Facebook Comments Box

Wednesday, July 15, 2015

HATIMAYE CUF WATOA MSIMAMO WAO KUHUSU KUJITOA / KUBAKIA UKAWA

Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kama wanavyo onekana wakiteta jambo Toka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, wa katikati yao ni Profesa Lipumba wa CUF na mwisho ni Joseph Mbatia wa NCCR.

Viongozi hao wakiwa wameshikana mikono kuonesha kuwa wao ni wamoja.

Baada ya Chama cha mapinduzi CCM kumpata Mgombea wake wa kiti cha urais wiki iliyopita mkoani Dodoma ambae ni John Pombe Joseph Magufuli.
 
Wanachama wa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) wamekuwa na duku duku la kufahamu mgombea wao atakuwa nani.

Hali hiyo imeleta hamasa sana kwa wanachama hao kiasi cha kuona kama viongozi wao wanachelewa kuwajulisha mgombea wao ni nani na pia kuleta hofu kuwa CUF wamejitoa katika umoja huo.

Lakini CUF kupitia Naibu Katibu Mkuu wao wa Bara Magdalena Sakaya ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazoendelea kuenea, amethibitisha kuwa wao hawaja jitoa Ukawa na kuhusu kutokuwepo kwenye kikao akasema walichelewa kupata taarifa za kikao hicho maana hata wao wana vikao vingi ambapo wanajadili jinsi ambavyo madaraka yatakavyo kuwa endapo wakishinda uchaguzi mkuu huo ambao utafanyika Oktoba.
Naibu Katibu Mkuu wa Cuf Bi Magdalena Sakaya akijibu baadhi ya Tuhuma hizo


Friday, June 5, 2015

BARCELONA NA JUVENTUS ZAWASILI KATIKA JIJI LA BERLIN TAYARI KWA FAINALI YA UEFA JUMAMOSI TAR 06-05-2015

 Mabasi ya timu hizo kama yanavyo onekana hapa:
Andrea Pirlo kama anavyo onekana hapo akishuka kwenye ndege:


175 WATHIBITIKA KUFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO GHANA

Takriban watu 175 wamefariki mpaka sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na stima.

Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto huo, Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
 
Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.

Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena. Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu, Accra alipotembelea eneo la tukio.



AFISA MMOJA WA FIFA AKIRI KUPOKEA RUSHWA

Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayoelezea jinsi Afisa wa zamani wa FIFA Chuck Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ikiwa ni pamoja na kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2010.

Katika taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa malipo ya rushwa ulivyokuwa ukifanywa ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA, taarifa zinazoegemea uchunguzi uliofanywa na shirika la kijasusi la Marekani FBI.

Taarifa hiyo ambayo inamwelezea Afisa huyo wa zamani wa Fifa kukiri kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayoindamana shirikisho la FIFA.

Mmerakani huyo kwenye taarifa hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998.

Taarifa za Kukiri zipo katika maandishi wakati wa kesi yake mwaka 2013 ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama ya Easten New York huko Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa yanamkabili.

Blazer alikuwa afisa wa ngazi ya juu wa FIFA eneo la kanda ya Amerika Kaskazini na Kati na ukanda wa nchi Caribbean kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2011.

Marekani imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.

CHANZO: BBC

Tuesday, March 10, 2015

MANCHESTER UNITED YATOLEWA NA ARSENAL F.A CUP OLD TRAFFORD

 Monreal akishangilia bao lake
 Danny Wellbeck akiifunga timu yake ya zamani bila huruma
 Angel Di maria akioneshwa kadi nyekundu na Mwamuzi baada ya kupata kadi mbili za njano, wakati timu yake ilipotolewa na Arsenal katika kombe lenye hadhi kubwa nchini Uingereza la F.A kwa kufungwa mabao mawili kwa moja(1-2).
Sant Carzola na Laurent Koscielny wakishangilia baada ya kipyenga cha kuashiria kuwa dakika 90 zimekamilika.

Kocha wa zamani wa Manchesta Utd Alex Furgasson alikuwepo uwanjani hapo kushuhudia timu yake ikifungwa katika kombe hilo lenye hadhi kubwa Uingereza.



Sunday, March 8, 2015

RAISI KIKWETE AREJEA NCHINI BAADA YA ZIARA YA SIKU MOJA NCHINI RWANDA

   Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokwenda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na aliyekatikati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi Sophia Mjema



Saturday, March 7, 2015

AENDA JELA KWA KUWAHI KUFIKA KAZINI NA KUANZA KAZI YAKE MAPEMAA

Kevin McGill

Mwendesha lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la Georgia nchini Kevin McGill Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.

Kervin McGill yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua usumbufu kwa 

wengine na majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.

Kesi hiyo imewashtua watu wengi na kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari huku wengi wao wakiwa wamepigwa na butwaa kwa mtu kwenda jela kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. 

Mtu kama huyu alistahili kupata onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.


WAMJUA SAID SALIM BAKHRESSA? HEBU MUONE HAPA KATIKA UZINDUZI WA STUDIO ZAKE ZA KISASA ZILIZO ZINDULIWA NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


a7_2b2c5.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a2_58044.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a5_f5589.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam, Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa
a8_8c9ac.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
ssb1_82b8d.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a6_cc23b.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU