Sir
Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea
Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME
ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK
Wanaume Family.
Monday, April 1, 2013
ANGALIA JUMA NATURE ALIVYOTAWAZWA RASMI KUWA MFALME WA TEMEKE BAADA YA KUWABURUZA TEMEKE FAMILY
WAKAZI WA BUKOBA WAMLAKI DIAMOND PLATNUMZ KWA KISHINDO
Jana msanii Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz alitua mjini Bukoba,
Kagera kuendelea na ziara yake ya kutumbuiza mikoa ya kaskazini
magharibi. Kama
inavyoonekana kwenye picha, umati mkubwa wa watu ulijitokeza kumlaki
Diamond, kitu ambacho kilimpelekea msanii huyo kuchomoza juu ya gari
kuwasalimia.
Kwa mujibu wa Diamond’s official website, kitendo cha
Diamond kujichomoza juu ya gari kilisababisha msongamano mkubwa zaidi,
na kusababisha barabara kufungwa, na baadhi ya kazi kusimama kwa muda.
“Juzi….Tarehe
30 march niliwasili salama salimini mjini bukoba Mkoani Kagera….Pili
niwashukuru Mashabiki zangu wote Mkoani Humu kwa kunipokea kwa hali na
mali ,Hii inaonyesha jinsi gani watanzania wanathamini na wana mapenzi
na wasanii wao…..!!” aandika Diamond.
Aliongeza “Nililazimika
kutoka Juu ya Gari kuwasalimu kabla sijaelekea hotelini…. Nilivotokeza
hali ilizidi kuwa mbaya zaidi….Polisi walilazimika kufunga barabara
kadhaa mjini bukoba na hata kazi zingine kusimama kwa muda kutokana na
watu kuzingira Gari nilokuwepo kila kona nilipokuwa napita”.
SOURCE:Diamond
KAULI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA BAADA YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16 DAR ES SALAAM
Picha hii kwa hisani ya maktaba:
Tarehe 29 Machi 2013, mnamo saa mbili na nusu asubuhi jengo linalojengwa kwenye kiwanja namba 2032/73 Mtaa wa Indira Gandhi lilianguka kutokana na sababu ambazo bado hazijathibitishwa kitaalam na mamlaka husika. Shirika la Nyumba la Taifa linasikitika sana kutokana na kuanguka kwa jengo hilo pamoja na maafa yaliyotokana na tukio hilo la kusikitisha. Pia Shirika linatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba uliotokana na ajali hii.
Mradi huu wa ubia kati ya NHC na M/s Ladha Construction Limited ya Jijini Dar Es Salaam ulianza kutekelezwa tarehe 4 Februari 2008 ambapo Shirika la Nyumba litakuwa na hisa asilimia 25 na mbia ana asilimia 75 mara baada ya mradi kukamilika. Kwa mujibu wa sera ya ubia iliyoanza kutumika mwaka 1993 na kuhuishwa mwaka 1995 na 2005, Shirika la Nyumba la Taifa lilikuwa likitoa ardhi ambayo ilikuwa ikihesabika kama asilimia 25 ya mtaji wake kwenye jengo husika na mbia alikuwa akipata asilimia 75.
Kwa mujibu wa mkataba huo mbia mwendelezaji M/s Ladha Contruction Limited kama walivyo wabia wengine, anapaswa kabla ya kuanza ujenzi kupata vibali kutoka kwenye mamlaka husika na kuwa na wataalam wa ujenzi na washauri waliokubalika na kuthibitishwa na mamlaka husika. Aidha, mbia huyu akishapata wataalam hao ndiye anayehusika kuingia nao mikataba ya kazi ya kujenga na kusimamia ubora wa jengo husika kwa mujibu wa sheria. Katika mradi huu mbia mwendelezaji aliajiri wataalamu wote waliosajiliwa na Mamlaka husika ambazo ni CRB, ERB, AQRB na Mansipaa husika na mamlaka nyinginezo. Kwa kuwa ujenzi ulikuwa bado haujakamilika, Shirika lilikuwa bado halijapata asilimia 25 ya umiliki wake.
Pia tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, Shirika la Nyumba la Taifa, lilisimamisha utoaji wa miradi mipya ya ubia mwaka 2010 ili kuweza kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa miradi ya ubia na hivyo kuwezesha kutengeneza sera mpya. Kama sehemu ya zoezi hilo, shirika pia lilifuta jumla ya mikataba 64 ambayo ilikuwa imesainiwa lakini haijaanza ujenzi.
Katika sera mpya ambayo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni Shirika litahusika moja kwa moja katika kuteuwa mjenzi mtaalam (contractor), msimamizi mtaalam wa mradi husika (consultant) na kusimamia kikamilifu shughuli zote za ujenzi.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya vyombo husika kuwasiliana na mjenzi wa mradi huu. Aidha, taarifa zinaweza kupatikana moja kwa moja kutoka M/s Ladha Construction Limited ambaye ndiye mbia mwendelezaji aliyekuwa anasimamia ujenzi huu.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII S.L.P. 2977 Simu: 2851590 DAR ES SALAAM
Telegrams : "NYUMBA" TANZANIA
Fax 2851442

Sunday, March 31, 2013
LADY JAY DEE: CLOUDS FM NI WANAFIKI WANATAKA WAHONGWE NDIPO WAPIGE NYIMBO ZA WASANII
Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.
"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. "Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"
Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhuru. Nakunywa maziwa daily, I will survive".
"Hee! Kuna watu wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"
" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"
Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa.
SOURCE:JAMII FORUM

YANGA WAKAMATWA NA POLISI HUKO MKOANI MOROGORO
UHURU KENYATA AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMANI BAADA YA MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUWA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA HAKI
MAHAKAMA:
Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili 9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.
uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nne walichaguliwa kwa
haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi huu, akimaanisha Kenyatta na
mgombea mwenza na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.
Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa
kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta
binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani,
utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya
asilimia 43,28 za Odinga.

Saturday, March 30, 2013
MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL ALIPOTEMBELEA ENEO LILIPODONDOKA GHOROFA JANA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dk. Gharib Bilal akiwa eneo la tukio ili kujionea mwenyewe pamoja na kupata maelezo kutoka kwa mashuhuda wa ajali ya kudondoka kwa Jengo la Ghorofa 16 jana asubuhi katikati ya Jiji.
Makamu wa Raisi Dk. Gharib Bilal akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa JWT kama anavyoonkana katika picha.
Askari wa JWTZ wakisaidiana na Wananchi kusukuma Jenereta kubwa kulisogeza eneo la tukio ili eneo hilo liwe na mwanga wakati wa usiku na kuwezesha uokoaji kuendelea hadi jana usiku.
Friday, March 29, 2013
DIAMOND NA WEMA WATAMBIANA KATIKA PESA
Wakati WEMA ISACK SEPETU akifungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, aliyekuwa Mpenzi wake Nasibu Abdul 'DIAMOND PLATNUM' amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliomgharimu takriban Shilingi za Kitanzania Milioni 260 hivyo kwa pamoja kuonesha jeuri ya pesa walizo nazo.
WEMA alifanya uzinduzi wa ofisi yake hiyo bila kumpa taarifa Mama yake mzazi MARIAM SEPETU ili iwe bonge la Surprise kwake pamoja na watu mbalimbali kama vile Diamond Platnumz mwenyewe siku ya Jumatano iliyopita, Jina la Ofisi hiyo ni ENDLESS FAME FILMS iliyopo Mwananyamala- Komakoma Jijini Dar es Salaam.
Wema akiwa Nyumbani kwake.
Wema akitoka kwake na gari yake aina ya Audi Q7.
Pamoja na Diamond kutoalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Ofisi hiyo ya Wema lakini chanzo cha habari kinasema alikuwa katika harakati za kumalizia Mjengo wake ulioko Tegeta ili nae afanye uzinduzi rasmi. Akizungumza na kitongoni blog akiwa
kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa ‘finishing’,
Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260 ni
zawadi kwa mama yake SANURA KASSIM ‘SANDRA’.
“Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo,” alisema Diamond.
Diamond alimzungusha paparazi
wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote
ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya
kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la
kuogelea ‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya
kufanyia mazoezi (gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu
kila kitu kitakuwa kimekamilika.
Hii ndiyo Nyumba ya Diamond anayojenga huko Tegeta na gari linalo onekana hapa ndilo gari lake anlotumia ukiachilia mbali Altezza aliyo mnunulia Mama yake.Ukiachana na ukubwa wa nyumba
hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine
ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo zitakuwa zikipangishwa.
Diamond akiwa Nyumbani kwake Sinza Mori anapoishi sasahivi.MHANDISI MKUU NA MHANDISI WA WILAYA YA ILALA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16
Bango linaloonesha Ujenzi wa Ghorofa lililoporomoka leo Jijini Dar es Salaam, Jengo ambalo Mhandisi Mkuu na Mhandisi wa Wilaya ya Ilala wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa Uchunguzi zaidi.
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Dar es Salaam Suleiman Kova wakati alipofika eneo la tukio ambapo Jengo la ghorofa 16 liliporomoka leo katika makutano ya Mitaa ya INDIRA GANDHI na ASIA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia kwa pamoja MHANDISI MKUU WA JENGO na MHANDISI WA WILAYA YA ILALA kutokana na kuporomoka kwa Jengo la ghorofa 16 leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.
Kwani Mhandisi wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyetoa kibali cha kujengwa jengo hilo na Mhandisi Mkuu kuwa yeye ndiye msimamizi mkuu wa Ujenzi katika jengo hilo. Lakini pia MKUU WA MKOA wa Dar es Salaam amesitisha ujenzi wa jengo lingine lililopo pembezoni mwa Jengo lililoporomoka ambalo pia linasimamiwa na Mhandisi huyo huyo anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi.
Kwa Habari zaidi juu ya Tukio hilo endelea kufuatilia kwa karibu kitongoni blog
Subscribe to:
Posts (Atom)