Facebook Comments Box

Saturday, June 14, 2014

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 14 JUNE 2014



RAIS WA KENYA IPELEKA HARAMBEE STARS BRAZIL

Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta akitoa hotuba yake katika Ikulu ya Nairobi wakati wa hafla ya kuiaga timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars aliyoipa ofa ya kwenda ziara ya mafunzo kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil

Rais Kenyatta akiongea na wachezaji wa Harambee Stars



Rais Kenyatta akigawa tiketi kwa wachezaji huku akishuhudiwa na mkewe Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto)


Rais Kenyatta, mkewe Mama Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko wakipozi Ikulu ya Nairobi na Harambee Stars wakati wa hafla hiyo fupi ya kukabidhi tiketi za ndege za kuendea Brazil kuona kombe la dunia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia 
Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil. 
Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.
Mmoja wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao. Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano, malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama. 
Hatua ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi sana nchini Kenya kwa kuwa timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu kushiriki michuano hiyo, sasa wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya. 
Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa kima cha dola elfu arobaini. 
Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa. 
Kenyatta mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil. Ufadhili huu unakuja miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo. 
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 Julai.
CHANZO:BBC


NYUMBA YA BALOZI WA MSUMBIJI TANZANIA YAUNGUA

Habari zilizotufikia ni kwamba nyumba ya balozi wa Msumbiji iliyoko maeneno ya Masaki imewaka moto. Habari zinaendelea kutupasha kwamba fire walifika lakini maji yalikuwa kidogo.


UHOLANZI WAIPA UISPANIA KIPIGO CHA MBWA MWIZI.

Van persie akishangilia kwa kugonganisha mikono na kocha wake
Magoli mawili  yaliyofungwa na Van persie na mawili yaliyofungwa na roben na moja la vrij yaliyosha kabisa kuisambaratisha uhispania japo wao ndio walikuwa wakwanza kupata goli kwa njia ya penati.
Timu ya uhispania ndio ilitabiriwa na wengi kuonesha mpira mzuri na kuchukua kombe ila kwa jana wengi wanasema huu ndio mwisho wa utawala wake kisoka na wanaipa nafasi kubwa uholanzi.
 
Van persie akifunga goli kwa kichwa cha kuchumpa watu wanakifananisha na ndege kubwa za mizigo na watu ikiwa inaruka



BOMU LAUA MTU MMOJA KWENYE DAURA ZANZIBAR

Hii ni picha ya mtu anaesadikiwa kufa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kurushwa zanzibar.eneo la darajani kulikokuwa kunafanyika daura ya masheikh wa Afrika mashariki. Inasemekana huyu aliekufa ni mwanafunzi wa sheikh Quasim Mafuta Qaasim wa tanga na sheikh mwenyewe kaumia mkono na mguu kulikuwa na sheikh mwingine kutoka kenya ambae hakupata madhara yoyote. Tunamtakia apone mapema. Na marehemu Allah amuhifadhi.
Inna lilayh wa inna ilayhi rajiuun 


Friday, June 13, 2014

PICHA: AJALI ILIYOTOKEA MOROCO MCHANA WA LEO

 
Baadhi ya Watu wakitazama ajali ya magari mawili kama yaonekanavyo pichani,iliyotokea mapema leo eneo la Moroco-Posta jijini Dar,katika ajali hiyo ambayo chanzo chake hakikufahamika mara moja,mtu mmoja alijeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha.



Mama ambaye jina lake halikufahamika mara moja moja aliyekuwa kwenye gari lenye usajili wa namba T679 CKC,akipewa huduma ya kwanza mara baada ya kupoteza fahamu



Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani



Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani,huku abiria wake mmoja akiwa amepoteza fahamu,kama aonekavyo kwa mbali



Majeruhi akipewa huduma ya kwanza na mmoja wa akina mama aliyekuwa akifanya usafi kando kando ya barabara mapema leo asubuhi,katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.

NAKUMATT WAUZA VITU NUSU BEI MLIMANI CITY MUDA HUU

Baada ya kununua duka la shoprite Nakumatt wameamua kuuza bidhaa zote zilizokuwepo ndani kwa nusu bei. Kwa mfano sukari kilo moja inauzwa elfu moja na hamsini. Hii imevutia watu wengi na kujaza duka hilo hii leo.

 



Thursday, June 12, 2014

PAUNDI MILIONI 30 ZAMPELEKA FABREGAS CHELSEA

Wakati watu wakiwa na hamu kubwa na shauku ya kujua nini kitatokea leo usiku katika ufunguzi wa kombe la dunia kocha mwenye maneno mengi na machachari Jose Mourinho maarufu kama special one kafanya yake kwa kusajili kiungo wa Barcelona fabregas kwa paundi za uingereza milioni 30.



KIBONZO: LIFT YA KWANZA MKOANI MBEYA




CHINA YAKATAZA MATUMIZI YA WINDOW 8 KWENYE COMPUTER ZA SERIKALI PAMOJA NA TAASISI ZAKE

Katika wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na China , Serikali ya Marekani inailaumu china kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni zake na biashara nyingine huku china nayo ikiilaumu marekani. China baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo.

Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS (China Operating System) kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .

Suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita huko ulaya , lakini umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya

Kitu kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .

Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote.

Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni , ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani .

TAHADHARI YA PICHA: ASKARI AUAWA KINYAMA KWA KUKATWA NA MAPANGA KIMANZICHANA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi (SACP) Ulrich Mtei


Marehemu Joseph Ngonyani:
 huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzichana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.

Jambo la kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye
silaha ambaye amefahamika kwa jina la Joseph Ngonyani na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30.

Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. 

Askari Ngonyani alifariki alipokuwa anapatiwa matibabu
kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye Venance amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.

Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye Veronica Musime, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU