Facebook Comments Box

Monday, April 22, 2013

LULU KATIKA MOVIE MPYA

www.kitongoni.blogspot.com



ANGALIA USHANGILIAJI MPYA WA MASHABIKI WA YANGA




LADY JAY DEE: MNAFIKI WA MIAKA 10 SHUJAA WA SIKU 30

 

Imeandikwa na Saleh Ally

MGOGORO wa kimuziki kati ya msanii Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na kituo kimoja cha redio umezidi kuchukua kasi huku makundi mawili, kila moja likitengeneza ngome yake na kuamini linachoamini.

Kundi ambalo linamuunga mkono Jaydee na kumuona ni mkombozi, anazungumza kwa niaba yake na wasanii wengine, la pili ni lile linalobaki upande unaoshambuliwa, linatetea ngome yake.

Jaydee anashutumu kubaniwa nyimbo zake na kituo hicho ambacho kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ameeleza wazi kuwa wanambania, wanaziponda lakini hata watangazaji wake wamekuwa wakionyesha chuki binafsi dhidi yake.

Jaydee pia aliwaponda wasanii Ben Pol na Linah anayetokea THT kwamba walishindwa kutokea kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Joto Hasira, kwa madai walizuiwa na bosi wao.


Ujasiri huu wa Jaydee ndiyo kitu bora ambacho kimekuwa kikitakiwa kufanyika kutoka kwa wasanii, yaani wapigane kutetea muziki wa Tanzania hasa kama kuna watu au kundi la watu limejikita katika kuuangamiza.

Lakini ni tofauti kidogo, kwani wasanii wengi wamekuwa imara na kuwa tayari kujitetea wenyewe tu na si vingine. Nasisitiza mara nyingi, wao ndiyo wahusika wa kwanza na wanapaswa kuanzisha mapinduzi kuanzia kwao, mfano kusema naonewa si kitu kibaya lakini je, umewahi kupigania wanaoonewa?

Kujitetea pekee unaweza kufanya, lakini vipi utafanikiwa kama asilimia kubwa ya kundi la wanamuziki linaendelea kuonewa. Ukibaki hauonewi pekee na asilimia kubwa ya wasanii au wanamuziki inaonewa, kunaweza kuwa na 
mapinduzi sahihi?

Ndiyo maana nashangazwa kusikia Jaydee leo anaona ubovu wa kituo hicho, anathubutu kusema hadharani akionyesha wazi ameumia. Lakini miaka 10 au zaidi iliyopita, Jaydee alikuwa kimya na hakuwaza kusema kwamba kituo hicho kinawabania wasanii wengine na ‘kumtukuza’ yeye hata kama muziki wake haukuwa wa kiwango kilichokuwa kinazungumzwa.

Siwezi kusema muziki wa Jaydee ni mbaya, nimekuwa kati ya mashabiki wake. Lakini yoyote atanichekesha akisema nyimbo albamu zake zote alizotoa zilikuwa katika kiwango cha juu sana na ndiyo maana leo ni maarufu.

Hakuna asiyejua kwamba miaka nenda rudi, wasanii wamekuwa wanaongoza kwa unafiki, kutopendana wenyewe, kugeukana na hata kujenga makundi lukuki, ndiyo maana kila kukicha wamekuwa wakishambuliwa maana katika maisha yao hawana umoja.

Jaydee alianza kuwa mtangazaji katika kituo hicho baada ya kuacha kurap, akaamua kuachana na kurap na mwisho kuwa msanii wa nyimbo za kubembeleza, mara ya kwanza akianza kutikisa na albamu ya Machozi, Solo Thang anaweza kuhadithia vizuri kuhusu hili.

Kuanzia albamu ya Machozi, kituo hicho ndicho kilisimama kuhakikisha anakuwa bora hata kama muziki wake haukuwa ukimzidi kila mwanadada wakati huo.

 Angalia, kulikuwa wasanii kama Stara Thomas, Carola Kinasha ambao kiuwezo walikuwa juu kuliko Jaydee, lakini hawakupewa nafasi ya kutosha, badala yake Jaydee ambaye hakuthubutu kuwatetea hata kidogo akaendelea ‘kubebwa’ na watu wakaamini ni bora kuliko yeyote kwa upande wa akina dada au kina mama katika kuimba, haikuwa hivyo.

Angalia albamu ya Binti, karibu nyimbo zote zilikuwa na ujumbe mmoja, ulikuwa ukimshambulia mwanaume mmoja ambaye alikuwa amemuumiza Jaydee. Takribani ujumbe wa nyimbo karibu zote ulikuwa ni mmoja, lakini ilibebwa na kuonekana ni moja ya albamu bora kabisa kuwahi kuwepo katika muziki wa Tanzania, kitu ambacho hakikuwa sahihi.

Wakati huo wasanii lukuki walilia kubaniwa, mmoja wao alikuwa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ndiye alimtambulisha mwanadada huyo alipomshirikisha katika wimbo wa Mambo ya Fedha, kabla ya hapo hakuwa na jina. Jaydee hakuwahi kuungana naye hata kidogo hata kwa mstari mmoja wa kumtetea au kuunga mkono kutetea muziki wa Tanzania, kuonyesha anapinga mwenendo wa wanaolazimisha kuwabagua wasanii au kufanya mambo kwa mabavu kwa kuwa wameshika mpini.

Hakuna aliyesikia kilio cha Sugu, wasanii wanaochipukia bila ya kujua wasemacho, kisa nyimbo zao zinapigwa redioni, ili kuonyesha shukrani za dhati wakaanza kutangaza Sugu anatapatapa na amekwisha kimuziki!

Ajabu, asilimia kubwa ya maneno yake ndiyo yanayozungumzwa leo, ndiyo yanatumiwa na kila msanii anayebanwa au kuhisi kaonewa. Angalia, hata Jaydee naye ameingia huko! Swali langu hapa je, Jaydee na wengine wanaolalamika, wamekwisha kisanii?

Ndiyo maana nasema, tasnia ya muziki hasa muziki wa kizazi kipya umejaza watu wavivu kufikiri, wenye mioyo ya ‘Kichina’, wasio na uwezo wa kuthubutu hata kidogo ambao wanasubiri wayumbe au kuumizwa wao ili wamtafute wa kumuangushia lawama.

Jiulize, kama Jaydee alibebwa kwa miaka 10, halafu leo analalamika atakuwa sahihi? Sitaki kumpinga kwa kuwa kuna kitu anakiona lakini ninaamini alikiona tokea mapema, akauchuna.

Bado nasisitiza, yeye na wengine wote wanaolia baada ya kuguswa wao nawaita wanafiki, wanapigana kwa ajili yao na si kwa muziki wanaoutumikia. Iwapo wangekuwa tayari kupambana kwa ajili ya muziki huo, msanii kama Jaydee asingeanza vita leo.

NARUDI KWA JAYDEE


Sijawahi kuingia naye katika malumbano zaidi ya miaka 10 tokea alipokuwa mwanahabari mwenzangu na sasa msanii. Lakini nathubutu kumueleza kuwa ni kati ya wasanii wasiojali muziki wa Tanzania na wanajiangalia wao zaidi.

Picha ya unafiki na kujiangalia mwenyewe inaonekana sasa ingawa takribani miaka mitano iliyopita nilianza kuinusa. Leo analia, anabaniwa na anauona moto unaounguza muziki wa Tanzania ulivyo mkali.

Naamini aliuona miaka kibao nyuma, lakini kwa kuwa alikuwa akitetewa hakuweza kuangalia kwamba rafiki zake, wasanii waliombeba kabla walikuwa wakiungua. Akaendelea kuwapita kwa raha zake mustarehe.

Tungeweza kumuita Jaydee ni mpambanaji kama angewakosoa hao anawakosoa sasa katika kipindi walichokuwa wamempa mbeleko yeye, basi kweli ingeonekana anapigania muziki wa Tanzania. Sasa anapigania chake tu!

Jaydee amefika mbali kimuziki, alikuwa bora jukwaani na nyimbo kadhaa na nyingi zikapewa ‘over promotion’ lakini bado ninaweza kumuita mkongwe. Ajabu alibaki chipukizi hadi leo katika suala la kutetea haki za wasanii na muziki wenyewe.

Sitaki kumkatisha tamaa kwa mapambano aliyoyaanza, ninaamini ana nafasi ya kuanza kuusaidia muziki ambao umemsaidia. Lakini ndiyo kipindi ambacho anaweza kupata machungu waliyopata wasanii wenzake kunyeshewa mvua na kuunguzwa na jua wakati akiwa kivulini kwa ‘msaada’.

Anachokifanya leo Jaydee ni nyongeza tu ya walichokifanya Sugu au Afande Sele au wasanii wachache walioamua kuwa wakweli au wale walioamua kuwa wabunifu kama Ambwene Yessaya ‘AY’, aliyekimbia vita ya redio na kuingia katika kurekodi video bora zilizoendelea kumng’arisha.

Simzuii, Jaydee kuendelea kupambana, lakini namuasa anachokifanya kama ni kwa ajili ya muziki akipozwa tena, asirudi nyuma.

Ninachomkumbusha, hata yeye amekuwa kundi moja na analowalaumu ambao angeweza kuwashauri mapema ‘ndani ya mjengo’ kama angekuwa na nia nzuri na muziki wa kizazi kipya.  Msisitizo ‘Joto Hasira’ liwe la kweli.

Source: WAVUTI


Sunday, April 21, 2013

ANGALIA PICHA ZA MKUTANO WA CCM MOROGORO NA WA CHADEMA MWANZA

Leo, vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA vimefanya mikutano ya hadhara katika maeneo tofauti nchini Tanzania.

CCM mkoani Morogoro.
CHADEMA mkoani Mwanza.
Picture
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro jioni hii, ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku nane mkoani Morogoro. (picha Bashir Nkoromo/CCM Blog)
Picture
Wananchi wakimshangilia mwanamuziki Diamond (picha Bashir Nkoromo/CCM Blog)
Picture
Nape Nnauye akihutubia (picha Bashir Nkoromo/CCM Blog)
Picture
Diamond akitumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro (picha Bashir Nkoromo/CCM Blog)
Picture
Msanii Lina akitumbuiza kwenye mkutano huo (picha Bashir Nkoromo/CCM Blog)
Picture
Wasanii Chege na Temba kutoka TMK Family wakishambulia jukwaa wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye mjini Morogoro jioni hii (picha Bashir Nkoromo/CCM Blog)
Picture
Wananchi wakisikiliza viongozi wa CHADEMA wakihutubia, Mwanza (picha: Peter Msigwa)
Picture
Mbunge, Highness Kiwia akihutubia (picha: Peter Msigwa)
Picture
Mch. Mbunge Peter Msigwa akihutubia (picha: Peter Msigwa)



HUU NDIO USHAHIDI WA SUAREZ KUMNG'ATA IVANOVIC UWANJANI LEO

Huu ni ushahidi wa  picha ukimuonesha Luis Suarez akimng`ata Ivanovic leo kwenye mechi ya Liverpool dhidi ya Chelsea ambapo timu hizo zilitoka droo ya magoli mawili kwa mawili



Saturday, April 20, 2013

DARASA LA SABA SASA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU

Jengo la Chuo Kikuu Dodoma(Udom) moja ya vyuo vitakavyo tumika katika utaratibu huo mpya
 
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”
Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.

SOURSE: MWANANCHI


VIDEO: MADEE- NANI KAMWAGA POMBE YANGU




VIDEO: ANGALIA MAJIBIZANO YA RISASI KATI YA WALIPUAJI WA BOSTON NA POLISI




MWALIMU ATUHUMIWA KUMUAMBUKIZA VVU MWANAFUNZI

 Na Gordon Kalulunga - Mbeya 

IMEELEZWA kuwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Vanessa (jina linahifadhiwa) iliyopo Mkoani Mbeya aliyekuwa na mahusiano ya kingono mwalimu wake aitwaye   John Mapunda ameambukizwa virusi vya UKIMWI (VVU).

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka (17) wakati anahusiana kingono na mwalimu wake alikuwa anajiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2012 lakini hakuweza kufanya mtihani huo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, Mwalimu Mapunda alikuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi wake tangu mwaka 2011 akiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo na wakati mwingine mwanafunzi huyo  alikuwa  analala nyumbani kwa Mwalimu  wake huyo kwa siku kadhaa, kama mkewe.

Vyanzo vya blogu ya Kalulunga vimeeleza kuwa mwalimu huyo ambaye anafundisha somo la jiografia alifanikiwa kumtongoza na kumrubuni mwanafunzi huyo tangu akiwa kidato cha kwanza kwa kumwongezea maksi kila mtihani unapofanyika.

Baada ya wazazi wa mtoto kufuatilia nyendo za mtoto baada ya kupotea kwa siku tatu mfululizo, wazazi walitoa taarifa  Central Polisi Mbeya ambapo Polisi walianza kufuatilia.

Siku tatu baadaye, mwanafunzi huyo wa kike alirejea nyumbani kwao. Wazazi walimpeleka Polisi. Alipobanwa, aliwaambia Polisi kuwa ametoka  kwa mwalimu Mapunda na kukiri kufanya naye ngono bila kinga.

Habari za kiuchunguzi zimeeleza kuwa Polisi na wazazi waliamua kwenda kumpima afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambapo majibu yalionesha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameambukizwa VVU.

Uchunguzi umebaini kuwa, jalada la uchunguzi wa polisi lipo chini ya askari anayefahamika kwa jina la Andrea Mwambembe na askari mwingine aliyefahamika kwa jina la Mwashiwuya.

Lakini katika hali ya kustaajabisha, inadaiwa askari hao walipokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa kumfuata mwalimu Mapunda kazini kwake, walipofika, Mkurungenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Shukran Mwasajobe alimshitua Mwl. Mapunda  na kusababisha kutorokea wilayani Chunya.

Siku iliyofuata Shukran anadaiwa kumfuata Afande Justine Kayombe na Afande mwanaume  lakini mwenye simu iliyosajiliwa kwa jina la Judith Juma, ili kumalizazana na tatizo hilo.

Katika hali ya kushangaza, Shukran baada ya kukutana na askari hao na kuweka mambo sawa, alionekana akimfokea askari  Sponsor Millinga na kwenda kumlalamikia kuwa anatafuta rushwa kwake.

Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa mwalimu Mapunda hajakamatwa kwa kosa lolote na mwanafunzi aliyebakwa ameshindwa kufanya mtihani huku wazazi wakilalamika.

Kwa sasa mwalimu Mapunda, Shukran na Afande Justine Kayombe wanadaiwa kuwa maswahiba na mara kadhaa wanaonekana wakiwa pamoja katika hoteli ya Moon Dust iliyopo kata ya  Ruanda eneo la Soweto Mkoani Mbeya.

Taarifa kutoka Ofisi za Ukaguzi kanda zinaonyesha kuwa mwalimu huyo  amekuwa na kashfa ya ngono tanga akiwa katika Shule ya Montifot Sekondari iliyopo Usangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya, na alifukuzwa hapo kabla ya mwakza 2008 baada ya kutuhumiwa kosa kama hilo, la kufanya mapenzi na mwanafunzi.

Taarifa kutoka kwenye familia ya mwalimu huyo  zinaonyesha kuwa  kati ya mwaka 2007, muda mfupi kabla hajafukuzwa kazi katika Shule ya Montifot, mwalimu huyo alianza kukorofishana na mkewe katika suala la ufuska na walipohamia jijini Mbeya, mkewe alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kike ndani na hivyo ndoa yao kuvunjika papo hapo, huku mkewe akirejea nyumbani kwao mkoani Tanga.

Ili kuzima sakata hilo, Mkurugenzi wa shule hiyo anadaiwa kutaka kumfukuza Mkuu wa shule hiyo ambaye anaonekana kuhoji mara kadhaa juu ya sakata hilo ili hali yeye tayari anadhani amelimaliza polisi.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU