Facebook Comments Box

Wednesday, July 17, 2013

PICHA: MAJENGO YA SCHOOL OF LAW YAKABIDHIWA KWA SERIKALI

Picture
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akitia saini hati ya makabidhiano ya majengo ya Law School of Tanzania wakati wa shughuli ya makabidhiano ya majengo hayo iliyofanyika jana Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam. Wanaoshuhudia ni Bw. Emmanuel Mayeji kutoka Wizara ya Katiba na Sheria (wa kwanza kulia), Mh. Jaji Gerald Ndika Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (wa pili kulia), na wa kwanza kushoto ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji kutoka Co-architecture.
Picture
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi amepokea hati ya makabidhiano pamoja na funguo za majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kutoka kwa Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group, Bw. Zhang Chengwei iliyokuwa ikijenga majengo hayo na kukamikika.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana, siku ya Jumanne, Julai 16, 2013 jijini Dar es Salaam.

Anayeshuhudia katikati ni Bw. Aloyse P. Mushi, Mkurugenzi Mtendaji wa Co-Architecture.

Picha, maelezo: Farida Khalfan


RAIS KIKWETE AONGEA KWA SIMU NA RAIS AL-BASHIR NA KUMUAGIZA AWATAFUTE WALIO WAUWA WANAJESHI WA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan Mheshimiwa Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur na kumtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

Katika mazungumzo yao, Rais Omar Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka  hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Rais Bashir amemueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini kuwa waliohusika ni wahalifu na hivyo kuahidi kuwa lazima 
watasakwa hadi kukamatwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Rais Bashir amempa pole Rais Kikwete kwa tukio hilo la kusikitisha ambapo wanajeshi wa Tanzania wameenda nchini Sudan kulinda Amani na Usalama wa wananchi wa Sudan.

Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Bw. Ban Ki Moon alimpigia Rais Kikwete na kumpa pole kwa mkasa huo mkubwa na wa kusikitisha ambao umewatokea wa Tanzania hao wakati wakiwa katika kutekeleza jukumu lao la kulinda amani nchini Sudan.

Hadi sasa hakuna kikundi chochote ambacho kimekiri kuhusika na shambulio hilo ingawaje kumekua na  kutupiana lawama baina ya vikundi vya kiserikali na  vya waasi katika jimbo la Darfur.

Mapigano baina ya vikundi vya kikabila na koo mbalimbali zimesababisha mapigano na uvunjifu mkubwa wa amani na usalama katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 10 sasa, na mara nyingi mapigano  na tofauti zao hizo zimesababisha vifo na uvunjifu wa amani kwa wananchi wa Sudan na wageni pia.

Mwishoni mwa mwaka jana  Wanajeshi wanne kutoka Nigeria waliuawa karibu na El Geneina , Magharibi mwa Darfur ambapo pia inaelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa wanajeshi wapatao 50 wameuawa tangu kikosi hiki cha Umoja wa Afrika kinachoundwa kwa  pamoja chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMID) kianze operesheni yake mwishoni mwa mwaka 2007.

Taarifa za Umoja wa Mataifa pia zinaeleza kuwa kabla ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha Tanzania jumamosi iliyopita, wanajeshi 6 wanaolinda Amani wameuawa tangu oktoba mwaka huu ambapo pia inasadikiwa kuwa watu wapatao 300,000 wameyakimbia makazi yao.

Hata hivyo kiini cha mgogoro huo unaosadikiwa kuwa ni ugomvi wa ardhi na rasilimali zilizoko katika jimbo hilo nchini Sudan.

Miili ya maaskari hao saba wa Tanzania inatarajiwa kuwasili nchini ijumaa tarehe 19, Julai kwa ajili ya maziko.

Imetolewa na:

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam, Tanzania

16 Julai, 2013


KIBONZO: HII TENA YA KIPANYA KUHUSU UCHAGUZI 2015

Picture


KIBONZO: HII NI KWA WAFUNGAJI WOTE




KIBONZO: KATUNI HII YA KIPANYA NAIPA HADHI YA JUU




Tuesday, July 16, 2013

MAWAIDHA: ADHABU 15 ZA MWENYE KUACHA SALA - SHEIKH HASHIM MBONDE




HANS POPE AISIFIA YANGA KWA KUSAJILI MSHAMBULIAJI TOKA NIGERIA

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wapinzani wao, Yanga SC sasa wanaanza kukua na kuachana na mambo ya kitoto, baada ya kuleta mshambuliaji kutoka Nigeria, Ogbu Brendan Chukwudi. 

Poppe amesema kwamba kwa muda mrefu Yanga wamekuwa kama watu ambao hawajui soka kwa kusikilizia Simba SC inataka kumsajili nani na wao ndiyo wamfuate.
Watani wanaanza kukua sasa; Zacharia Hans Poppe amewapongeza Yanga kwa hatua ya kutafuta wachezaji wao na si kusikilizia Simba SC wanataka kumsajili nani na wa wamfuate “Kwenye kikosi cha sasa cha Yanga kuna wachezaji wangapi wa Simba, wengi tu, yule Barthez (Ally Mustafa), Yondan (Kevin), Chuji (Athumani Iddi) na bado walitaka kuwasajili Amri Kiemba na Shomary Kapombe,”.

 “Usisahau Mbuyu Twite ni mchezaji ambaye tulikwishamsajili sisi, wao wakacheza faulo na kumchukua juu kwa juu. Sasa namna hii hatuwezi kukuza soka na ushindani hata wa utani wetu wa jadi,”.

 “Lazima Yanga iwe na wachezaji wake na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wake, na sisi tuwe na wachezaji wetu na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wetu,”. “Ona kama sasa, sisi tumesajili mfungaji bora wa Kombe la Kagame, wao wameleta mfungaji bora wa Nigeria, sasa hawa watu wawili washindane kuzipatia matokeo mazuri timu hizi,”.
Kifaa cha Jangwani; Ogbu Brendan Chukwudi akielekea Jangwani baada ya kuwasili jana usiku Dar es Salaam

Endelea kuisoma hapa

HATIMAYE MAHAKAMA YAMPA DHAMANA LUDOVICK JOSEPH

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Ludovick Joseph anayeshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miezi minne.

Ludovick aliachiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa Juni 10 mwaka huu.

Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 18 mwaka huu, wanakabiliwa na shitaka la kutaka kumdhuru Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky kwa kutumia sumu.

---HabariLeo 



VIDEO: JINSI YA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO - MASHAURI




Monday, July 15, 2013

MAWAIDHA: UMUHIMU WA TAWBA - SHEIKH NURDIN KISHK




THIAGO ALCANTARA AITOSA MAN UNITED NA KUJIUNGA NA BAYERN MUNICH



Hatimaye kiungo wa kimataifa wa Spain na FC Barcelona Thiago Alcantara ameuzwa rasmi kwenda kujiunga na mabingwa wa ulaya na Ujerumani Bayern Munich.

Thiago ambaye alikuwa akihusishwa mno na kujiunga na Manchester United ingawa juzi kocha David Moyes alisema hawakuwahi kusema wanamhitaji mchezaji, amejiunga rasmi ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa 25 million euros.

Mapema wiki iliyopita kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alikaririwa akisema kwamba anamhitaji Thiago kwenye timu yake na amewaomba viongozi wake kumsajili mchezaji huyo tu msimu huu.

Thiago amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Bayern Munich.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU