![]() |
Mheshimiwa Kallaghe akiongea na mwanamuiki wa kitanzania Shilole |
Tuesday, December 24, 2013
Monday, December 23, 2013
BAADA YA KIPIGO: YANGA WAMTIMUA KOCHA WAO
KOCHA Ernie Brandts hana chake tena Yanga na ndani ya siku mbili, uongozi wa klabu hiyo utatangaza kumtimua.
Taarifa za uhakika ambazo blog hii imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza Brandts ameshafukuzwa kazi.
“Kweli Brandts ameonekana hafai na wakubwa walikaa jana kikao mara tu baada ya mechi ya Simba na Yanga, wamefikia hatua ya kumuachisha kazi.
“Mimi ninavyojua tayari mawasiliano na makocha kadhaa yameanza na Brandts atapewa muda kidogo tu ili akusanye virago vyake na kurejea kwao Uholanzi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Lakini viongozi wa Yanga walikuwa wagumu kulizungumzia suala hilo, ingawa mtu mwingine wa karibu na uongozi wa Yanga, alisema huenda leo Yanga wakatangaza.
“Wanaweza kutangaza kesho (leo), nimeelezwa kuwa wamefikia uamuzi huo na kuna bosi mmoja atatangaza leo au kesho,” alisema na kuongeza: “Kama mtaandika wanaweza wasitangaze.”
Brandts amejikuta katika wakati mgumu baada ya kikosi chake kulambwa na Simba kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe iliyopigwa juzi jijini Dar.
Inaelezwa baada ya mechi hiyo, kocha huyo aliyeipa Yanga ubingwa msimu uliopita, alishindwa kuwaridhisha mabosi wake baada ya kuulizwa sababu za kufungwa.
Mbali na Brandts, inadaiwa kuwa uongozi wa timu hiyo una mpango wa kutimua benchi zima la timu hiyo, akiwemo Kocha Msaidizi, Fred Felix Minziro.
Kocha wa sasa wa Mbeya City, Juma Mwambusi, ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Minziro kwenye kikosi hicho cha Jangwani.
Yanga inatarajia kwenda kuweka kambi na inaelezwa zitakuwa nchi kati ya Hispania, Uturuki au Ureno na taarifa zinasema kuwa inataka kwenda na benchi zima la ufundi.
Na katika tofuti ya Yanga wameeleza muda huu kuwa kocha huyo amepewa notisi ya siku thelathini ya kusitisha mkataba wake kuanzia tarehe 22 mwezi huu..
Saturday, December 21, 2013
WAKIWA NA ASILIMIA ZAIDI YA MIA ZA USHINDI YANGA YATANDIKWA 3 KWA 1 NA MAHASIMU WAO BILA YA HURUMA
Timu ya Simba ya Msimbazi Dar es Salaam leo wameonesha kwamba wao sio wa kuchezea japo hawakupewa kabisa nafasi ya ushindi na mashabiki walio wengi.
Simba ailionesha kuwa leo watapoteza mawazo ya mashabiki walio wengi wa Yanga pale ilipojipatia bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka Burundi ambae anaongoza kwa ufungaji wa mabao katika ligi kuu ya Vodacom Amis Tambwe.
Tambwe baadae akaipatia timu yake bao la pili kwa mkwaju wa Penati baada ya Mshambuliaji wao mwenye chenga za maudhi Ramadhan Abdallah Singano 'MESI' kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki wa Yanga David Charles Luhende na mwamuzi kuamuru ipigwe penati.
Simba walipata bao la tatu kutoka kwa mchezaji wao mpya Awadh Juma baada ya kufanikiwa kumpokonya mpira kipa wa Yanga Juma Kaseja Juma aliyetaka kuurudisha mpira ndani ya box ili audake ndipo ukamgonga na mfungaji kuuwahi na kuuweka nyavuni.
Yanga walijipatia bao la kufutia machozi kupitia kwa Emanuel Okwi kwa kichwa baada ya kuwazidi ujajnja mabeki wa timu ya simba ambao leo wamestahili pongezi kubwa kwa kuwa imara tangu mwanzo.
HEBU JIONEE JINSI WANAOBEBA MADAWA YA KULEVYA WANAVYO PASULIWA ILI KUYATOA
Dawa za Kulevya hazifai hakuna asiyefahamu jambo hili lakini unakuta baadhi ya watu wanayaweka maisha yao rehani na kukubali kuwa 'Punda' na kubeba mizigo hii haifai waache mara moja wote wenye tabia hii ni hatari kwa maisha yao.

Picha ya X-ray inavyoonesha tumboni madawa yaliovyo kwa mtu aliyebeba.

Athari inayoweza kupatikana yakiwa mwilini kama unavyoweza kujionea hapo juu.

Operesheni ikifanyika tayari kuyaondoa madawa hayo yaliyo sababisha kijana huyu kufariki.

Utumbo umetolewa tayari ili kuanza kuyatoa madawa hayo.

Kama uonavyo weza kujionea dawa hizo zikiwa ndani ya utumbo mpana.
Dawa zikianza kutolewa pamoja na kushafishwa kama unavyoona katika picha.


Kabla mtu hajazimeza zinakuwa hivi, sasa hebu fikiria mtu anameza kete hadi 5000 hii ni balaa kubwa sana.
Friday, December 20, 2013
RAIS ATENGUA UTEUZI WA MAWAZIRI WANNE WALIOTAKIWA KUJIUZURU NA WABUNGE
Waziri wa Maliasili na Utalii - Mh. Khamis Kagasheki
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Mh. Shamsi Vuai Nahodha
Waziri wa Mambo ya Ndani - Dk. Emanuel Nchimbi
Waziri Mkuu - Mh. Peter Pinda
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini.
Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa,kubakwa,kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, akitoa utetezi wake, akidai kuwa ameonewa na kamwe hawezi kujiuzuru.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa amekutaja kuwa ni muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya kuongea na Rais, Mkuu wa nchi huyo ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika awajibike.
Amesema Rais ameshauri kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe James Lembeli alisema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha. Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba kuundwa tume ya kisheria ya mahakama.
UWANJA WA AMANI ZANZIBAR WAREKEBISHWA NA KUWEKWA NYASI BANDIA
Na Camera ya Kitongoni Mjini Unguja:
Uwanja wa Amani wa Zanzibar maarufu kama Amani Stadium umefanyiwa marekebisho na kuwekewa nyasi bandia.
Baada ya kukamilika ulifanyiwa majaribio kwa mechi ya vijana wa chini ya miaka 20.
Hii ni katika maandalizi ya sherehe za mapinduzi. Uwanja huo umekuwa wa kisasa zaidi kwa wakati huu kama unavyoweza kujionea mwenyewe kwenye picha mbalimbali hapo juu.
Subscribe to:
Posts (Atom)