Facebook Comments Box

Wednesday, November 5, 2014

REAL MADRID YAINGIA HATUA YA 16 KWA KUIFUNGA LIVERPOOL

Timu ya R.Madrid jana usiku ilipata ushindi kiduchu kwa kuichapa Liverpool ya England katika michuano ya kuitafuta Klabu Bingwa wa Ulaya. Wenyeji walipata bao la kuongoza na la ushindi katika dakika ya 27 ya mchezo kupitia kwa Kareem Benzema.
 Uwanja wa Santiago Bernabeu ulipofanyika mchezo huo kati ya wenyeji R.Madrid vs Liverpool.
 Kareem Benzemaa akishangilia bao lake lililoipa ushindi Real Madrid dhidi ya Liverpool.
Wachezaji wa Real Madrid wakimpongeza mfungaji wa bao pekee la mchezo huo, Kareem Benzemaa.
 Kareem Benzemaa katikati ya Kolo Habib Toure na Martin Skrtel.



Tuesday, November 4, 2014

MRISHO NGASSA NDIO MFUNGAJI BORA AFRIKA

Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa amepata zali Afrika, baada ya kumaliza kinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake kuaga mashindano hayo katika mzunguko wa pili. Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.

Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya wakibebwa na bao la ugenini kutokana na matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa Algeria na sare mabao 2-2 mchezo uliochezwa Kinshasa.

Ngassa aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2. 

Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huwa haitoa zawadi.


HISTORIA FUPI YA MAREHEM JAFAR SIRAJ

Kabla ya kuwepo MuM alikuwa ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu cha Kiislamu Ubungo Islamic Teacher's College ambako alihitimu mwaka 2004 na kisha akasomesha Msamala Muslim Songea na baadae Matangini Islamic Dar, akajiunga na
Chuo cha Waislamu Morogoro wakiwa ndio Batch ya mwanzo 2005. Baada ya kuhitimu alichaguliwa kuwa Mhadhiri Msaidizi na mwaka mmoja baadae alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamili na kurejea MuM ambako amekuwa akifanya kazi mpaka mauti yalipomkuta.

Bro. Alianza kupata mtihani wa maradhi mwaka 2011 na 2012 au 13 aligundulika kuwa na Maji kwenye mapafu waislamu wakachukuwa  jukumu la kumpeleka India kwa matibabu akafanyiwa upasuaji na tatizo likapungua alirejea Alhamdulillaah ingawa alionekana wazi kuwa tayari amedhoofika, hakuwa Siraji yule handsome tuliyekuwa tukimjua.

Bro. Katika uhai wake ukiacha kwamba alikuwa superbright kitaaluma na kihoja na aliyekuwa na khofu ya dhati kwa Mola wake alikuwa role model, and very inspiring, fasaha na mtulivu sana asiye na papara katika mambo yake na huu ni sehemu ya urithi aliyotuachia.

Bro. Siraji alikuwa mtu huru na anayenyoosha maneno alipokuwa akisimamia haki, Kipindi cha mwangaza wa jamii Radio Iman na wasikizaji wake watashuhudia kwa hili na watasikitika sana kipindi hiki kumkosa huyu Akhy.

"Hao ni umma umekwishapita, wao wana malipo yao nanyi mna malipo yenu wala hamtoulizwa wao wamefanya nini (Bali mtaulizwa ninyi mmefanya nini) 2:141

Bro. Siraji ameacha mke na  watoto wawili wa kiume. Tunaamini wajibu wake kwa jamii ya waislamu na watanzania kwa jumla ameutekeleza kikamilifu na hivyo anastahiki akapumzike.

Sisi sote ni wa Allaah na kwake ndio Marejeo. Allaah amsamehe madhambi yake amrehemu na ampe makazi mazuuri peponi.


Sunday, November 2, 2014

MLIPUKO WA KITU KINACHODHANIWA KUWA BOMU WAUA MMOJA KISHAPU



Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45 hrs katika center ya Muhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu.

Gari no T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, Muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) msukuma wa Muhunze.

Wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid 21-23, mwangaza wa Ngara ambaye ni
familia ya mwenye gari.

Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.

Pia mfanyabiashara Donard s/o Nzugala Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.

Wengine ni Maganga s/o Piusi (14 ), msukuma,mkulima wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto, mgongoni na mkono wa kushoto.

Seni s/o Edward (25 ), msukuma mkulima wa Lubaga Kishapu amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa.



SIMBA YAENDELEZA SARE: PHIRI ABAKIZA MECHI MOJA KUTIMULIWA


SIMBA SC imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya jana.

Hii inakuwa ni mechi ya 12 kwa Simba bila ushindi ukijumlisha na mechi sita za mwisho za msimu uliopita. Swala hili la kutoa suluhu limepelekea Simba kumpa kocha wa Phiri mechi tatu za mwisho na akihitajika kushinda mechi mbili. Jana wametoa suluhu mechi ya kwanza na zimebaki mbili, Hii ina maana akitoa suluhu yoyote au kufungwa ndio utakuwa mwisho wa Kocha huyo ambae ana historia ya kuja Simba na kufundisha mara kwa mara nusu msimu ikifika  msimu mwingine anaaga kuwa ana matatizo ya kifamilia na harudi tena.

Suluhu hiyo inawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC imefikisha pointi 6 jana.Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki wa kimataifa wa Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi.
 
Hali hiyo iliwafanya vinara wa hao wa Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika ya 58, mfungaji Mussa Hassan Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia, William Lucian ‘Gallas’ kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.

VIKOSI VILIKUWA HIVI:
 
Mtibwa Sugar: Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka na Ally Shomary.

Simba SC: Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Awadh Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla na Emmanuel Okwi/Uhuru Suleiman dk75.


Saturday, November 1, 2014

PICHA YA LEO: KIONGOZI WA YANGA AKIKAGUA UDONGO WA UWANJA

Yanga leo inapambana na timu ya Kagera Sugar chini ni picha ya mmoja wa viongozi wa Yanga akifukia kitu katika uwanja wa kaitaba jana.



Friday, October 31, 2014

SHEIKH SORAGA UNAJICHANGANYA NA UNAPOTOSHA

Sheikh Fadhil S. Soraga
Hivi karibuni kumekuwa na barua ya katibu wa mufti wa zanzibar Sheikh Fadhil S. Soraga kilichonichanganya ni Katibu huyo kuto ikanusha barua hiyo ambayo haina kichwa cha juu cha barua na anuani (Headed letter). Ukiiangalia utaiona imekaa kama tangazo na chini ina saini ya sheikh huyo.Nadhani wengi wetu hatuuijui saini ya Sheikh Soraga na huenda watu wameitumia vibaya ili kumdhalilisha. Kingine kinacho nichanganya ni kuwa kikao kilifanyika tarehe 18 mwezi wa 8 kwanini leo ndio iwekwe kwenye mitandao ya kijamii na iwe gumzo?

Nahisi kuna watu wanataka kuwavuruga waislam wa Zanzibar au kuanzisha mjadala huu ili baadae walipitishe maana ni dhahiri kuwa ile kuswali kufuata uislam na idadi ya waislam wa Zanzibar ina waumiza.

Labda tuzungumze upande wa pili huenda ni kweli Sheikh Soraga ameandika maana hawa BAKWATA kutumiwa ni raisi sana (Naomba wanisamehe kwa kauli hii lakini ndio ukweli) watakuwa wameambiwa na mtu mmoja mwenye hela ambae huwapa vijisenti sasa wamelileta hili. Wakasahau kuwa ikiishakuhusu swala atawaambia hata adhana na kwenda msikitini pia inamkera maana inaonesha haridhiki na uislam kabisa. Inakuwaje asichukizwe na adhana ambayo hutolewa kwa nguvu na kuna wakati mtu hugeuka kulia na kushoto ili kutawanya sauti. Aje achukizwe na nyiradi ambazo husemwa na imam mara moja tu na wengine kufuatiliza kwa mdomo.

Naomba BAKWATA wawe wanafikiria kidogo kabla ya kuamua jambo. Kwani huko kuna matamasha ya filamu na mziki ambayo yanakesha usiku kucha na sijasikia malalamiko. Mi nina uhakika wameanza hapo ila watakuja mpaka kwenye adhana.

Tangazo/Barua ya katibu wa mufti Zanzibar



DAR ES SALAAM MPAKA ZANZIBAR SASA KWA BARABARA


Picha(maktaba)

BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.

Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara na Unguja, kwa upande wa Zanzibar.

Umbali kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni kilometa 73.43, sawa na maili 45.62 hivyo kuwapo kwa mradi huo ni jambo linalowezekana, kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.

Kwa sasa, daraja refu kabisa duniani ni lile la Danyang–Kunshan lililopo China ambalo lina umbali wa kilometa 165, sawa na maili 102.4. Daraja hilo lilifunguliwa Juni mwaka 2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau wakati alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda ambaye alitaka kufahamu kama kuna matarajio ya kujenga daraja kubwa zaidi, ikiwezekana la kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema wapo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ambapo mazungumzo hayo yakienda sawa, ujenzi wa daraja hilo huenda isiwe ndoto, bali ukweli.

"Hilo wazo lipo mheshimiwa na tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali, kwa hiyo hilo wazo lipo na sisi tulilifikiria," alisema Dk Dau.

Kamati hiyo ilifanya ziara katika miradi mikubwa mitatu ya shirika hilo ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi na 'Dege Eco village' ambao una nyumba zaidi ya 7,000.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mtanda alisema, kamati yake imeridhishwa na miradi hiyo ya NSSF ambayo inaendelea huku akitaka kuongezwa kwa kasi ili watanzania waanze kunufaika na miradi hiyo.

"Muangalie na hilo la ujenzi wa daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na mradi wa makazi bora na salama ambao utaweza kubadili taswira ya Jiji la Dar es salaam," alisema.

Alisema kamati yake isingependa kuona changamoto zozote ambazo zinaweza kukwamisha miradi hiyo na kwamba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaangalia namna ya kuunganisha miundombinu karibu na miradi hiyo.

"Lakini pia tumesikia kuwa serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi, tunashauri serikali kuilipa mifuko hii ili kuifanya kuwa na nguvu na kuweza kuleta maendeleo," alisisitiza Mtanda.


NDUMBARO ATEMA CHECHE

Kampuni ya Mawakili ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ambayo inawakilisha vilabu 13 vya LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA, inapenda kutoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:

Kampuni ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, iliteuliwa na vilabu 13 vya LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA, kwa maandishi, ili kuwawakilisha na kuwatetea katika kudai haki zao ambazo tayari SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF) liliamua kukata fedha za udhamini na viingilio vya mechi pasipo kuwashirikisha. 
 
Dk. Damas Daniel Ndumbaro, wakili mwandamizi, ndiye aliyekabidhiwa file hilo kwa mujibu wa utaratibu wa ofisi yetu.
Kwamba, tarehe MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, kupitia wakili wake mwandamizi, Dk. Damas Daniel Ndumbaro, iliandika barua ya madai (Demand Notice) TFF na kuongea na waandishi wa habari.
 
Kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Juma Nkamia (MB) aliitisha mkutano kati ya TFF (ambayo iliwakilishwa na Wilfred Kidau-Mjumbe Kamati ya Utendaji, na Selestine Mwesiga, Katibu Mkuu), Bodi ya Ligi, Vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na Dk. Damas Daniel Ndumbaro (kama wakili wa vilabu). 
 
Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mh. Juma Nkamia alitoa fursa kwa TFF, Bodi ya Ligi, na Wakili wa vilabu kutoa maelezo yao na hatimaye Mh. Juma Nkamia alitoa maelekezo kama ifuatavyo:
 
Jamal Malinzi sio Rais wa Nchi, na aliwaagiza wawakilishi wa TFF wafikishe ujumbe huo kwa Bw. Jamal Malinzi. Makato ya Tshs. 1000/= kwa kila tiketi ni wizi wa mchana.TFF isitishe makato ya 5% na Tshs. 1000 kwa kila tiketi mpaka watakapoongea na kukubaliana na vilabu.
 
Baadaya hapo, MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ilikutana na vilabu ambayo vilikuwepo siku hiyo na kukubaliana kuwa sasa tusibiri majadiliano na TFF na kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ikiongozwa na Dk. Ndumbaro iandae mapendekezo ili yajadiliwe na mkutano mkuu wa vilabu.
 
Kwamba tarehe 11 Oktoba 2014 TFF ilifanya mkutano wa Kamati ya Utendaji na kutoa tamko kuwa kumekuwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni za ligi kuu na kwamba Sekretariati ya TFF imefungua mashtaka dhidi ya Dk. Ndumbaro ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba.
 
Kwamba Kamati ya Utendaji ya TFF iliendelea kusema kuwa Kutokana na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla na kwamba.
 
TFF imefanya kosa kumshitaki Dk. Ndumbaro kwa kofia ya Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba kwasababu barua toka MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, barua za vilabu 13 na taarifa kwa vyombo vya habari ilikuwa bayana kuwa Dk. Ndumbaro anawakilisha vilabu vya ligi kuu kama wakili toka kampuni ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES na wala sio mwakilishi wa Bodi au Mwenyekiti wa uchaguzi wa Simba kwasababu hakukuwa na uchaguzi wa Simba.

Kwamba TFF inakiri kuwa klabu za Ligi kuu zinapaswa kukutana na TFF kujadili kasoro za Kanuni za Ligi kuu. Hapa TFF inakiri kuwa haikukutana na vilabu katika mchakato wa kutunga kanuni hizi na kwamba kanuni hizo zinakasoro. Ifahamike kwamba hayo ndio madai ambayo vilabu kupitia MALETA & NDUMBARO ADVOCATES iliyapeleka TFF kwa maandishi.

Tarehe 7 Oktoba 2014 TFF iliepeleka Mshtaka katika Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Ndumbaro. Kamati ya Nidhamu ilipanga kusikiliza Mashtaka hayo tare 09 / 10 / 2014 saa 08: oo mchana, yaani siku mbili tu baadaya ya kuwasilishwa katika kamati ya nidhamu. Mashitaka hayo yalijaa ubabaishaji na chuki binafsi dhidi ya wakili wa vilabu 13 vya Ligi Kuu.

Kwamba TFF ililazimisha kusikiliza mashtaka hayo kwa haraka na dharura ya ajabu pasipo kuwepo Dk. Ndumbaro ambaye alitoa taarifa ya maandishi kuwa atakuwa safarini Nchini Marekani kikazi, kwa barua ya tarehe 8th October 2014.

Kwamba Kamati ya Nidhamu ya TFF ilitoa maamuzi ya kumfungia Dk. Ndumbaro asijihusishe na Soka kwa kipindi cha miaka saba pasipo kutoa sababu za msingi za kufanya hivyo wala kutoa nakala ya hukumu hiyo.

Kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES kwa niaba ya vilabu vya Ligi kuu inapinga adhabu hiyo ya uonevu kwa misingi ifuatayo:-

Kamati ya nidhamu ya TFF haina mamlaka ya kisheria ya kushughulikia suala hili. (ARTICLE 2, 3,76 and 77 of TFF Disciplinary Code) Kamati ya nidhamu ya TFF ilikosea kuamua suala hili bila kutoa haki ya msingi ya kuisikiliza MALETA & NDUMBARO ADVOCATES na Dk. Damas Daniel Ndumbaro
Hakuna Chombo chochote cha TFF chenye mamlaka ya kumzuia au kumfungia Wakili wa kujitegemea kuwawakilisha wateja wake.

MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inaandaa kesi ya madai dhidi ya TFF kwa kuizuia isifanye biashara yake halali.

MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inapenda kuwajulisha wadau wote kuwa kupinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF sio kosa. Ikumbukwe kuwa JAMAL MALINZI aliwahi kupinga maamuzi ya FIFA, CAF na TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013, kwa njia ya Circular Resolution, ili kuunda Kamati za Rufaa ya Uchaguzi, Kamati ya Maadili na Club Lincensing. Lakini leo Jamal Malinzi hataki kupingwa huyu ni dikteta.
 
Kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inaandaa mashtaka dhidi ya Uongozi wa TFF, katika mambo yafuatayo:
Ubadhirifu wa US$ 200,000 fedha za TBL udhamini wa Taifa Stars
Kupinga Maamuzi ya FIFA kurejea Karume ( Haya yalikuwa mapendekezo haikuwa amri) Kufanya matumizi na manunuzi bila kibali cha kamati ya fedha ambayo ndiyo kamati ya manunuzi ya TFF kwa mujibu wa kanuni za manunuzi za TFF, manunuzi yaliyofanyika yanahusiana na Vifaa vya michezo wakati wa maboresho ya Taifa stars, Tiketi za ndege za Taifa Stars, timu ya wanawake na za vijana katika michezo yake na hotel za kambi ya timu ya Taifa ambapo hakukuwa na tenda zilizotangazwa wala ushindanishwaji wa aina yoyote jambo linaloashiria matumizi mabaya ya madaraka na fedha na kwa kuwa Rais ndiye msimamizi wa shughuli za sekretariet kikatiba jambo hili linakuwa pamoja na mengine ni suala la kimaadili kwa sheria za mpira.

Kwamba MALETA& NDUMBARO ADVOCATES inaandaa mashtaka dhidi ya Jamal Malinzi kwa Kupinga Maamuzi ya FIFA, CAF na TFF ili kufanya marekebisho ya Katiba mwaka 2013.
 
Tarehe 21 Oktoba 2014, Dk. Damas Daniel Ndumbaro alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya TFF lakini mpaka sasa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu TFF haijasema lina inakaa. Tunatarajia kuwa haraka na dharura iliyotumika katika kuamua shauri katika kamati ya nidhamu itatumika pia kuamua shauri katika rufaa. Leo ni siku ya 10 toka rufaa ikatwe lakini bado kimya wakati ilichukua siku 2 tu kusikiliza kesi ya msingi.
 
KWAHIYO Dk. Damas Daniel Ndumbaro wa MALETA & NDUMBARO ADVOCATES kwa naiba ya wateja wetu tunasema kuwa:

Tutaendelea na kuwawakilisha wateja wetu kwa uadilifu wa hali ya juu. Kwamba madai yote tuliyoyasema katika barua ya awali dhidi ya TFF ikiwemo madai yanayohusiana na Mkutano Mkuu yapo pale pale.
 
Tumekata Rufaa dhidi ya maamuzi ya kamati ya nidhamu ya TFF kuanzia tarehe 21 Okotba 2014 Tunaandaa mashtaka dhidi ya Uongozi wa TFF kwa ubadhirifu wa fedha za umma Tunaandaa mashtaka dhidi ya TFF kwa kosa la kupinga agizo la FIFA kurejea Karume.
 
Tunaandaa Mashtaka dhidi ya Jamal Malinzi kwa kosa la kupinga Maamuzi ya TFF, CAF na FIFA katika mabadiliko ya Katiba ya TFF mwaka 2013.
 
Wako 
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
For: Maleta & Ndumbaro Advocates
www.maletandumbaroadvocates.com

Nakala: i. Vilabu 13 vya Ligi Kuu
ii. Mh. Naibu Waziri
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Maleta & Ndumbaro Advocates
www.maletandumbaroadvocates.com


BAADA YA LORI KUFELI BREAK USO KWA USO NA SIMBA MTOTO WAMI


Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tanga limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani, Dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.

Kitongoni blog inaendelea kutafuta taarifa zaidi za tukio hilo.

Wednesday, October 29, 2014

ROLI LA MAFUTA LAANGUKA NA KUUNGUA LOTE KIMARA KWA THOMAS

Lori la mafuta limeanguka na kuungua lote eneo la kimara kwa Thomas. Ajali hiyo imesababisha foleni kubwa kwa magari yanayo elekea kimara. Lori hilo limeanguka katika kituo cha magari yaendayo kasi. Hamna mtu alie jeruhiwa au kufa.




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU