Facebook Comments Box

Tuesday, May 6, 2014

MSIBA WA USTAADH ILUNGA WAINGIA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA

Katikati ni Sheikh Ilunga na pembeni ni.Salum Ally Mkangwa na nyuma ni Mohamed Said picha ilipingwa CBE mwaka 1988.
Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kaingia katika historia ya Dar es
Salaam katika kifo chake. Bahari ya watu walijazana Msikiti wa
Kichangani kuja kuswalia jeneza lake na kisha kulifata nyuma jeneza
hilo hadi Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa. Sheikh
Ilunga ni mgeni katika mji wa Dar es Salaam kwa maana ya kuwa
hakuzaliwa Dar es Salaam wala hakuwahi kuishi Dar es Salaam.
Alikuwa akija na kuondoka zamani akirejea kwao Tabora na baadae
baada ya kuhamia Mwanza, akija Dar es Salaam na kurejea
Mwanza. Iweje leo mji mzima wa Dar es Salaam usimame na utoke
kuja kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu? Hakika hili ni swali
linalotaka majibu ya kuridhisha. Jibu ni dogo na rahisi sana. Hivi
ndivyo Waislam wa Dar es Salaam wanavyofanya kila wanapofiwa
na kipenzi chao. Labda linaweza kuja swali jingine, ''kipenzi?''
Sheikh Ilunga kawaje kuwa kipenzi cha Waislam? Naam Sheikh
Ilunga Hassan Kapungu juu ya udogo wake wa umri alikuwa kipenzi
cha Waislam si Waislam wa Dar es Salaam peke yake. Sheikh Ilunga
Hassan Kapungu alikuwa kipenzi cha Waislam wa Tanzania nzima.
Kibla cha kila msikiti wa Waislam katika Tanzania kilikuwa
kinamkaribisha kama si kuwaidhi basi angalau asimame awasalimie
nduguze Waislam. Sheikh Ilinga Hassan Kapunga hakuwa katika lile
kundi la mesheikh ambao wao wenyewe kwa hofu tu kuna baadhi ya
misikiti wanaogopa si kuingia kuswali, bali hata kupita nje. Sheikh
Ilunga hakuwa katika lile kundi la masheikh wenyeji katika futari za
serikali ''misikiti ya wakubwa'' na shughuli zinazohusiana na mambo
kama hayo lakini wageni katika misikiti ya ndugu zao Waislam.
Kubwa Sheikh Ilunga hakukosa usingizi kwa kukosa kualikwa futari
Ikulu au kualikwa katika dhifa za serikali akapigwa picha na
waheshiwa na kutokea katika runinga na magazeti siku ya pili
ukurasa wa mbele. Sheikh Ilunga Hassan Kapungu
hakushughuliswa na hayo. Yeye alishughulishwa na kuliweka juu
jina la Allah Subhana Wataala. Hili ndilo lililokuwa likimshughulisha
mpaka siku Allah alipomfisha. Sheikh Ilunga kaweka historia katika
historia ya mazishi makubwa Dar es Salaam, historia inayokwenda
nyuma kiasi miaka takriban 100 ukianzia mazishi ya Sheikh
Mwinyikheri Akida sheikh aliyeasisi Msikiti wa Mwinyikheri Akida,
Kitumbini unakuja kwa Sheikh Idrissa bin Saad Khalifa wa Tariqa
Askariyya, kisha Sheikh Kaluta Amri Abeid, halafu Abdulwahid
Sykes, kisha Sheikh Kassim bin Juma, halafu Prof. Kighoma Ali
Malima unaishia kwa Mzee Kitwana Dau baba yake Dk. Ramadhani
Dau. Iweje Ilunga kijana mdogo mno aungane na majina ya watu
maarufu kama hawa na katika hao wote walikuwa katika umri
mkubwa ukimtoa Abdul Sykes? Kitu kimoja ndicho
kilichompandisha daraja Ilunga katika jamii ya Kiislam Tanzania.
Ilunga alikuwa mtumishi wa Waislam. Wakimtuma Ilunga kila kazi
na akiifanya kwa moyo mkunjufu, kuanzia kujenga madras na shule
kisha akawasomeshea na watoto wao hadi siku aliposimama
Ukumbi wa Diamond kuitahadharisha serikali kuwa kuna
''Mfumokrsisto'' nchini unaotawala na kudhulumu haki za Waislam.
Hii ilikuwa mwaka 2012. Nilikuwa mmojawapo wa Waislam
waliokuwa pale ukumbini kushuhudia kitendo kile cha kihistoria.
Kwa nini nakiita kitendo cha kihistoria kwa kuwa kwa takriban miaka
40 Waislam walikuwa wanasemea pembeni. Wakati ulikuwa umefika
Waislam wakasimama kuitahadharisha serikali kuhusu kujiachia dini
moja ikahodhi fursa zote za nchi kwa hila na Radio Imaan na TV
yake vilikuwapo na Radio Imaan ilirusha hafla ile na mubashara,
yaani ''live.'' Kote Radio Imaan ilikosikika Waislam walimsikia Sheikh
Ilunga akieleza nini Waislam walifanya katika Tanganyika wakati wa
kupigania uhuru kuuondoa dhulma na kuleta haki kwa kila
mwananchi. Hili lilikuwa jambo kubwa na zito kwa serikali yoyote ile
kuwa inashutumiwa kwa kulea udini ndani ya serikali. nchi nyingi
Afrika zimeangamia kwa ugonjwa huu. Vyombo vyote vya habari
ukitoa vile vya Kiislam viligoma kabisa kuitaarifu jamii kuhusu
kongamano hili la Waislam. Ikawa kama vile hapajapatapo kutokea
kitu chochote. Kuanzia siku ile Sheikh Ilunga alitembea nchi nzima
na kufanya mikutano ya hadhara kuitahadharisha kwanza serikali
kuhusu Mfumokristo na pili Waislam ili wajue nini kilikuwa
kinawatafuna.

Profesa Lipumba akisali nje baada ya kukosa sehemu ya kusali ndani ya msikiti
Mohamed Said anaelezea alivyomjua Ustaadh Ilunga
Nilimfahamu vipi Sheikh Ilunga Hassan Kapungu? Nilianza kuzisikia
sifa zake katika miaka ya 1980 kabla sijauona uso wake. Wkati ule
Sheikh Ilunga alikuwa kijana mdogo sana na mdogo kwangu kwa
miaka kadhaa. Wakati naingia kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam Ilunga alikuwa maarufu pale chuoni msikiti wa Muslim
Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD)
kiasi unaweza ukadhani kuwa na yeye ni mwanafunzi. Ilikuwa Ilunga
na wenzake ndiyo walioleta ''documents'' za Mzee Bilali Rehani
Waikela MSAUD. Hizi ''documents'' zilikuwa zimefichwa Tabora kwa
karibu miaka 20. Katika ''documents hizi,'' kulikuwa na kisa kizima
cha kile kilichokuja kujulikana kama ''Mgogoro wa East African
Muslim Welfare Society (EAMWS),'' Ndani ya jalada lililofikishwa
MSAUD kulikuwa na ''minutes,'' za mikutano ya EAMWS, taarifa ya
Kamati ya Upatanishi iliyokuwa inajaribu kupatanisha kati ya kundi
la Adam Nasibu na wenzake waliokuwa wanaipiga vita EAMWS,
kulikuwa na ''cuttings'' ya magazeti ya ''Uhuru,'' ''Nationalists'' na
''Tanganyika Standard,'' magazeti makubwa ya zama zile yaliyokuwa
yakifuatilia kwa karibu sana mgogoro ule. Nyaraka hizi za Mzee Bilal
Rehani Waikela zilikuwa hazina kubwa. Kutokana na nyaraka hizi
ndipo ukweli wa nini na nani alikuwa nyuma ya kuvunjwa EAMWS na
kuundwa kwa BAKWATA. Lakini kubwa zaidi waliokabidhiwa
Nyaraka za Waikela walizileta zikiwa na maelezo ili maelezo yale
yaenda na kile kitakachosomwa ndani ya jalada. Ilunga alikuwa
kijana wa Mzee Waikela. Katika hali ya unyonge sana walikuwa
wakiendesha shule ya Nujum katika juhudi za Waislam kujitoa katika
dhulma ya elimu. Mzee Waikela alimsomesha vyema Ilunga kuhusu
fitna na chuki ya Nyerere kwa Uislam na Waislam na mbinu
zinazotumika kuudhalilisha Uislam. Bilali Rehani Waikela alikuwa
mmoja wa waasisi wa TANU Western Province mwaka wa 1955 na
ni yeye na wenzake ndiyo waliomleta Nyerere Nyerere na Bi. Titi
Mohamed kuja kuitia nguvu TANU Western Province. Mzee Waikela
vilevile alikuwa Katibu wa EAMWS Western Province. Mzee Waikela
alikuwa mfano na kigezo kikubwa kwa Ilunga katika maisha yake ya
kuwatumikia Waislam.
msikiti ulijaa hadi nje wakati wa Sala ya jeneza




Monday, May 5, 2014

MAELFU NA KIONGOZI WA SERIKALI WAMZIKA SHEIKH ILUNGA.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif akikaribishwa katika msikiti wa kichangani
Maelfu ya waumini wa dini ya kiislam akiwemo makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif wamehudhuria mazishi ya mwanaharakati na mpiganiaji haki wa kiislam Ustaadh Ilunga Hassan Kapungu.
Chini ni gari la Maalim Seif likiingia viwanja vya msikiti wa kichangani magomeni Dar es salaam

waumini wakizika mwili wa sheikh Ilunga Hassan Kapungu
Jeneza lililombeba sheikh Ilunga likiingizwa msikitini kwa ajili ya Sala ya mwisho


HUU NDIO MSHAHARA WA SENETA MIKE SONKO.



USTAADH ILUNGA HASSAN KAPUNGU AFARIKI DUNIA

Nchi ya Tanzania imezizima kwa huzuni baada ya mwanaharakati wa kiislam Ustaadh Ilunga Hassan Kapungu kuaga dunia jana kwenye saa tano usiku.

Mwili wa marehemu utaswaliwa leo Alasir katika msikiti wa kichangani magomeni. Mwili utazikwa kwenye makuburi ya Mwinyi mkuu

Inna lilayh wa inna ilayhi rajiuun.

Allahuma ghfirlahu warhamhu waskanahu filjannah




Saturday, May 3, 2014

WARIOBA NI "BWANA KERO" KWA SERIKALI TOKEA ZAMANI

Kama alivyoandikika Edson Kamukana katika makala yake moja
"ukiachilia mbali wasomi kadhaa walioamua kulamba matapishi
yao na kumtusi Jaji Warioba na wana-CCM wengi wanaotukana
bila kujua wanamtusi nani, katikati yake utaona wanaosalia si bure
wana jambo na sababu za kufanya hivyo, hawa bila shaka
wanalipa kisasi."
Mnamo tarehe Julai 17, 1997, Rais Mkapa alimteua Jaji Warioba
kuongoza Tume ya Rais (Warioba Commission) kuchunguza na
kubainisha mianya na vyanzo vikuu vya rushwa nchini. Baada ya
kufanya mapitio ya sheria, kanuni na taratibu ndani ya serikali na
kuonyesha mianya ya kukua na kuongezeka kwa rushwa nchini,
Tume ya Warioba ilichapisha ripoti yake (Ripoti ya Warioba) tarehe
7 December 1997.
Baadhi ya mambo ambayo Tume ya Warioba iliyakuta ni pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa umma kuchukua rushwa kama
sehemu ya kujazia mishahara yao (petty corruption) midogo.
Lakini pia Tume ya Warioba ilikuta kuwa kulikuwa na rushwa
nyingine (grand corruption) aka ufisadi iliyohusisha maafisa wa
ngazi za juu na baadhi ya wafanyakazi wa serikali walio na ulafi wa
kujilimbikizia mali.
Tume ya Warioba ilitoa mapendekezo ya hali ya juu yaliyogusa
wizara na idara zote za serikali. Ripoti ya Warioba iligusa mioyo ya
walalahoi na wengi waliotoa maoni ya kumtaka Rais Mkapa
awafikishe mahakamani wale wote waliohusishwa na ufisadi
kwenye Ripoti ya Warioba. Hata hivyo, ripotii hiyo iliwekwa
kabatini na kutiwa kofuli. Ripoti ya Warioba ni imekuwa adimu
sana kupatika ilivyokuwa kwa Hati ya Muungano.
Japokuwa ripoti hiyo iliwekwa kabatini, iliwagusa moja kwa moja
vigogo kadhaa hasa wa CCM na wengi wao au watoto, ndugu na
jamaa zao ndio wanaoshika madaraka leo. Kama mnakumbuka
baada ya ile ripoti, ndipo vyombo vya habari vilianza kuripoti
masuala ya rushwa, ikiwemo ile skendo ya IPTL iliyomfanya
Mwalimu Nyerere aseme kuwa "kama huu ndiyo ushirikiano wa
nchi za kusini, basi bora ukoloni urudi." Waliounga mkono au
kuipinga IPTL wanajulikana. Wengine mtakuwa mnawakumbuka
hata watawala wa miaka hiyo na wizara/idara walizokuwa
wanaziongoza.
Akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Mei 13, 2008, Jaji Warioba
alisema kuwa "Baadhi yetu tumepiga kelele muda mrefu kuhusu
hali ya rushwa nchini mpaka ikafika mahali ikawa watu wanatoa
dhihaka tu. Kuna rafiki yangu mmoja, yeye alinipachika jina la
‘Bwana Kero’ kwa sababu ya taarifa ile ya Tume ya Kero ya
Rushwa. Alisema mimi nimegeuka kuwa kero kwa kuzungumzia
rushwa kila wakati." Bado anaendelelea kuwa "Bwana kero" kwa
kutetea Rasimu ya Katiba Mpya.
Kama alivyouliza Edson Kamukana, inawezekana kweli hao vigogo
au watoto wao, ndugu na jamaa zao walioguzwa moja kwa moja
na ile ripoti wakamsifu "Bwana Kero" wakati alishawaharibia
kitumbua chao? Hatuoni vigogo hao wanautumia mchakato
mzima wa Katiba mpya kama mwanya pekee was kumdhoofisha
"Bwana Kero" na kujaribu kuendelea kuficha madhambi yao
yaliyoyafichuliwa na "Bwana Kero" kwenye ile ripoti yake ya kero
za rushwa 1997?
Kwa wale ambao hawakuwahi kuisoma Ripoti ya "Bwana Kero"
itafuteni muisome halafu muone "kero" ambazo "Bwana Kero"
aliziodhoresha kwenye ripoti yake. Halafu muunganishe the dots
kwa kujiuliza ni kwa nini kigogo A na B au mtoto/ndugu/jamaa wa
Kigogo C "anakereka" sana mpaka kumtusi "Bwana Kero"? Mara
ya mwisho nilisoma muhtasari wa ripoti kwenye maktaba ya
HakiElimu. Ilikuwa imejaa vumbi kweli kweli. Inaitwa " The Report
of the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption",
kwa kifupi "The Warioba Report".
CHANZO: JAMII FORUM


Thursday, May 1, 2014

MBUYU TWITE NAE KUJIUNGA NA AZAM?

Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha
wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa
taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank
Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni
mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi
kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi
kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na
kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu
zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel
Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa
TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya
kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji
hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa
muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa
ajili msimu mpya ujao 2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa
mwishoni waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi
wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia
Yanga na kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa kilichokuwa
kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa
kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo
linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu
Uongozi wa Yanga uliandikia TFF barua mapema kuomba kupewa
mwongozo wa kanuni zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji
wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia Azimio la Bagamoyo
kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji watatu
wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya
utaratibu utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.
Hivyo makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite
na uongozi wa Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya
kanuni zipi zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa
wachezaji wa kigeni na katika hali ya kushangaza Kavumbagu
akaonekana tayari ameshasaini kuichezea timu ya Azam FC.
Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia
alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai
2013, alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na
kilichobakia ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini
Domayo alisema hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja mjomba
wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda
wa mwaka mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa
Young Africans lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walisindwa
kuwa wakweli kwa viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango
yao ya kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini
wachezaji wanaonekana hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga
SC.
Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na
ripoti ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi
zitatolewa hivi karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi kukaa
kwa pamoja na kuafikiana mipango ya msimu ujao.
Aidha uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake,
wapenzi na washabiki wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa
wachezaji hao kwani Yanga bado ina nafasi wachezaji wengi wenye
vipaji na itaendelea kuboresha kikosi chake kwa kuzingatia
maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu ujao.
Kwa maelezo hayo hapo juu inaonesha Mbuyu twite hana nafasi tena maana azimio la Bagamoyo limetiliwa mkazo sana na TFF.
Na kuna habari kocha wa Azam ameuambia uongozi uhakikishe imemsajili 


Saturday, April 26, 2014

WILAYA MBILI KUUNDWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa DarEs Salaam
Said Mecky Sadick.
Wilaya mbili zinatarajiwa kuongezwa na kufanya idadi ya
wilaya kuwa tano katika jiji la Dar Es Salaam. Wilaya hizo
ni Kigamboni na Ubungo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said
Mecky Sadick wakati wa kuhitimisha kikao na baraza la
Mashauri jijini Dar Es Salaam siku ya Jumanne ambapo
wilaya ya Kigamboni itagawanywa na kuwa na majimbo
mawili ya Mbagala na Kigamboni.
“Mapendekezo hayo yatafikishwa kwenye serikali kuu na
uamuzi wake utatolewa mwezi ujao’, alisema Mkuu wa
Mkoa , ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo,
lililokuwa likijadili pia muswada wa bajeti wa mwaka wa
fedha wa 2014/2015.
Wilaya hizo zitaungana na Manispaa za Kinondoni, Ilala na
Temeke za jijini Dar Es Salaam linalokadiriwa kuwa na
watu zaidi ya milioni 4.5 .


MKUTANO WA TAASISI YA DHI NUREYN WAANZA ARUSHA

Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali duniani wamefika jijini Arusha kwa ajili ya mkutano mkubwa ulio andaliwa na taasisi ya Dhi Nureyn Tanzania yenye makao makuu mkoani Iringa.
Taasisi hiyo huji usisha na utoaji wa misaada na uendelezaji wa dini.
Sasa hivi taasisi hiyo inamiliki radio inayosikika mikoa ya nyanda za juu kusini.



Thursday, April 24, 2014

MACHOZI YA SHEIKH HAMID JONGO BUNGENI.


Mashekh wa BAKWATA hakika wana mambo sana.Kuna kitu
kinaitwa ''theatrics,'' masheikh wa BAKWATA ni mabingwa na wana
medali za dhahabu. Sheikh Mkuu wa BAKWATA Shaaban
Simba aliwahi kutoa medali kumpa Reginald Mengi kwa utumishi
wake uliotukuka kwa Waislam. Hakika umma ulipigwa na butwaa.
Umma ukajiuliza. Sheikh Shaaban Simba hajapata kumsikia Sheikh
Hassan bin Amir bingwa wa tafsir ya Qur'an na bingwa wa lugha ya
Kiarabu aliyeandika vitabu lukuki mpaka akapewa shahada ya
heshima na Al Azhar, Cairo mwaka 1964?Ukiachia sifa yake ya
kupigania uhuru wa Tanganyika nk. nk.
Umma ulijiuliza Sheikh Shaaban Simba hajamsikia Sheikh Mohamed
Ayub aliyesomesha dini maisha yake yote na ana wanafunzi Afrika
ya Mashariki nzima na hao wote wanafunzi wake wana vyuo
wanaisomesha Qur'an? Sheikh Shaaban Simba hivi kweli hajapatapo
hata siku moja kumsikia Sheikh Aboud Maalim aliyejenga misikiti
chungu mzima kwa kuwahamasisha Waislam matajiri na masikini
wachangie ujenzi kila mtu kwa uwezo wake alojaaliwa na
Allah? Sheikh Aboud Maalim akaweza kujenga Msikiti wa Manyema,
Msikiti wa Ngazija, Msikiti wa Maamur, Msikiti wa Mwinjuma
Mwinyikambi na mingine tusiyoijua. Achilia mbali kuanzisha
scholarship kwa vijana wa Kiislam kusoma Udaktari na Uhandisi
Uturuki chini ya taasisi aliyoanzisha, Tanzania Muslim Trust Fund.
Sheikh Shaaban Simba hawa wote hakuwaona ila kamuona
Reginald Mengi?
Kwa wasiowajua masheikh wa BAKWATA hakika wanapata tabu.
Kwa wanowajua masheikh wa BAKWATA hawashangazwi.
Wakati mwingine hakika huwa vioja na vichekesho khasa mtu
unatamami kucheka lakini kinachokuzuia ni kuwa jambo lenyewe si
la kuchekesha.
Kuna msemo wa Kiarabu unaosema,''Sababu ikijulikana ajabu
huondoka.'' Naamini Sheikh Jongo anaujua msemo huu.
Sasa hili la kulia Sheikh Jongo ni mlolongo tu wa hizo ''theatrics'' za
masheikh wa BAKWATA.


Wednesday, April 23, 2014

JE, HUU NDIO MWISHO WA WENGER ARSENAL?


Baada ya Manchester United kumfungashia virago kocha wao fununu,tetesi,masikio na macho yote yamehamia  kwa washika bunduki wa London

Wengi wanasema kuwa huu ndio mwisho wa enzi za mzee huyo hapo kilabuni

Baada ya Moyes kuachia ngazi,kocha
anayetajwa sana kurithi mikoba yake ni
boss wa timu ya taifa ya Uholanzi Luis
van Gal. 
Lakini Van
Gal amehusishwa kuhamia Arsenal na
gazeti moja maarufu la kwao uholanzi
liitwalo Vuetbal international state kwa
kutaja sababu kadhaa.

1:Wenger amebakiza wiki 6 tu katika
mkataba wake wa sasa na hajaongeza
bado.

2:Arsenal imemuajiri aliyekuwa msaidizi
wa Van Gal walipokuwa Bayern
Munich. Adries Jonker kama Director
of academy. (Mkurugenzi wa vipaji) hili likitafsiriwa kama
matayarisho ya ujio wa Van Gal.

3:Kama hilo halitoshi,Arsenal pia
imeshawaajiri makocha wadachi wa
vijana wa miaka chini ya 18 na 16 wanaoitwa Jans de kaart
na Luis van Hoon. Kitu
kinachotafsiriwa kwamba ni maandalizi
ya kumnyakua kocha mkuu mdachi.




WANASAYANSI WAGUNDUA MIWANI INAYOGUNDUA MIHEMKO YA MTU.

Mwanasayansi nchini Japan anaitwa Osawa amegundua miwani ambayo imeitwa miwani ya kipelelezi "AgencyGlass"

Wakati akifanya mahojiano na shirika la habari la AFP amesema kuwa "nilikuwa nataka kutengeneza kitu ambacho kitaeleza tabia halisi za kijamii za binaadamu"


organic light-emitting diode (OLED) ambayo imewekwa kwenye miwani hiyo inaunganishwa na kifaa cha kugundua mihemko "emotion" ambacho kimewekwa nyuma kidogo ya miwani hiyo

Mwanasayansi huyo ambae anafanya kazi katika chuo kikuu cha Tsukuba anasem. miwani hiyo itasaidia kugundua wasafiri wakorofi au wanafunzi wakorofi na sehemu ya kazi ambapo mahusiano sio  mazuri

Miwani hiyo ina uzito wa gram 100 na inauzwa  kwa dollar za kimarekani 290.





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU