Mtu mmoja ameuwawa mida hii katika majibizano ya risasi 
yaliyotokea maeneo ya Msimbazi kariakoo, mtaa wa Livingstone kati ya 
Polisi na majambazi waliotaka kupora fedha zilizokuwa zinapelekwa benki 
ya NBC.
 
 Majambazi hao waliokuwa wamevalia nguo za kiraia 
inasemekana walijua fedha hizo zinapelekwa leo hivyo walijiandaa kupora 
na Mapolisi nao waligundua hilo mapema hali iliyofanya majambazi hao 
kurusha risasi hovyo na kukimbia ili kukwepa kukamatwa.
 
 Hadi 
sasa ni mtu mmoja anayeripotiwa kuuwawa ila bado haijajulikana kama ni 
raia au jambazi wale maana pia majambazi walivaa kiraia.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog