Facebook Comments Box

Tuesday, October 1, 2013

SABABU YA CHUJI KUWEKWA BENCHI NA BRANDIS YAWEKWA HADHARANI





Athumani Idd Chuji - Kiungo mpigaji wa pasi ndefu Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts amewataka wachezaji wake wacheze pasi fupi zenye akili kwa sababu ndiyo ushindi wao na si ndefu kama wanapopoa maembe mtini na akaweka wazi kuwa, alimtumia kiungo wake mkongwe, Athuman Idd ‘Chuji’ kama mchezaji wa akiba kwa sababu hajafanya mazoezi na timu kwa muda mrefu.
Chuji aliingia kipindi cha pili katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo na dakika chache baadaye Yanga ikapata bao la ushindi lililofungwa na Hamis Kiiza raia wa Uganda matokeo yakawa ya ushindi wa bao 1-0 mwishoni mwa wiki.
Kutokana na kitendo hicho mashabiki wa soka walihoji na kupiga kelele kulikoni kiungo huyo aachwe nje wakati ni msaada kwenye timu.
Brandts alisema: “Nataka timu icheze mpira kwa pasi fupi fupi na kwa umakini na si ndefu zisizo na mpango kwa sababu ndiyo zinatugharimu na hata mechi yetu na Ruvu kipindi cha kwanza hatukuwa vizuri.” 

Akimzungumzia Chuji, kocha huyo alisema: “Sikuweza kumtumia kipindi cha kwanza kwa sababu hakuwa na muda mzuri wa pamoja na wenzake katika mazoezi na alikuwa kwao, kulikuwa na matatizo ya kifamilia.
Hali hiyo ndiyo ilinifanya nisimpange kikosi cha kwanza na ndiyo maana nilimtumia kipindi cha pili.”
Chanzo:Mwanaspoti


HEBU MTAZAME MOYES KATIKA KIBONZO HIKI ANAFURAHISHA KWELIKWELI




EVERTON YAICHAPA NEWCASTLE UNITED MAWILI KWA BILA


Mshambuliaji Romelu Lukaku amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa Everton dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja wa Goodison Park.
 
Lukaku alifunga mabao hayo katika dakika za tano na 37,wakati lingine lilifungwa na Barkley dakika ya 25 na mabao ya Newcastle United yalifungwa na Cabaye dakika ya 51 na Remy dakika ya 89.
 
Mshambuliaji huyo anamuonyesha kocha wa Chelsea, Mreno Jose Mourinho kwamba alikosea kumruhusu kuondoka majira ya joto. 
 
Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard, Baines, Distin, Jagielka, Coleman, Mirallas/Deulofeu dk73, McCarthy, Barry, Osman/Stones dk90, Barkley/Naismith dk88 na Lukaku.
 
Newcastle United: Krul, Debuchy, Yanga-Mbiwa/Williamson dk45, Coloccini, Santon, Anita/Cisse dk69, Tiote, Sissoko, Gouffran, Remy na Ben Arfa/Cabaye dk45.
Main man: Romelu Lukaku scored two of Everton's goals to put Newcastle to the sword at Goodison Park
Romelu Lukaku ameifungia mabao mawili Everton ikiilaza Newcastle 3-2 Uwanja wa Goodison ParkOpening salvo: Lukaku needed just five minutes to score Everton's first as they eased to victory
Dakika tano zilitosha kwa Lukaku kufunga bao la kwanzaBright spark: Ross Barkley continued to showcase his potential with a calmly taken second goal for Everton
Barkley akishangilia baada ya kufunga
Open goal: A defensive mistake from Newcastle allowed Lukaku to slam the ball home from close range
Lukaku akifunga bao la kwanzaOpen goal: A defensive mistake from Newcastle allowed Lukaku to slam the ball home from close range
Lukaku akifunga bao lake la pili


CHEZEA MVUA ZA DAR WEWE? MREMBO APANDA MKOKOTENI MWENYEWE!!!


Kama anavyoonekana hapo juu katika picha mbili, mrembo huyu akionekana japo akiwa na woga lakini alikuwa hana jinsi baada ya mvua kunyesha Dar na hali kuwa kama inavyoonekana hapo, hali ilibadilika ghafla na maji kujaa barabarani na foleni za hapa na pale ndani ya Jiji hili hapo Jana Tarehe 30/09/2013.


MKENYA ALIYE DAIWA KUMTEKA DR ULIMBOKA ATOZWA FAINI TSH 1, 000


Mtuhumiwa wa kutoa ushahidi wa uongo wa kumteka aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha madaktari, Dk Steven Ulimboka, Joshua Muhindi akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,mara baada ya kulipiwa faini ya Sh 1,000.
Dar es Salaam. 

Mkenya Joshua Muhindi aliachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh1,000 kwa kupatikana na hatia ya kuidanganya polisi kuwa alihusika kumteka na kumjeruhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini hiyo. Mulundi alilipiwa faini hiyo na Mwandishi wa Habari wa Redio Times, Chipangula Nandule.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka kusoma maelezo ya awali na mshtakiwa huyo kukiri alitoa taarifa ya uongo kwa polisi kuhusu tukio hilo.
Kabla ya hukumu hiyo, Mulundi aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hilo lilikuwa kosa lake la kwanza. Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na kupelekwa Dar es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi kufika.
Alisema kutokana na kutekwa huko alichanginyikiwa hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa aliyemteka alikuwa na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.
“Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho hivyo, nilikwenda Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye eneo la Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na kuungama kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande,” alisema Mulundi na kuongeza.
“Siwalaumu Serikali, upande wa mashtaka wala polisi kwa kitendo cha kuniweka gerezani kwa muda mrefu, najilaumu mimi mwenyewe.” Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Kweka aliiambia Mahakama kuwa hana kumbukumbu za uhalifu za mshtakiwa lakini aliomba apewe adhabu kali kutokana na mazingira ya tukio hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Katema alisema alifikia uamuzi huo kwa kuzingatia maombi ya mshtakiwa ya kupunguziwa adhabu.
CHANZO: MWANANCHI


Monday, September 30, 2013

NGASSA AOMBA WAPENZI NA WANACHAMA WA YANGA KUMCHANGIA ILI AWEZE KURUDISHA PESA ALIZO ILIPA SIMBA


Mshambuliaji nyota Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ameonekana akifanya mazoezi mara mbili, baada ya kumaliza awamu ya pamoja na wenzake Yanga SC chini ya kocha wake, Mholanzi Ernie Brandts akaenda katika ufukwe wa Coco kufanya mazoezi binafasi. 

Ngassa ambae ameanza kucheza juzi katika mechi kati ya Yanga na timu ya Ruvu Shooting ya RUVU, Mkoani Pwani baada ya kutumikia kifungo cha michezo 6 pamoja na kuilipa timu ya Simba pesa zake shilingi milioni 45 baada ya kuamuriwa kufanya hivyo na TFF ikiwa ni adhabu baada ya kuingia mkataba na Simba huku akijua kuwa bado ana mkataba na timu ya Azam.

Mchanganuo wa pesa hizo ni kwamba shilingi 30 milioni ni fungu alilolipwa na Simba na shilingi milioni 15 ni fidia. Mchezaji huyo alilazimika kulipa pesa hizo kutoka katika akaunti yake mwenyewe ambazo alilipa siku ya Ijumaa na siku ya Jumamosi alicheza mchezo kati ya Ruvu na Yanga ambapo timu yake ilipata ushindi wa bao 1-0 huku yeye akitoa pasi ya goli hilo kwa mfungaji Hamis Kiiza 'Diego'.


Katika hali ya kushangaza Ngassa ameomba wanachama na wapenzi wa Yanga walioguswa na kitendo cha kulazimika kujilipia mwenyewe fedha za Simba SC, Sh. Milioni 45 kumchangia katika akaunti namba 01J2095037800 katika benki ya CRDB kwa jina la Mrisho Halfan Ngasa. “Naomba wanachama na wapenzi wa Yanga SC walioguswa kunichangia fedha katika akaunti hiyo ili tuwe tumesaidiana kulipa deni hilo,” alisema.
Ngassa akijifua peke yake Coco Beach




Ngassa alipoulizwa kuhusu kufanya mazoezi ya ziada, alisema ni kwa sababu pia anakabiliwa na kazi ya ziada kuisaidia timu yake katika Ligi Kuu, hivi sasa ikiwa inazidiwa na wapinzani wa jadi, Simba SC kwa pointi tano kileleni.  

Ngassa anadai Simba SC ilimwambia kuwa anasaini kucheza kwa mkopo kumalizia Mkataba wake wa Azam, lakini kumbe ni Mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo baada ya ule wa mkopo kumalizika.

“Nawashauri wachezaji wenzangu kwamba, wanapoingia mikataba na klabu, wahakikishe wanakuwa na mawakili, ili wawasaidie kujua kilichomo ndani yake na wasaini mikataba ambayo wanaielewa,”
Chanzo:http://tinyurl.com/k6td4pn


TAARIFA MPYA KUHUSU UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA YANGA


[Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Francis Kifukwe (katikati) ambaye pia ni mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa uwanja eneo la jangwani akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, kushoto ni mzee Jabir Katundu (mwenyekiti wa baraza la wazee) na kulia Lawrence Mwalusako katibu mkuu wa Yanga SC ]

LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana mara ya mwisho tuliongea na kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabidhi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. 

Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari. 

Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:-
• Kupata na kuwa na eneo la kutosheleza malengo ya mradi
• Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na mkandarasi mzuri wa mradi
• Kupata na kutenga fedha za kukamilisha usanifu na ujenzi wa mradi
Kwa upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.
Kutokana na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-
1. Uwanja wa mpira wenye viti 40,000
2. Hostel ya wachezaji na football academy ya vijana
3. Viwanja vya mazoezi
4. Uwanja wa kutosha kuegesha magari
5. Hoteli na sehemu ya makazi
6. Ukumbi wa mikutano
7. Sehemu ya maofisi, benki, zahanati (sports clinic)
8. Maduka, supermarket na sinema
9. Sehemu za kubarizi, kupumzikia (Recretional and Open spaces)

Mara baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City” na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na kitalii.
Ili kukamilisha azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.
Mwezi wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Klabu ya Yanga ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na haba hujaza kibaba.
Ndugu Wandishi wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu kuhusu michoro ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi na BCEG limesimama, likisubiri majibu ya nyongeza la eneo.  Ni matumaini yetu zoezi hili litakamilika hivi karibuni na kuendelea na mradi.
YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
Dar es Salaam, 30 September 2013
Francis Mponjoli Kifukwe


Saturday, September 28, 2013

TAARIFA: GAZETI LA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA NA SERIKALI

Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne (14) kuanzia 27 Septemba, 2013. Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 333 la tarehe 27 Septemba, 2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti, 2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya Kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli. Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. 

Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi, kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini (90) kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari. Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi, 2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”, tarehe 12 Juni, 2013, toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano, tarehe 18 Septemba, 2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.

Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishutumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii. Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332 (Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.

Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini, kuzingatia weledi, miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma, kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.

Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA, 2013


PICHA YA LEO: WAFUASI NA WANA CHAMA WA CCM WAKIPEWA LIFTI NA CHADEMA

Wafuasi na wanachama wa CCM wakipewa lifti na gari la Chadema lenye nembo ya M4C



Friday, September 27, 2013

USHAHIDI WA NGASSA KULIPA MILIONI 45 ZA SIMBA LEO HUU HAPA

Mrisho Ghalfan Ngassa akionesha risiti ya malipo aliyopewa na TFF baada ya kulipa milioni 45 anazo alizo takiwa kuilipa timu ya simba
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Young Africans Mrisho Khlafani Ngassa leo amelipa jumla ya mil 45, deni la mil 30 pamoja na faini ya mil 15 za klabu ya Simba SC kwa Shirikisho la Soka nchini TFF ili aweze kuitumikia timu yake kuanzia kesho.
Hundi ya milioni 45 ya Ngassa kwenda TFF kwa ajili ya kuwalipa simba

Ngassa ambaye aliambatana na viongozi wa klabu ya Yanga mjumbe wa sekretariat Partick Naggi, Afisa Habari Baraka Kizuguto na mhasibu Rose Msamila alikabidhi hundi za malipo kwa idara ya fedha ya shirikisho hilo.
Mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Ngassa aliongea na waandishi wa habari nje ya ofisi za TFF na kusema ameamua kulilipa deni hilo ili aweze kuitumikia klabu yake, kwani kukosa michezo sita kumemnyima fursa ya kuisaidia timu yake.
hapa Ngassa akionesha hundi hizo
Naomba mnielewe hizi fedha nimezitoa mimi mwenyewe kwenye akiba yangu iliyopo bank, hivyo kama kuna mtu yoyote ataguswa na hili suala anaweza kuwasiliana na mimi katika kujaribu kunichangia juu ya hili.
Hizi hapa
Aidha Ngasaa amesema kwa sasa akili yake yote ipo kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom na lengo lake ni kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya vizuri n akupata ushindi katika kila mchezo watakaocheza.
Kocha Ernie Brandts kwa sasa ana fursa ya kumtumia mchezaji Mrisho Ngasa kwa kuanzia kwa mchezo wa kesho kutokana na kuwa amekamilisha kila kitu.
Naye Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amewaomba wapenzi, washabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kuja kuishangilia timu yao itakapokua ikicheza na maafande wa Ruvu Shooting.
Muhasibu wa TFF akikunja goti kuandika risiti
Young Africans itacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

CHANZO: BIN ZUBEIRY




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU