Facebook Comments Box

Wednesday, December 11, 2013

ABIRIA WA TRENI YA MWAKYEMBE WAANZA KUPITIA MADIRISHANI HEBU JIONEE KATIKA PICHA HAPA

Na Kamera ya kitongoni Blog:
 
Treni inayobeba abiria katika Jiji la Dar es Salaam maarufu kama Treni ya Mwakyembe ambayo inafanya safari zake kutoka Stesheni katikati ya Jiji hadi Ubungo - Maziwa. Imejizolea umaarufu mkubwa katika kuwasaidia abiria wengi wanaopata taabu ya usafiri katika Jiji hili.

Kadri siku zinavyozidi kwenda usafiri huu wa treni umekuwa unapendwa sana na watu walio wengi japo hauwasaidii watu wote ndani ya Jiji hili kutokana na sababu kwamba hauna foleni hivyo kuwafanya watu walio wengi kuwahi kufika nyumbani kwao ukilinganisha na usafiri mwingine wa gari ambapo umekuwa na foleni kila kukicha.

Kutokana na kupendwa huko na watu walio wengi usafiri huu sasa umeanza kuwa wa taabu sana kwa abiria kupanda pindi safari inapotaka kuanza Stesheni. 

Baadhi ya abiria wamekuwa wakipitia madirishani kama ambavyo tumezoea kuona kwenye baadhi ya mabasi ya kubeba abiria maarufu kama 'daladala' hapa Dar es Salaam kama walivyokutwa na Kamera ya Kitongoni hapo jana siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013. 
Abiria wakiwa wamepanga foleni kabla Treni haijafika Stesheni.
Abiria huyu kama unavyomuona hapa akilipigia dirisha hesabu ili apande na kulifanya dirisha ndiyo mlango.


Baada ya kulitathmini dirisha Jamaa aliweza kupanda na kama anavyoonekana akiingia kupitia dirishani na huu sio ustaarabu kabisa.
Abiria wastaarabu wakipanda Treni hiyo kupitia mlangoni kama wanavyoonekana hapo.



MANJI KUTOGOMBEA TENA UENYEKITI YANGA: YANGA YAPATA KATIBU MKUU MPYA

Mwenyekiti wa Young Africans Yusuf Manji leo amemtambulisha rasmi Bw. Beno Njovu kuwa katibu mkuu mpya wa klabu akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua kaimu katibu mkuu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua nae pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka atakapokabidhi kazi rasmi.
Aidha Manji ametangaza mkutano mkuu wa wanachama Januari 19,2013 ambapo wanachama watapata fursa ya kupitia mapato na matumizi,  na ajenda zingine mbalimbali ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo.
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kimemteua Bw.Seif Ahmed "Magari" kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji wa klabu ya Yanga. 
Katika mkutano na wandishi wa habari makao makuu ya klabu Manji ametangaza rasmi kutogombea tena uenyekiti katika uchanguzi mkuu ujao, hili nimeliamua mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa nimefuata demokrasia.
Nina miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani hivyo sasa ninajitahid kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa kama mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania.


Sunday, December 8, 2013

TAASISI YA THE ISLAMIC FOUNDATION YATOA MATIBABU YA MACHO BURE

Taasisi ya The Islamic Foundation imetoa huduma bure ya matibabu ya macho ikiwa inashirikiana na Taasisi ya Al Basra ya Saud arabia.
Huduma hiyo imetolewa katika hospitali ya Aljamiah iliyopo msamvu mjini Morogoro.


HUU NDIO WARAKA WA SIRI ULIOVUJA CHADEMA

Ndugu watanzania, nimelazimika kuusambaza kwa KUUATACH waraka huu wa siri wa mawasiliano ya ndani ya chama baina ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Katibu mkuu, na wanaoitwa wajumbe wa baraza la maamuzi la chama ambao kwa kweli sijafanikiwa kuwafahamu.
Waraka huu nimeuchomoa kwenye file la kazi za kila siku za ndugu HEMEDI SABULA ambaye ni Afisa wa kurugenzi ya ulinzi na usalama wa CHADEMA MAKAO MAKUU.
Ujumbe uliokuwepo ndani ya huu waraka ni wa kusikitisha sana  kiasi kwamba nimeshindwa kuvumilia kuacha kuona watanzania wakiendelea kupotoshwa namna hii.
Tafadhali wanahabari sambazeni ujumbe huu ili watanzania wengi zaidi waweze kuendelea kutambua kinachoendelea ndani ya chama chetu.
Ninaomba niendelee kuficha jina langu kwa sasa
Niiteni mwanamapinduzi mzalendo.
Makao makuu chadema

CHAZO: AUDIFACE JACKSON BLOG



Saturday, December 7, 2013

HILI NDIO BASI LIENDALO KASI LILILO JARIBIWA JANA DAR

Chini ni basi liendalo kasi lililo jaribiwa jana kutoka ofisi za BRT eneo la ubungo plaza mpaka kimara likarudi mpaka kivukoni na kurudi tena ubungo.

Barabara ilionekana ipo safi na mabasi hayo yataanza kuitumia njia hiyo mwaka 2014 itakapokuwa tayari kabisa. Akhsante kwa Deo Mutta mwanatanga


Friday, December 6, 2013

NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga dunia.
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Taarifa zinazohusiana
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kuwa mwanawe wa kiume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004


Wednesday, December 4, 2013

WANAUME WAAZIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUVAA NAVAZI YAO.

Ili kuonyesha uelewa na jinsi wanavyo
thamini mchango wa wanawake kwenye
maisha yao wanaume hawa wamekubali
kuvaa viatu vya kike aina ya High Hill
[Skuna] ilikuonyesha wako tayari kupitia
tabu na matatizo wanaopitia wanawake
duniani na wanakubali sana mchango wao
kwenye jamii. Wewe upo tayari kupiga
picha na viatu hivi sasa?



HII NDIO RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI YA YANGA

Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetoa ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka Julai 14, 2013 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu hayo kwa wapenzi, washabiki, na wanachama na jamii ya kwa ujumla.
[Lawrence Mwalusako akiongea na waandishi wa habari (picha na maktaba)]
Lawrence Mwalusako akiongea na waandishi wa habari (picha na maktaba)
Baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni pamoja na usajili wachezaji na mishahara.Akiongea na waandishi wa habari juu ya mahesabu hayo katibu mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako amesema mapato makubwa ya klabu yanatokana na viingilio vya mechi na ufadhili.
    Juhudi mbalilmbali zinafanyika kuongeza kipato cha klabu kama kuingia mikataba ya ufadhili, kutumia haki miliki za klabu.
    Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti matumizi ya klabu kama njia moja ya kuhakikisha klabu inajitegemea.
    Klabu bado inaendelea kutegemea ufadhili wa TBL ambao kwa sasa inapata wastani wa mIL 30.25 kila mwezi, Madhumuni ya ufadhili huu ni kuwezesha klabu kulipia mishahara ambayo wastani inzaidi mil 60 kwa mwezi. Tayari klabu imeshaomba mazungumzo na mfadhili kuboresha mkataba huo.
    Katika kipindi cha Januari 2013 hadi Julai 2013 klabu iliweza kupata mil 110 kama zwadi mbalii mbali za ushindi ikiwemo mil 15 kutoka vodacom kwa kuwa timu yenye nidhamu.
    Bado kuna mali za klabu hazija thaminiwa zikiwemo majengo.


Monday, December 2, 2013

HAYA NDIO MAKOSA 11 YA ZITTO ALIYOANDIKIWA NA SLAA


MASHITAKA 11 dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, yamebainisha kuwa kosa kubwa la kiongozi huyo kijana, ni nia yake ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.
Chanzo chetu cha habari kilichoona mashitaka hayo kabla ya kutumwa kwa washitakiwa, kimebainisha kuwa makosa saba kati ya makosa 11, yanahusu kugombea uenyekiti Taifa, au kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa.
“Ukiona hayo mashitaka yenyewe ndugu yangu, yanajirudia rudia na kuzunguka katika kosa moja la nia ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa… angalia kosa la kwanza, kosa la tatu, tano, sita nane na tisa, ni kama vile kuwania uenyekiti ndio kosa kubwa.
“Hata hivyo kwa jinsi mgawanyiko ulivyo ndani ya chama sasa, nakuhakikishia hawa jamaa (Zitto, Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba), watarudishwa katika nyadhifa zao na hakuna atakayeadhibiwa,” alisema mtoa taarifa wetu.
Alinukuu kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyehoji kama makosa wanayotuhumiwa akina Zitto ni makubwa kiasi cha kuyeyusha mema aliyoyafanya katika chama. “Si umesikia akina Baregu wakizungumza? Kwa mashitaka yale nakuhakikishia kitakachofanyika ni kufunika kombe mwanaharamu apite,” alisema mtoa habari wetu.
Kosa la kwanza kwa Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, wanadaiwa kuvunja Kanuni ya Chama inayokataza kukashifu chama, kiongozi au mwanachama yeyote. Katika maelezo ya kosa hilo, akina Zitto wanadaiwa kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.
Moja ya madai katika mashitaka hayo, ni kilichoandikwa katika Mkakati wa Mabadiliko 2013, kuwa Mbowe amekuwa akinunua vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambayo haihojiwi popote. Wanadaiwa pia wamemkashifu Dk Slaa kwa kudai ni mdhaifu kwa kumruhusu Mbowe kuingilia shughuli za kiutendaji.
Zitto na wenzake wanadaiwa katika kosa la pili, kutokuwa wawazi na wa kweli wakati wote na kushirikiana na vikundi vya majungu na udanganyifu kinyume na Kanuni za Uendeshaji kipengele cha 10.1 (VIII.
Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).
Katika kosa la nne, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama, miongoni mwa jamii, kisiasa au kijamii. Katika kosa hilo wanadaiwa kwenda kinyume na kipengele cha 10.1 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Akina Zitto katika kosa la tano, wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya kuchonganisha na kuzua migogoro kwa viongozi wa chama au wanachama, kinyume na kifungu cha 10.1 (IX), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Katika kosa la sita ambalo mtoa habari wetu alisema ndio kubwa, Zitto na wenzake wanadaiwa kutekeleza mpango wa kusudio la kugombea uenyekiti wa Chama Taifa, bila kutangaza kusudio la kutangaza nafasi hiyo.
Hatua hiyo inadaiwa kuwa ni kinyume na kifungu 2.C cha Muongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi ya Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali wa 2012.
Zitto na wenzake katika kosa la saba, wanadaiwa kutengeneza mitandao ya kuwania uongozi ndani ya chama kwa nia ya kujihakikishia ushindi kinyume na kanuni ya 2 (D), ya Muongozo wa Kuwania Uongozi.
Katika kosa la nane, Zitto na wenzake wanadaiwa kuwachafua viongozi na wanachama wengine wenye kusudio/nia ya kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti kinyume na kifungu 2 (E) cha Muongozo wa Kuwania Uongozi.
Katika kosa hilo, kumewekwa maelezo ya ziada kuwa kosa hilo linaunganishwa na kosa la kwanza ambalo washitakiwa wanadiwa kuwakashifu Mbowe, Dk Slaa na Lema.
Kosa la tisa, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na upinzani dhidi ya chama na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa chama, kinyume na kifungu cha 10.3 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji.
Kosa la kumi linamhusu Zitto peke yake, ambapo anaidaiwa kukashifu chama na kiongozi wa chama nje ya Bunge kinyume na kifungu 2 C (B), kikisomwa pamoja na kifungu 3 B cha Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Wabunge.
Katika hilo Zitto kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa chama yaani Dk Mkumbo na Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana, wanadaiwa kusambaza waraka uitwao Mkakati wa Mabadiliko 2013.
Mkakati huo, unadaiwa kukashifu chama na/ au viongozi wake wakuu kama ilivyoelezwa katika kosa la kwanza, tatu, nne na nane.
Mwisho katika kosa la 11, Zitto na wenzake wanadaiwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama kinyume na kanuni ya 3 F ya Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Bunge.
CHANZO: HabariLeo


AZAM TV KUANZA KURUSHA MATANGAZO DESEMBA 6: ANGALIA PICHA ZA UZINDUZI ULIVYO KUWA

IMG_6374
Mtangazaji wa Televisheni ya Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akiwa kwenye Red Carpet kabla ya mahojiano na Mkurugeni wa Kajunason Blog Cathbert Angelo.
IMG_6378
Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV. Pichani akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwambulambo.
IMG_6379
IMG_6405
Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akifanya mahojiano na Mdau William Malecela a.k.a LEMUTUZ na Mmiliki wa Blog ya Wananchi.
IMG_6505
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akizungumza kwenye uzinduzi wa Azam TV uliofanyika Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel mwishoni mwa Juma ambapo amesema Azam TV imekujali kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa Digitali na kutoa fursa ya ajira kwa Vijana wa Tanzania wenye vipaji sanjari na kuitangaza nchi yetu katika bara la Afrika hasa kwenye upande wa Soka na Filamu.
Azam TV itaanza kurusha matangazo yake Desemba 6 mwaka huu, Watanzania kaeni mkao wa kula kupata King’amuzi kwa bei rahisi ambacho kitakuwa na chaneli zisizopungua 50.
IMG_6513
Fashi fashi zikipamba uzinduzi rasmi wa Azam TV.
IMG_6518
Baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwa wameshikilia Ving’amuzi vya Azam TV wakati wa uzinduzi huo.
IMG_6537
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Azam TV mara baada ya kuzindua rasmi kwenye sherehe zilizofanyika mwishoni mwa Juma Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel.
IMG_6426
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) katika tete-a-tete na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington mara baada ya kuzindua Azam TV itakayoanza kurusha matangazo yake hewani Desemba 6 mwaka huu.
IMG_6456
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Tv, Rhys Torrington akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Azam Television jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
IMG_6478
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam Tv Efe Atiyio akifafanua juu ya program mbalimbali za Azam Tv .Na MO BLOG
IMG_6431
Yusuf Bakhresa akizungumza jambo na watoto wake kwenye uzinduzi huo.
IMG_6415
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Concepts Limited, Benny Kisaka (katikati) alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

IMG_6429
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.
IMG_6422
Yusuf Bakhresa akibadilishana mawazo na wadau wa michezo nchini waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_6494
Mkurugenzi Mtendaji wa Aggrey & Clifford Bw. Rashid Tenga naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
IMG_6460
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Boniface Wambura (kushoto) akifuatilia yanayojiri kwenye uzinduzi huo.
IMG_6419
IMG_6484
IMG_6391
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mh Mohammed Dewji (MB) akifurahi jambo na wadau.
IMG_6388
IMG_6414
IMG_6571
Mtangazaji maarufu wa Radio One na ITV Maulid Kitenge na Mfanyabiashara maarufu CEO wa Delina Group Enterprises Bw. Davis Mosha wakifurahi jambo wakati wa uzinduzi huo.
IMG_6492
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_6497
IMG_6398
IMG_6421
IMG_6463
IMG_6427
IMG_6589
Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya SSB Ltd. Said Muhammad Said (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za Bakhresa.
IMG_6586
Mdau Omar Said ( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kwenye picha ya pamoja.

CHANZO: TANZANIA NEWS


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU