Facebook Comments Box

Sunday, September 8, 2013

MWILI WA ALIE UAWA NA MUMEWE KWA KUTOBOLEWA KOO WASAFIRISHWA KWA MAZIKO DODOMA

Picture


TAIFA STARS YAPIGWA MBILI NA GAMBIA NA KUHITIMISHA SAFARI YAKE YA BRAZILI

Timu ya taifa ya Gambia inayoshika mkiani mwa kundi la C kwenye michuano ya kugombea nafasi ya kushiriki michuano ijayo ya kombe la dunia imemaliza mbio hizo kwa ushindi wa kulinda heshima dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania kwa kushinda 2-0 katika uliomalizika hivi punde huko Gambia.
 
Kiungo Mustapha Jarjue alifunga mabao yote mawili katika mchezo huo - kila kipindi akifunga bao moja.

Jarjue aliiweka mbele Gambia kwa bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza dakika za mwisho kabla ya kuongeza la pili dakika 6 baada ya mapumziko.

Pamoja na ushindi lakini Gambia imeshindwa kuiondoa Tanzania katika nafasi ya 3 ya kundi hilo baada ya kumaliza nafasi ya nne - wakiwa na pointi sita kutoka michezo sita iliyopita ya kundi hilo.
Cote d'Ivoire wamemaliza wakiwa juu ya kudni hilo wakiongoza kwa pointi 13 huku wakielekea kwenye mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba dhidi ya Morocco.


TUNAOMBA UTUPIGIE KURA ILI TUSHINDE; PIGA KURA MARA NYINGI UWEZAVYO


TUNAPENDA KUTANGULIZA SHUKRANI ZETU KWA WALE WOTE MLIOTUCHAGUA KUINGIA KWENYE MASHINDANO HAYA YA BLOGS AWARDS,TUNAOMBA KURA YAKO ILI TUWEZE KUIBUKA WASHINDI SASA,CLICK LINK HAPO CHINI NA UTUPIGIE KURA MARA NYINGI UWEZAVYO,

TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU,

JINA LA BLOG YETU NI kitongoni.blogspot.com

click hiyo link hapo chini upige kura mara nyingi uwezavyoooo

Vote For The Best Sports News Blog 

 

GONGA HAPA KUTUPIGIA KURA 



KIBONZO: MBUNGE ANATAFUTWA

Picture


Saturday, September 7, 2013

HUYU NDIO BINTI ALIEZAA NA DIAMOND

MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
MCHEZO MZIMA
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano.
Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo.
Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo.
Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.
WAKUTANA
Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.
Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa.
WEMA ATAJWA
Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo.
Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu.
Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.
Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.
‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.
Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia.
Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana.
Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya  na walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa.
Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao.
Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina.
SASHA AKIRI
Baada ya kupata madai hayo,tulimsaka Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena,  naye aliacha kumfuatilia.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.
HUYU HAPA DIAMOND
Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya kiganjani akiwa Nairobi, Kenya na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya ishu hiyo, alieleza:
“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Katika kuonesha ‘usiriazi’, tuliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha



Friday, September 6, 2013

KESI YA BILIONEA WA MADINI YAAHIRISHWA IKIWAACHA NDUGU WAKIPOTEZA FAHAMU MAHAKAMANI


 Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
 Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya  kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.

Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo 
Picha na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.


DAKTARI FEKI AKAMATWA KCMC

Hali ya wasiwasi imejitokeza kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa huduma za  matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi Kilimanjaro baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumkamata mtu anayejifanya kuwa ni daktari wa watoto akiwa kwenye wodi ya upasuaji. Daktari huyo feki aitwae Alex Sumni Massawe amewekwa chini ya ulinzi na Jeshi la Polisi baada ya kukutana na mmoja wa wagonjwa ambae alimuahidi kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa ngozi.
Alex anadaiwa kutaka kumfanyia upasuaji kijana MAKASI TIPESA mkazi wa Manispaa ya Moshi ambae amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa muda mrefu sasa. Afisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC Gabriel Chisseo amesema daktari  aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambae amekuwa akijinadi kwamba anafanya huduma hiyo hospitalini hapo.

Chisseo anasema ‘Katika jitihada za wazazi kumuokoa mtoto wao wakawa wamewasiliana na mtu mmoja mtaani aliwapa namba ya huyu daktari feki kwamba angewasaidia, walipokutana nae alisema wamlipe shilingi laki tatu ili afanye huo upasuaji hospitalini KCMC ambapo alitanguliziwa laki mbili za kuanzia’ Uongozi wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo aliyekamatwa ndani ya Hospitali hiyo si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake cha kazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha jeshi hilo kumtia mbaroni Alex.

Daktari feki akiwa chini ya ulinzi


Thursday, September 5, 2013

VIDEO: VURUGU ZA BUNGENI LEO




PICHA: ANGALIA PICHA ZA VURUGU BUNGENI LEO HII





Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.

****
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.

Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.

Mara baada ya  zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.


PICHA: RAIS KIKWETE ALIPO KUTANA NA RAIS KAGAME







WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUSOTA NA FOLENI ZA BARABARANI


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wataendelea kukumbwa na kero ya msongamano wa magari barabarani baada ya mpango wa serikali wa kupunguza tatizo hilo kupitia ujenzi wa barabara zilizopo nje ya jiji kukwama kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo wakandarasi wanaojitokeza kuomba kujenga kuomba  kiasi kikubwa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale, alisema mpango huo wa kujenga barabara za nje ya jiji upo ingawa unakabiliwa na changamaoto mbalimbali zikiwamo watu kutojitokeza kuomba kazi ya kujenga na wanaojitokeza kuomba kiasi kikubwa cha fedha hatua iliyoifanya serikali kurudia kutangaza tenda.

Katika mkutano wa Bunge la bajeti mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alitangaza kwamba kwa  mwaka 2013/2014 serikali itajenga barabara za nje ya jiji la Dar es Salaam ili kukabiliana na msongamano wa magari.

Alizitaja kuwa ni pamoja na inayoanzia Mbezi Beach Tangi Bovu hadi Mbezi Shamba kupitia Goba, Mbezi Shamba hadi Tegeta kupitia Goba na ile ya Mbezi Shamba hadi Uwanja wa Ndege kupitia Kinyerezi.

Ahadi nyingine aliyotoa Dk. Magufuli kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 ni ujenzi wa barabara za juu katika maeneo ya Tazara, Mwenge na Ubungo mipango ambayo mpaka sasa haijaanza kutekelezwa.

Wakati ahadi hizo zikichelewa kuanza, Tanroads  imesema barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha Lami na nyingine Changarawe kulingana na upatikanaji wa fedha.

Kuhusu bomoa bomoa mbalimbali zinazoendelea jijini Dar es Salaam, Mfugale alisema baadhi hawahusiki nazo na kutoa mfano nyumba zilizomolewa wiki iliyopita eneo la Mbezi Beach.

Alisema wananchi wakiona Tingatinga linabomoa mahali popote wanajua ni Tanroads na kusema kuwa baadhi ya maeneo yanabomolewa kwa ajili ya kupitisha bomba la maji au shughuli zingine za serikali siyo lazima iwe ujenzi wa barabara.

SOURCE: NIPASHE


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU