Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya 
na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari wa
 Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo 
hicho mwaka  2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza
 Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 
2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
 Makamu
 Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata 
Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha Udaktari
 wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na 
Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika 
kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar 
es salaam..
Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Ardhi 
Prof Anna Tibaijuka, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein 
Mwinyi na viongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili 
baada ya kukabidhiwa  Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris 
Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka  2010 kwa 
Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini 
leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. 
Rais
 Jakaya  Mrisho Kikwete  akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa 
Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko 
wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel 
Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam .
 Rais
 Jakaya  Mrisho Kikwete  katika picha ya kumbukumbu baada ya kupata 
 maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha 
Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health 
Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar
 es salaam.
K
 Rais Jakaya  Mrisho Kikwete  na ujumbe wa Wizara ya Afya na  Mfuko wa 
Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba 
leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam
=======  ========  =========  
Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa Novemba 23, 2012 amepokea taarifa ya 
maendeleo ya ujenzi wa Kampasi mbili za tiba ya afya vinavyojengwa 
katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mloganzila huko Kisarawe, ambavyo pia 
vitatumika kama hospitali hapa nchini.
Kwanza
 Rais amepokea maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha 
Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health 
Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba .
Ujenzi wa kampasi hii  umeshaanza na kufikia hatua ya juu na hospitali inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015.
Kulingana
 na Bw. Humba, maandalizi ya kufanikisha uanzishaji wa Chuo/ Hospitali 
hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na 
watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na 
mafunzo mbalimbali.
Chuo
 hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi 
mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa.
Rais
 pia amepokea taarifa ya  maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila 
ambapo katika ujenzi na uanzishwaji wa Kampasi hizi zote, Rais Kikwete 
amesimamia kuanzia hatua za awali.
Kampasi
 ya Mloganzila ambayo ni sehemu ya Hospitali kuu ya Muhimbili inajengwa 
kwenye eneo la ekari 3800 na itakua sehemu ya kutolea mafunzo kwa 
wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya, lakini pia itakua sehemu ya 
kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na  ya kawaida nchini.
Ujenzi
 wa Hospitali hii unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na
 unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi.
Katika
 hafla hiyo Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
 Prof. Ephata Kaaya ametumia nafasi hiyo kumkabidhi Rais Kikwete Cheti 
cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada 
aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili 
Disemba, 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza 
Sekta ya Afya nchini.
Akitoa
 taarifa hiyo ya maendeleo kwa Rais Kikwete, Prof. Kaaya amesema tayari 
wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya 
Mloganzila wameshaanza mafunzo. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa 
itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita 
(600).
Rais
 Kikwete amewapongeza wataalamu wote kwa juhudi zao na kuwa ahidi kuwa 
lengo lake ni kuhakikisha nchi inaondokana na adha ya kupeleka wagonjwa 
nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Rais
 amesema moja ya lengo kubwa la serikali yake,  ni kutoa kipaumbele 
katika sekta ya Afya ili kuhaklikisha watanzania wanapata huduma bora, 
kupanua mafunzo ya Afya na kuongeza wataalamu watakaoweza kutibu 
magonjwa yote makubwa hapa hapa nchini.
Rais
 amewaahidi watendaji wa Kampasi zote mbili kuwa atahakikisha ujenzi wa 
huduma hizi muhimu kwa Umma haukwami kwa sababu ya ukosefu wa pesa kwani
 ni jambo ambalo amedhamiria.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
23 Novemba, 2012.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog





