Pichani ni sehemu ya paa la chumba cha habari cha chama cha mpira wa 
miguu Tanzania (TFF),ambacho kinatumika kukutana na Wanahabari wa vyombo
 mbalimbali  kuhusiana tasnia ya michezo kwa madhumuni ya kuihabarisha 
jamii.Kwa wanahabari za Michezo naamini kabisa mtakubaliana na mimi 
kuhusiana na hali iliyopo ndani ya ofisi hiyo,ambayo kimsingi nayo una 
umuhimu wake mkubwa,lakini imetelekezwa kama hivyo.
 Chombo cha kutoa ubaridi ambacho kiliwekwa angalau kupunguza joto la 
Daslam ofisini humo,lakini kwa sasa ndege wamepata mahala pa 
kujipumzikia na kuzaliana,lakini sio ishu.
 Taa nazo ziko hoi zinaning'inia tu, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watu.
 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo  mbalimbali wakisubiri wahusika wa 
TFF, kukutana na Wanahabari hao kwa ajili ya kuwapa taarifa mbalimbali 
za michezo, ili jamii ihabarishwe.
 Dude la kuwekea Maji ya Kunywa ambalo sijui kwa mara ya mwisho  lilitumika lini,kwani limejaa vumbi, haliangaliwi tena.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog



