaid atatoa baadae.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog


