Chris Brown na Rihanna ndani ya Swimming Pool

Nyumba ya Chris Brown iliyopo Holiwood Marekani
Polisi Hollywood Marekani 
wanamtafuta mwanaume ambae aliwafanya wakimbie spidi mpaka kwenye jumba 
la mwimbaji staa Chris Brown baada ya mwanaume huyo kuripoti habari za 
kutisha kwa alichoshuhudia nyumbani kwa Chris Brown.
Kwa mujibu wa CME, huyu 
mwanaume akijidai ni shuhuda alipiga simu kuomba msaada polisi baada ya 
kudai kashuhudia ugomvi wa mwanamke na mwanaume ukiendelea kwenye nyumba
 ya Chris Brown na baadae risasi zikapigwa baada ya majibizano ya mdomo 
kuzidi.
 Kwa mujibu wa polisi ambao 
walikimbia spidi kuokoa hiyo hali kuendelea, hakuna chochote 
kilichotokea nyumbani kwa Chris Brown ambae hata hivyo hakuwepo nyumbani na wala 
hakuja tokea tukio kama hilo kwenye huo mtaa ndio maana kwa sasa 
wanachunguza ni nani alipiga simu na akawazingua kwa kuwapotezea muda na
 mafuta.
Huyu jamaa alikua anamaanisha 
ugomvi wa mwanamke na mwanaume yani ni Rihanna na Chris Brown ambao 
wanadaiwa kurudiana mapenzini sasa hivi baada ya kuachana kwa kesi ya Chris Brown
 kumpiga Rihanna kwenye penzi lao la mwanzo. 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
