Sunday, October 20, 2013
Saturday, October 19, 2013
Friday, October 18, 2013
Thursday, October 17, 2013
SHABIKI WA YANGA AMESEMA ATAJINYONGA KAMA SIMBA ITAIFUNGA YANGA
SHABIKI maarufu wa Yanga, Steven Mwamwala amedai kuwa, kama wakifungwa na Simba mechi ya Jumapili ijayo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, atajinyonga.
Na akamsisitizia mcheza filamu, Wema Sepetu afike uwanjani kuona mechi ya Simba na Yanga Jumapili ili ampe zawadi yake ya jezi ya Yanga aliyoigharamia Sh45,000.
Mwamwala ana historia na Yanga ilipopigwa mabao 5-0 aliangua kilio cha nguvu na video zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli ya shabiki huyo inakuwa mzigo kwa wachezaji wa Yanga kama, Athuman Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani, Mrundi Didier Kavumbagu na Wanyarwanda Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ kuhakikisha wanafanya vizuri na kuokoa maisha ya kijana huyo mwenye miaka 31.
Aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Nimeandaa kamba ya katani kabisa, nimeificha na siwezi kusema nilipoiweka kama Yanga itafungwa mchezo huo, nitajinyonga ili kupoteza uhai wangu. Unajua inauma sana mnapofungwa, nataka timu yangu ishinde Jumapili ili niwe na amani kwa ushindi wowote ule ilimradi tutoke na pointi tatu.”
Kuhusu, Wema shabiki huyo alisema anampenda sana kama dada yake na anatamani akutane naye.
“Nimemtafuta sana na naomba siku hiyo aje kwa sababu nimemwandalia zawadi. “Nimemnunulia jezi ya Yanga na tayari nimeiandika jina la Wema, imenigharimu Sh 45,000,” alifafanua Mwamwala ambaye anaishi Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.
CHANZO: MWANASPOTI
Wednesday, October 16, 2013
WANACHAMA WA YANGA KUPIGA KURA ILI KUIBADILI CLUB KUWA KAMPUNI
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetangaza rasmi kuanza kwa zoezi la kupiga kura ya NDIYO juu ya uundwaji wa kampuni au kura ya HAPANA kwa kutoridhia klabu kuwa kampuni maazimio yaliyofikiwa katika mkutano mkuu uliofanyika Januari 16, 2013.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga kaimu katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema zoezi hilo linanza leo kwa wanachama hai kufika makao makuu ya klabu na kupiga kura ya NDIYO au HAPANA na zoezi hilo litaendelea mpaka novemba 10, 2013.
Ifuatayo ni Taarifa kwa Wanachama na Waandishi wa Habari
MAONI YA WANACHAMA YA KUUNDA KAMPUNI
Katika Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 16 Januari 2013 Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama wafikirie mapendekezo ya YANGA kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa YANGA.
Nachukua nafasi hii kuwaambia Wanachama wa YANGA kuwa kuanzia leo tarehe 16 Oktoba 2013 mpaka tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja (1) hapa Klabuni kwa ajili ya kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni (HAPANA)
Kila Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.
Zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya YANGA.
“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
LAWRENCE MWALUSAKO
HIVI NDIO VIINGILIO VYA MECHI YA YANGA NA SIMBA
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumapili(Otoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam, ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na Ferdinand Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe

Tuesday, October 15, 2013
HATIMAE DR NDALICHAKO AONDOKA NECTA
MCHUNGAJI WA KANISA LA ANGLIKANA GONGO LA MBOTO AFUMANIWA GUEST NA MKE WA MTU

TOFAUTI na inavyoaminika na wengi
kuwa watumishi wa Mungu ni watu safi, safari hii Mchungaji Obed Ntimba
wa Kanisa la Anglikana Gongo la Mboto, Dar es Salaam amejikuta akivunja
agano la Muumba baada ya kunaswa gesti akiwa na mke wa mtu.
Tukio hilo la aibu lilimkuta mchungaji huyo Ijumaa iliyopita saa saba na nusu za mchana katika gesti moja (jina lipo) iliyopo nyuma ya Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar.
Siku moja kabla ya tukio, makachero wetu walitonywa kuhusu dhambi hiyo na mtu wa karibu na watu hao akisema kuwa anaumia kwa sababu mchungaji huyo ana mke na watoto na mwanamke huyo, Rose ni mke wa mwanajeshi kwa hiyo aliamini tendo wanalotaka kulifanya ni uovu katika jamii.
Mtoa habari wetu huyo alisema tukio hilo lilipangwa kukamilika kesho yake Ijumaa katika gesti hiyo ndipo kazi ya kuwafuatilia hatua moja baada ya nyingine ilianza.
Ijumaa saa sita mchana, mtonyaji wetu alipiga simu na kuweka wazi kwamba wawili hao wapo njiani kuelekea gesti, kila mmoja kwa usafiri wake.
Ndipo makachero wetu walipowatonya polisi na kuambatana nao mpaka kwenye gesti hiyo na kujipanga kwa mbinu za kisasa za kutoonwa na ‘adui’.
Makachero hao walifanikiwa kupata ramani ya chumba walichoingia wawili hao ambapo ‘rumu’ namba 1B ndiyo iliwasilishwa kwamba Rose na mchungaji wake wamo humo.
Saa saba na nusu mchana, Makachero wetu na polisi waliingia hadi mapokezi ya gesti hiyo kwa kificho na kutoa maelekezo kwa mhudumu. Mhudumu aliongozana nao hadi mlangoni na kugonga lakini haukufunguliwa.
BAADA YA DAKIKA TANO
Wakati mlango huo ukigongwa na mhudumu bila kufunguliwa, mchungaji huyo alisikika akisema na kuuliza:
“Subirini kwanza.”
“Lakini ninyi ni akina nani?”
Baada ya dakika tano kupita, mlango ulifunguliwa, mchungaji akakutana na macho ya timu nzima. Alipigwa butwaa asijue la kufanya huku akitetemeka, Rose alikuwa ndani ya khanga moja!
MCHUNGAJI MSOBEMSOBE HADI POLISI
Polisi waliwabeba msobemsobe wote hadi Kituo cha Polisi cha Urafiki-Ubungo, Dar ambapo kila mmoja alianza kujieleza.
MCHUNGAJI APANGULIA HUDUMA YA KIROHO
Kituoni hapo, Mchungaji Ntimba alipobanwa kuhusu sababu za kuingia gesti na mke wa mtu, alisema waliingia kwa ajili ya huduma ya kiroho kwani mwanamke huyo alikuwa anataka kufungua kanisa ndipo alipomuomba yeye amsaidie.
“Mimi sikuwa na lengo baya jamani. Huyu dada alihitaji kufungua kanisa, akaniambia ili nimshauri hawezi kukaa sehemu ya wazi kwa kuwa mume wake ni mwanajeshi anaweza kuonekana na watu wakampa taarifa.
“Ndipo nikaamua kwenda naye katika nyumba ile ya kulala wageni kwani wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya huduma, wakitokea nchi mbalimbali huwa wanalala pale na wahusika wa pale wananifahamu sana.
“Baada ya kuingia gesti nilibanwa na haja ndogo, nikaenda kujisaidia. Cha kushangaza niliporudi nilimkuta huyu dada amevua nguo zote na kuanza kunishawishi lakini sikuwa na lengo hilo jamani,” alijitetea mchungaji huyo.
Baadhi ya picha zilizopo zinamuonesha mchungaji huyo akiwa amevaa suruali lakini amesahau kufunga zipu huku kondom zikiwa pembeni kitandani!
MSIKIE MKE WA MTU SASA
Baada ya mchungaji kutoa maelezo yake, mke wa mtu naye alianza kutiririka ya kwake huku akionesha ushahidi wa meseji za simu ambazo mchungaji huyo alikuwa akimtumia akimshawishi kumpa penzi.
“Huyu mchungaji nilikwenda kwake kwa lengo la kufanya kazi kanisani lakini kuanzia hapo amekuwa akinishawishi kuwa anataka nimpe penzi ili aweze kuniweka katika sehemu nzuri kanisani.
“Nilikuwa nakataa, lakini akasema tukutane pale gesti tuongee zaidi. Nilikataa kukutana gesti, akaniambia pale ni ofisini, mara nyingi akiwa anaongea na waumini mambo muhimu ya huduma ya kiroho huwa anakutana nao pale.
“Nikakubali lakini kabla hata hatujaongea chochote alianza kuvua nguo zake na kuanza kunilazimisha tufanye mapenzi huku akiwa na ‘kinga’ kabisa na mimi nikavua nguo lakini kabla hajatimiza lengo lake ndipo wakaingia watu wakiwa na askari.
“Mimi nashukuru sana kwa sababu hawa ndiyo wameniokoa. Nilikuwa nikisikia habari za huyu mchungaji kuwa ana tabia ya kuwafanyia wasichana wengi vitendo hivyo na kweli leo ndiyo nimeamini,” alieleza mwanamke huyo.
Katibu wa kanisa hilo (jina halikupatikana mara moja) alimuombea msamaha mchungaji kwa waandishi huku akionesha kuumizwa na kitendo hicho baada ya kuoneshwa ushahidi na kukiri kwamba una ukweli tofauti na alivyokuwa akifikiria awali kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
-Source: Global Publisher.

Subscribe to:
Posts (Atom)