Facebook Comments Box

Thursday, October 16, 2014

SIMBA NA YANGA NA IMANI ZA USHIRIKINA WA MVUA

 KIKOSI CHA TIMU YA SIMBA.
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO PATRICK PHIRI.
 KIKOSI CHA TIMU YA YANGA.
WACHEZAJI WA YANGA WAKISHANGILIA MOJA YA BAO LAO.
kitongoni blog:


Mpaka  kwenye  miaka  ya  90  kulekea  mpambano  wa  watani  wa  jadi  kulikuwa  na  imani  za  kishirikiana za mvua  zikichukua  nafasi  kuliko  hivi  sasa, itakumbumbukwa  kwamba  ilifikia  hatua  timu  ya  Yanga  wanapoona  mvua  imenyesha  wao  walikuwa  wakiingiwa  na  hofu  zaidi  ya  kuupoteza mchezo  huo  huku  upande  wa  pili  wa  Simba nao  wakichekelea  kunyesha  kwa  mvua   wakimaanisha  kuwa  lazima  wataibuka  washindi.

Ama  kwa  hakika  tukio hilo  lilikuwa  lina  nafasi  kubwa  kwa  kuwa  kweli  siku  ya  mpambano  huo  kama  mvua  haikunyesha  Simba  walifungwa  au  kutoka  sare  na  pale  iliponyesha  mvua  tu  ni  lazima  Yanga  wangefungwa.

Lakini  kunako  miaka  hii  ya  2000  mambo   sasa  yamebadilika  na  yeyeto  Yule  anaweza  kupata  ushindi  katika  hali  yoyote  ile liwake  jua  ainyeshe  mvua,  na  hili  ndiyo  miongoni  mwa  mambo  yanayozidi  kuupa  ladha  mchezo  huu  kuwa  vigumu  kupata  utabiri  wa  nani  mshindi. 

Jambo lingine  ni  zile  kambi  zao  ambazo  kama  Yanga  wakitokea  Pemba  au  Bagamoyo   Mbegani  huwa  wana  uhakika  zaidi  wa  kupata    ushindi  kuliko   kuweka  kambi  yao  Jijini  Dar  es  salaam,  wakati  Simba  wao  huwa  wana  uhakika  zaidi  wa  kupata  ushindi  kama  tu  wametokea  Unguja  au  Dar  es  salaam  maeneo  ya  Bamba  Beach. 

Katika  mechi  hii  kambi  za  timu  zote  hizo  hazikuwa  kwenye  sehemu  zile  zilizo zoeleka  na hali  hiyo  imefanya  kuwa  na  tambo  nyingi  kutoka  kwa  mashabiki  wake  na kila  upande  kuamini  kuwa  wataibuka  washindi.

Jicho  la  kitongoni blog litakuwepo  kukujuza  kila  kitu  ambacho  kitatokea  ikiwa  ni  pamoja  na  visa na  vibweka  vyote  vitakavyojiri  uwanja  wa  Taifa  tarehe  18/10/2014, Jumamosi.




 



Wednesday, October 15, 2014

RAIS KIKWETE AWASILI DODOMA KWA AJILI YA VIKAO VYA CHAMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya CCM. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watatu kushoto ni Makamu wa CCm Bara Ndugu Philip Mangula.
Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Dodoma wakimvika skafu na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo anatarajiwa kuongoza vikao vya ngazi ya juu vya CCM, picha na Freddy Maro.






Tuesday, October 14, 2014

SOMA MAGAZETI YA LEO






KANISA KATOLIKI LAJADILI KUHUSU WAPENZI WA JINSIA MOJA

Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa 

Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.

Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.

Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.

Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu mapema mwezi huu,katika mkutano huo ni papa Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.

Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi suala la wapenzi wa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.

Mwaka uliopita katika ripoti aliyo itoa papa Francis kuhusiana na mwenendo wa kanisa katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha mkono kanisa hilo kutokana na mafunzo yahusianayo na ngono na dawa za uzazi wa mpango.

Papa huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja kama zisizo na utaratibu akiinukuu ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa mwaka 1986,wakati Papa Francis alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya kanisa katoliki wa hayati papa John Paul wa pili.

Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu ya kauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa jana alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro alitoa kauli kua kama mtu anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni nani wa kuhoji?

Papa Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni kutumia jina (hasha kum si matusi) WASENGE hadharani kuliko kutumia neno wapenzi wa jinsia moja.

CHANZO: BBC SWAHILI


Monday, October 13, 2014

TETESI ZA KUCHINJWA WATOTO TABATA: WAZAZI WAKUSANYIKA SHULE YA MSINGI TABATA

Kutokana na tetesi za kuwa watoto watatu wa shule ya msingi tabata kutekwa na kuchinjwa wazazi wamekusanyika katika shule ya msingi tabata. Katika eneo hilo kuna shule za msingi tatu zilizopo pamoja.

Wazazi wamejaa hapo baada ya kupata taarifa kuwa gari aina ya Noah ambayo inatumika kuwakamata watoto imeshikwa na walimu na ipo hapo shuleni.

Kuna baadhi ya wazazi wanawataka watoto wao warudi nao nyumbani. Ni muda sasa kumekuwa na tetesi za watoto kushikwa na kuchinjwa na Noah yenye vioo vyeusi. Kwa leo wazazi wamekusanyika baada ya uvumi kuzagaa kuwa watoto watatu walio kamatwa na Noah hiyo wamechinjwa.


Kitongoni blog wakati inafika eneo la shule ilikuwepo noah ambayo ni nyeusi ya mmoja wa walimu na huja nayo shuleni hapo kila siku za kazi. Mwalimu mkuu ameahidi kutoa maelezo kwa wazazi baadae.

Sunday, October 12, 2014

MECHI YA MASHEIKH WA BAKWATA NA VIONGOZI WA KIKRISTO YAMALIZIKA

Mh Mizengo Pinda akiongea
Mechi ya kudumisha amani na mshikamano baina ya Viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo, imekwisha kwa timu ya Amani kuifunga timu ya Mshikamano kwa goli moja kwa bila.

Mechi hiyo iliyochezwa kwa dakika 30 kwa kila kipindi, goli la timu ya Amani lilifungwa katika dakika za mwisho za mchezo huo na timu zilikuwa mchanganyiko bila ya kuweka watu wa dini moja kuwa timu moja.

Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Mheshimiwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.

Refarii wa mchezo huo alikuwa Kamanda wa polisi kanda maalumu Dar es Salaam, zawadi kwa Mshindi wa kwanza na wa pili zilikabidhiwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza Kepteni wa timu ya Amani Sheikh Alhad Mussa aliyefahamika kwa
jina la muda katika mchezo huo 'Jaja', ndiye aliyekabidhiwa kombe na Waziri Mkuu.

Pambano hilo litafanyika kila mwaka na kufahamika kama 'Amani Cup'.


Saturday, October 11, 2014

WATU SABA WACHOMWA MOTO KWA TUHUMA ZA UCHAWI


Moja ya nyumba zilizoteketezwa katika Kijiji cha Murufiti ambapo watu saba waliuawa kwa kuchomwa moto. Picha na Diana Rubanguka.
Na Diana Rubanguka na Antony Kayanda, Mwananchi

Kigoma. Watu saba wameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba katika tukio ambalo nyumba 18 ziliteketezwa na mbili kubomolewa na wananchi waliodai wanawaua wachawi katika Kijiji cha Murufiti, Kasulu, mkoani Kigoma.
Polisi wameeleza kuwa tayari watu 17 wamekamatwa kwa kuhusika kwenye tukio hilo.Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo lililotokea

Jumatatu iliyopita ni John Mavumba (68) na mkewe Elizabeth Kaje 55 ambao pamoja na wenzao walikuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Josephat John ambaye ni mtoto wa Mavumba, alisema wazazi wake walichomwa moto na kundi la vijana waliokuwa wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.

Alisema vijana walikuwa wamebeba mapanga, marungu na kupita katika nyumba mbalimbali wakifanya mauaji wakisema maneno kwa kurudiarudia kwamba watawamaliza wachawi kwa kuwaua, ndipo yeye na wenzake walikimbia usiku huo wakihofia kuuawa.

“Niliporudi alfajiri niliukuta mwili wa mama ukiwa umbali wa mita 10 kutoka ilipo nyumba yetu ukiwa umeungua na mwili wa baba ukiwa umeungua ndani ya nyumba,” alisema John.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed alisema mauaji hayo yalitokea Oktoba 6 kuanzia saa 4:00 usiku katika kijiji hicho. John alisema baada ya tukio hilo wanaume wengi wameyakimbia makazi yao wakihofia kuuawa na kundi la vijana hao. “Kijiji kimebaki na wanawake tu, wanaume wamezikimbia nyumba zao wanahofia kuuawa,” alisema.

Mohamed alisema mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina.

Aliwataja waliouawa kuwa ni John Muvumba (68), Elizabeth Kaje (55), Dyaba Kitwe (55), Vincent Ntiyaba (42), Herman Ndabiloye (78), Redempta Mdogo (60) na Ramadhan Kalaliza (70) wote wakazi wa kijiji hicho.

Alisema nyumba zilizochomwa moto ni 18, mbili zilibomolewa na kufanya jumla ya nyumba 20 zilizoharibika kabisa.Wakazi wa kijiji hicho, Zablon Andrew na Eveline Enock walisema kwa nyakati tofauti kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mganga wa jadi aliyefika kijijini hapo na kupiga ramli akiwataja watu waliouawa kuwa ni wachawi.Andrew alisema baada ya mganga huyo kuwataja, vijana walikusanyana na kuanza kuwateketeza watu bila huruma.

“Kitendo hiki kimeturudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu nyumba zetu zimechomwa moto na mazao yetu yameharibiwa,” alisema Andrew.

Hali ilivyo kijijini

Mmoja wa watu aliyechomewa nyumba, Evelyne Msilu alisema sasa kijiji hicho kina askari wengi wanaofanya doria. “Hali inasikitisha, tumepoteza ndugu zetu waliouawa, wanaume
wengi wamekikimbia kijiji kwa hofu ya kuuawa na vijana wengine wamekimbia
wakiogopa kukamatwa,” alisema.

Kwa nini ipigwe ramli?

Akisimulia, Enock alisema kuna kijana mmoja katika kijiji hicho ambaye kazi yake ni kufyatua matofali aliwaomba vijana wanzake kuwa siku inayofuata wamsaidie kuyapanga katika tanuru. Alisema jambo la ajabu ni kwamba walipoamka asubuhi walikuta matofali yamekwishapangwa na haikujulikana aliyefanya kazi hiyo.

Alisema kijana huyo na wenzake waliamini kwamba waliofanya kazi hiyo ni wachawi. Akisimulia kisa kingine, Enock alisema siku chache zilizopita kuna msiba ulitokea kijijini hapo na baada ya mazishi, siku iliyofuata walikuta msalaba umeng’olewa na haujulikani ulipo, jambo ambalo pia
lilihusishwa na ushirikina.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Ogen Gasper aliyeomba Serikali kujenga kituo cha polisi kijijini hapo, alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifanya jitihada kubwa kuwapata askari, lakini hawakufika kwa kilichodaiwa ni kukosa usafiri.

Gasper alisema hilo ni tukio la tatu kwa watu kuuawa kwa kutuhumiwa kuwa ni wachawi, la kwanza likiwa limetokea mwaka 1996.


CHANZO: MWANANCHI

TIMES FM WATOZWA FAINI KWA WATANGAZAJI WAKE KUTUMIA MANENO YASIYO NA STAHA

Kituo cha Redio cha Times FM kimetozwa faini ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni moja na kupewa onyo kali kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya TCRA, Margareth Munyagi, alisema ‘Times FM’ imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua Tatu’ kinachosikika saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani’, kilichosikika mchana wa Agosti 29, 2014, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono, na kukiuka maadili ya utangazaji..

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri lakini kinyume chake, zilitangazwa muda ambao vipindi hivyo vingeweza kusikilizwa pia na watoto.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao. Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri. 

Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.


BENIN WATUA NCHINI TAYARI KUIKABILI STARS




BENIN YATUA NCHINI TAYARI KUUMANA NA TAIFA STARS JUMAPILI HII
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.

Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.

Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg, Austria), Sessi D'almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa). 


(P.T)Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).

Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).

Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.

Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.

Chanzo:Shaffihdauda.com


CBA YAFANYA VIZURI IKISHIRIKIANA NA VODACOM

Huduma ya M-PAWA inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianzishwe.

Pamoja na fedha hizo huduma hiyo imewezesha kuwepo na amana za shilingi bilioni 6 kutoka kwa wateja laki 7 ambao wanapata huduma ya M-Pawa,Taarifa hiyo ya mafanikio imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Julius Mcharo akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika Kariakoo.
 

Mcharo alisema huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na Vodacom imepata muitikio kutokana na watanzania kuweza kufungua akaunti za huduma hiyo mahali popote pale walipo kwa kutumia mtandao.

Alisema huduma hiyo ambayo pia inawezesha kupatikana kwa mikopo na kupokea na kulipa huduma mbalimbali kwa m-pesa imerahisisha maisha ya wananchi wengi na kusema kwamba itaendelea kuboreshwa na kutanuliwa.

Akizungumzia wiki ya huduma kwa wateja alisema kwamba watendaji wote wa benki hiyo wanakwenda katika matawi yapatayo 11 nchini kote kutoa huduma kwa karibu zaidi na wateja wao kwa lengo la kufahamu changamoto zao.

Alisema changamoto hizo zitawawezesha kutambua mahitaji halisi ya wateja na kutengeneza bidhaa zinazolingana na mahitaji yao.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo watatu kutoka kushoto akiwa na wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la k.koo




Wednesday, October 8, 2014

BABA ATELEKEZA WATOTO WACHANGA HOSPITALI BAADA YA MAMA KUFARIKI

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Aison Majiyatamu mkazi wa Nankukwe Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya anatafutwa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha Ustawi wa Jamii kwa kutelekeza watoto wake Hospitalini.

Akizungumzia kisa hicho, Afisa Ustawi wa Jamii, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Annah Geretha, alisema wanalazimika kumtafuta mzazi huyo kutokana na kutoonekana Hospitali hapo kufuatilia maendeleo ya watoto wake kwa muda mrefu tangu walipozaliwa.

Alisema Mama mzazi wa watoto hao ambao ni mapacha wa kike aliyejulikanakwa jina la Edah Simia alifariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua watoto hao salama kabisa ambapo mume aliuchukuwa mwili wa marehemu kwa lengo la kwenda kuzika kijijini kwao "Namkukwe" lakini tangu kipindi hicho hakurudi tena.

Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu ambapo tangu kipindi hicho watoto wamekuwa wakihudumia na kuhifadhiwa kwenye chumba cha joto katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.

Alisema lengo la kuwatafuta ndugu wa watoto hao ni kutokana na muda wa kuendelea kukaa kwenye chumba cha joto umepitiliza kutokana na umri wao hivyo wanashindwa kuwatoa kwa sababu hawana mtu wa kuweza kuwahudumia nje ya chumba hicho kutokana na uhaba wa wauguzi unaoikabili hospitali hiyo.

Alisema yoyote atakayekuwa na taarifa za ndugu wa marehemu ama baba wa watoto hao atoe taarifa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya au Hospitali ya Wazazi ya Mbeya.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU