Facebook Comments Box

Wednesday, May 22, 2013

MACHAFUKO YA MTWARA OFISI YA CCM YACHOMWA MOTO


clip_image001

MAPAMBANO kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara umefika katika hatua mbaya,kiasi cha mtu mmoja kudaiwa  kujeruhiwa vibaya baada ya kurushiwa bomu wakati wa mashambulizi hayo katika eneo la Magomeni.
Mbali na kujeruhiwa kwa mtu huyo aliyekuwa katika maandamano ya kupinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia imechomwa moto.
Taarifa zilizonaswa na Fahari ya Kusini hivi punde zinadai kwamba wananchi wa Mkoa wa Mtwara wamefungiwa majumbani tangu asubuhi, huku Jeshi la Polisi likifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwanasa watuhumiwa wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo kwa njia ya vipeperushi.
Shuhuda wa wa tukio hilo ameitaarifu Fahari ya kusini  kwamba waandamanaji hao wameapa kufa endepo serikali itaendelea na mipango yake ya kusafirisha gesi hiyo hadi Jijini Dar es Salaam. "Hali hapa ni mbaya, tangu asubuhi wananchi wote wamefungiwa ndani ya majumba yao, hakuna anayeruhusiwa kutoka nje, Polisi wanapiga mabomu ya machozi kila mtaa huku wakiwasaka watuhumiwa waliosambaza vipeperushi na kuwatawanya wandamanaji waliozagaa katika mitaa  mbalimbali, mpaka hivi sasa kuna mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya raia na Asakari Polisi wanaotumia mabomu ya machozi na silaha zigine za moto"alisema shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo imedaiwa kuwa hali hiyo imesababisha barabara zote kufungwa kiasi cha kuzuia mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU yametanda kila kona za mji, huku taarifa zidi ikifafanua kwamba hakuna mawasiliano, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi ya nyumba maeneno ya Shangani zimechoma moto.


Tuesday, May 21, 2013

HII NDIO RATIBA YA KAGAME CUP NA MAKUNDI WALIYOPANGWA SIMBA NA YANGA




















Droo ya makundi kwa ajili ya mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati al-maarufu kama (KAGAME CUP) imefanyika leo mchana mjini Khartoum nchini Sudan huku Mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Young Africans wakipangwa kundi C kwenye michuano hiyo itakayoanza 18 Juni - 2 Julai 2013.
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye imeonyesha mashindano ya mwaka huu itakua na jumla ya timu 13 kutoka katika nchi 10 wanachama ambapo droo hiyo imegawanyika katika makundi 3 ya A,B,C.
Timu zitakazo shiriki mashindano hayo na nchi zinazotokea kwenye mabano ni : Al-Hillal, El-Merreikh na Al Shandy (Sudan), Al Nasri (Sudan Kusini), Yanga & Simba (Tanzania), Express (Uganda), Tusker (Kenya), APR (Rwanda), Vitaloo (Burundi),  Ports (Djbouti), Elman (Somalia) na Falcon (Zanzibar)
Aidha mashindano ya mwaka huu yameongeza zawadi kwa washindi kutoka kitita cha dola za kimarekani 60,000 mpaka kufikia dolla 80,000 ikiwa kuna ongezeko la dola 20,000 ambapo zawadi kwa washindi zitapangwa na kamati ya utendaji kabla ya mashindano kuanza.
Mashindano ya CECAFA mwaka huu yatafanyika nchini Sudan katika miji ya El-Fashir na Kadugli ambayo ni miji iliyopo kusini mwa nchi ya Sudan yenye wakazi wapatao milioni 34 na eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 1,886,068.
Makundi ya michuano hiyo itakayoanza mwezi ujao ni kama ifuatavyo:

KUNDI A: El-Merrekh -(Sudan), APR (Rwanda), Simba SC (Tanzania), Elman (Somalia) - EL FASHER

KUNDI B: Al-Hillal (Sudan), Tusker (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar),  Al Shandy (Sudan) - KADUGLI

KUNDI C: Yanga SC (Tanzania), Express (Uganda), Ports (Djibout), Vitaloo (Burundi) - EL FASHIR

 KAGAME CUP FIXTURE 18th JUNE - 2nd JULY 2013 (EL-FASHIR & KADUGLI - SUDAN)
DATETEAMTEAMGROUP/TIMEVENUE
18.06.2013.TUSKER SUPER FALCON B - 2:00 PMKADUGLI
 AL HILLAL AL NASRI B - 4:00 PMKADUGLI
19.06.2013.VITALOOPORTS  C - 4:00 PMEL-FASHER
20.06.2013.YANGA SC EXPRESS C - 2:00 PMEL-FASHER
20.06.2013.ELMAN FC APR FC A - 4:00 PMEL-FASHER
20.06.2013.SUPER FALCON AL NASRI B -2:00 PMKADUGLI
20.06.2013.TUSKER AL-SHANDY B - 4:00 PMKADUGLI
21.06.2013.EL MERREIKH SIMBA SC A - 4:00 PMKADUGLI
22.06.2013.EXPRESS FC VITALOO C - 2:00 PMEL-FASHER
 PORTS YANGA SC C - 4:00 PMEL FASHER
22.06.2013.AL NASRITUSKER B - 2:00 PMKADUGLI
 AL SHANDY AL HILAL B - 4:00 PMKADUGLI
23.06.2013APR SIMBA SC A - 2:00 PMEL-FASHER
 EL MERREIKH  ELAM FC A - 4:00 PMEL-FASHER
24.06.2013AL NASRI AL SHANDY B - 2:00 PMKADUGLI
 SUPER FALCON AL HILLAL B - 4:00 PMKADUGLI
24.06.2013. PORTSEXPRESS FC C - 4:00 PMEL-FASHER
25.06.2013.VITALOO YANGA SC C - 4:00 PMEL-FASHER
26.06.2013.AL SHANDY SUPER FALCON B - 2:00 PMKADUGLI
 AL HILLAL TUSKER B - 4:00 PMKADUGLI
26.06.2012.SIMBA SC ELMAN FC A - 2:00 PMEL-FASHER
 APR FC EL MERREIK A - 4:00 PMEL-FASHER
27.06.2013.REST DAYREST DAYREST DAY  REST DAY
28.06.2013.(23) B2 VS C2(24) B1 VS BEST QTBDKADUGLI
28.06.2013.(25) C1 VS A2(26) A1 VS B3TBDEL-FASHER
30.06.2013.WNR 23 VS WNR 25WIN 24 VS WIN 26TBD 
01.07.2013.REST DAYREST DAYREST DAYREST DAY
02.07.2013.LOOSER LOOSER 283RD - TBDEL-FASHER
  WINNER 27 WINNER 28  FAINAL - TBDEL-FASHER




AZAM TV KUONESHA LIGI KUU YA TANZANIA BARA MSIMU UJAO WA 2013/2014



Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) inayomiliki klabu tajiri ya Azam FC ipo mbioni kumwaga zaidi ya 1.5 bilioni kwa timu zote za ligi kuu Bara msimu ujao na itarusha moja kwa moja (Live) zao kupitia televisheni yao mpya ya AZAM TV ambayo inatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni ambapo ujenzi wa kituo hicho unaendelea katika Jengo moja lililopo Barabara ya Mandela, Jijini Dar es Salaam.

Habari za uhakika zinasema Azam itauza Ving'amuzi na inakusudia kutoa kiasi cha shilingi Milioni 100 kwa kila timu kwa timu zote 14 zitakazo shiriki ligi kuu msimu ujao na Mkataba huo utakuwa ni wa miaka mitano (5). Kamati ya ligi chini ya Wallace Karia na viongozi wa TFF walikutana na klabu za ligi kuu kujadili mkataba huo ambao utazipunguzia mzigo klabu ndogo ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ukata kutokana na kutegemea udhamini wa Vodacom pekeyake ambao hautoshi.




RAIS OBAMA KUJA TANZANIA MWEZI WA SITA

Habari imetangazwa kwenye BBC NEWS WORLD ikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack Obama  kuja Tanzania itakuwa ni tarehe 1/06/2013




MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YAREKEBISHWA KUFICHA AIBU


MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.

“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.

 "Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa.

" Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika na wanafunzi wapya, yaani kama wanaanza kidato cha kwanza wawe wanapewa mitihani ya kupimwa kwa kuzingatia alama mpya na waendelee nazo hadi mitihano yao ya mwisho.

“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato cha tano mara wanapoanza shule, kila mitihani wanayopewa isahihishwe na kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka NECTA.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya alama, alama mpya zilizokuwa zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34 hadi sifuri; badala ya alama hiyo F kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia 35 tofauti na awali, yaani alama 21.

Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita tofauti na muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa kidato cha nne ambapo matokeo yalitangazwa na kisha kufutwa ili kuyapanga upya kwa kutumia alama za zamani.

Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema; “Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa kuandaa matokeo ya kidato cha sita unaendelea, siwezi kusema lini hasa utakamilika lakini nina uhakika ni katika muda muafaka.”

Kuhusu matokeo ya kidato cha sita kucheleweshwa kutokana kupangwa upya ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana na matumizi ya alama mpya za kufaulu, Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa kuzingatia alama za zamani) yamekuja wakati mchakato wa kuandaa matokeo ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa kufuata maagizo hayo.”

Hata hivyo, hakuweka bayana kama matokeo ya awali kabla ya maagizo ya Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia alama za zamani yamewafanya wanafunzi wengi kufeli na badala yake akasema; “Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato wa matokeo hayo haukuwa umefika mwisho. Takwimu rasmi hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si sahihi kusema rasmi walifeli.”

Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa matokeo yanayotarajiwa ya kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi 50,000 wamepata unafuu katika matokeo yao tofauti na awali.

Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yaliyotangazwa Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Katika matokeo hayo idadi ya wasichana waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi 80,686 na idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361.

Katika matokeo hayo watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni 15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903 lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo itabadilika kwa sababu ya alama kuongezwa kwa watahiniwa hao wa mwaka 2012.

Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja na vituko walivyofanya baadhi ya wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani na kutokana na makosa hayo, watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao.

Source: Raia Mwema


MMOJA WA WAPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA AZIKWA LEO

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais wastaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes, mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika na wa waasisi wa chama cha TANU, leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwet akiongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes, mmoja wa waasisi wa chama cha TANU, leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2013.PICHA NA IKULU.


PICHA YA MBUNGE TUNDU LISSU ALIPOTAKA KUMPIGA ANNE KILANGO


Baada ya Bunge kuahirishwa jana, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.

 
Maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.


PICHA ZA PROFESA JAY AKIJIUNGA NA CHADEMA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Joseph Haure (Profesa J) kushoto akionyesha kadi ya Chadema kulia ni Mbunge wa Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu)

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imeongeza idadi ya makamanda kutoka katika kundi la Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Joseph Haule (Profesa J).
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni aliyesoma hotuba ya  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ndiye alisimamia zoezi zima la kumpokea mwanachama huyo mpya.
Profesa J alijikuta katika mtandao wa Chadema kirahisi baada ya kutinga katika kikao cha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Ingawa Profesa J pekee ndiye aliyefanya uamuzi wa kujiunga na Chama hicho kilichojizolea umaarufu mkubwa katika miaka ya hivi karibuni hususan katika Jimbo la Mbeya Mjini inayongozwa na Sugu.
Wasanii wengine waliotinga katika Jiji hilo ni pamoja na Judith Wambura(Laddy jdee),Joseph Haule(Profesa J)Mkoloni na wengine
 

Kitendo cha Profesa Jay kuchukua kadi ya CHADEMA au wasanii kujiingiza kwenye siasa kinatupa mwanga gani kwanzia kampeni mpaka uchaguzi 2015?? kwangu naona watasaidia kuwaelimisha wengi na kuwapa motisha ya kupiga kura!!!! wewe unafikiria nini????.........................


######LIKE PAGE#############
Sugu na Prof Jay





Monday, May 20, 2013

HATIMAYE MBUNGE WA IRINGA MJINI AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mh Msigwa akishuka kwenye gari la polisi kuingia mahakamani
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji,  Peter Msigwa akishuka katika gari ya  polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana  huu katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa  wa Iringa  pamoja na  watuhumiwa  wengine  zaidi ya 60 .
 
Ulinzi mkali uliwekwa katika eneo hilo la mahakama  kuzuia wafuasi  wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuingia eneo la Mahakama jambo lililowafanya wafuasi hao kushindwa kushuhudia vyema kesi hiyo, inayomkabiri Mbunge wao, kwa vile walilazimika kushuhudia wakiwa nje ya geti

 Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi  wengine wa chadema mahakamani hapo huku  wafuasi  wao  wakizuiwa nje ya mahakama
 Wafuasi  wa Chadema  wakiwa  wamezuiliwa nje ya viwanja  vya mahakama kuu kanda  ya Iringa  wakati mbunge  alipofikishwa katika mahakamani   mchana  huu


WIMBO MAALUMU KWA AJILI YA USHINDI WA YANGA





VIDEO YA YANGA WAKIPOKEA KOMBE NA JINSI NGASSA ALIVYOBEBWA NA WASHABIKI WA YANGA




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU