Facebook Comments Box

Wednesday, January 2, 2013

HII NDIO SIKU AMBAYO SAJUKI ATAZIKWA

TAARIFA ULIYOKO MPAKA MUDA HUU NI KUWA MAZISHI YA JUMA KILOWOKO 'SAJUKI' YATAKUWA IJUMAA SAA TANO KWENYE MAKABURI YA KISUTU DAR ES SALAAM

HALI ILIVYO NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI

 Mke wa marehemu, Juma Kilowoko 'Sajuki', Wastara Juma, akiwa na simanzi nzito kwa kumpoteza mumewe.
 Baba mzazi  wa marehemu, Juma Kilowoko 'Sajuki' akiwasiliana na ndugu na jamaa msibani hapo.…
 Dada wa marehemu Sajuki akilia kwa uchungu.


Bibi wa marehemu Sajuki akiwasili msibani leo.
Pichani juu ni baadhi ya taswira za waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki', Tabata- Bima jijini Dar es Salaam. Sajuki amefariki dunia leo alfajiri akiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ambapo alikuwa akitibiwa.


BREAKING NEWS: SAJUKI AFARIKI DUNIA

Msanii wa filamu nchini Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa mujibu waa katibu wa chama cha waongoza filamu wilaya ya ilala Juma Amir Sajuki alikuwa akisumbuliwa na upungufu wa damu.
Sajuki alipata maradhi ambayo yalisababisha aende kutibiwa India. Hivi karibuni akiwa jukwaani Arusha Sajuki alizidiwa na kushindwa kusalimia washabiki wake.
Hivi sasa ilikuwa ikifanyika mipango apelekwe India tena na milioni 28 zilikuwa zikitafutwa kwa safari hiyo.
Inna Lillah wa inna illah rajiuun.

Tuesday, January 1, 2013

MH LOWASSA AFANYA KALI YA MWAKA MPYA: USHAHIDI WA PICHA HUU HAPA

Waziri mkuu msataafu Mh Edward Ngoyai Lowassa amefanya sherehe kubwa sana ili kuukaribisha mwaka mpya na kuuaga mwaka 2012. Akiwa kama leigwanani amewaalika watu mbalimbali katika sherehe hiyo.

Wananchi wa monduli wakienda kwa Mheshimiwa kusheherekea mwaka mpya

Hapa pilau likiandaliwa

Magari ya wageni mbali mbali wa sherehe hiyo. Ulinzi ukiwa umezingatiwa

Vijana kutoka pande mbalimbali za Tanzania walishiriki katika sherehe hiyo


Ulinzi ni wa kutosha kabisa

Wageni waalikwa wakiwa kwa kiongozi wao mpendwa Leigwanan Lowassa
Chifu Chege nae alialikwa

Laigwanan akisalimiana na kijana Kimeta wa Mpui wakati akifika kwenye sherehe



DOWNLOAD FREE WIMBO WA R.O.M.A MKATOLIKI 2030 HAPA

www.kitongoni.blogspot.com 
Habari za mwaka mpya wote natumaini mmekesha salama na nitoe pole kwa wale ambao mkesha huu umekuwa mbaya kwa kuwaletea majeruhi na nitoe pole kwa familia ambazo zimepoteza baadhi ya watu wa familia zao kutokana na mkesha huo wa mwaka mpya. 
Nianze kwa kusema nafurahi kwa kuwajua wasanii baadhi tokea wakiwa na umri mdogo kama wangu kama George Alex maarufu kwa jina la Squeezer akiwa anasoma Highland high School pale Iringa, Mike Mwakatundu maarufu kama Mike T tukiwa tunasoma wote pale Lugalo sekondary School Iringa hapo nikapata nafasi ya kumuona Ambwene Yesaya maarufu kama AY hapo akiwa mwanafunzi wa Ifunda Tech School kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Don Bosco baada ya hapo Disco pale ruaha, R.O.M.A Mkatoliki pale Old Moshi High School nikiwa nimemtangulia.
Nirudi katika mada moja kwa moja kwa jina na heshima waliojijengea ndani na nje ya Tanzania naweza kusema hawaishi maisha ambayo wanapaswa kuishi. Rais Jakaya Kikwete Jana amezindua majibu ya sensa na kusema watanzania tupo milioni 44 sitaki kuamini na siwezi kuamini kuwa mtu kama R.O.M.A hana washabiki milioni 4 ambao wanaweza kununua Albam yake au wimbo wake huu ambao anauza elfu 3. Kwa hii elfu 3 akipata watu milioni 4 hapa nazungumzia 12,000,000,000  kijana wa kitanzania anakuwa katoka na anawaajiri watanzania wengine wengi katika matamasha "show"  zake. 
Leo hii baada ya kutoa wimbo wake wa 2030 ambao kila mtu kaupenda watanzania wengi tulikuwa tukisubiri zile tovuti zetu ziandike DOWNLOAD FREE WIMBO WA R.O.M.A MKATOLIKI 2030 HAPA halafu tuuchukue na kujiburudisha kwa bure na ikifika siku ambayo kuna matamasha tukaingie kwa elfu 7 ambayo sidhani kama katika hiyo elfu 7 anapata hata elfu kwa kila kichwa. Watanzania tumekuwa washabiki wanafiki. Tuna shusha kwenye tovuti nyimbo za wasanii badala ya kununua na kuwaacha wasanii masikini tukisubiri waumwe ili tuwachangie.
Hongera sana R.O.M.A kwa hatua ya kishujaa ya kuamua kujikwamua na mimi napenda niite hatua ya Kininja. Hilo ni jasho lako naomba ulisimamie ipasavyo. Shime watanzania tuwaunge mkono wasanii wetu ili wapate matokeo ya jasho lao.




Monday, December 31, 2012

MATOKEO YA SENSA YA MWAKA 2012

Picture
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi wa matokea ya awali ya sense ya watu na mazi Mjini Dar es Salaam

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ina idadi ya watu Milioni 44,929,002 kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka huu wa 2012.

Matokeo hayo yanaonyesha ongezeko la idadi ya watu Nchini Tanzania lililofikia watu Milioni 33,000,000 ikilinganishwa na lile la sensa ya watu la Milioni 12,313,054 baada ya Uhuru .

Akitangaza matokeo ya awali ya sensa ya idadi ya watu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Dar es salaam Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema matokeo hayo yanaifanya Tanzania bara kuwa na Idadi ya Watu Milioni 43,625,434 wakati Zanzibar ina watu Milioni 1,303,568.

Rais Kikwete alifahamisha kwamba takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inakadiriwa kufikia watu zaidi ya Milioni 51,000,000 ifikapo mwaka 2016 kiwango kisichokidhi mahitaji halisi ya uchumi na mipango mengine.

Dkt. Kikwete alitahadharisha kwamba idadi ya watu imekuwa kwa kiwango kikubwa na ongezeko lijalo linaweza kuwa mzigo mkubwa kwa Taifa ambapo alishauri kuwepo kwa mikakati katika kipindi cha miaka minne ijayo ili kukabiliana na ongezeko hilo.

Alizishauri familia kuzingatia zaidi umuhimu wa suala la kuwa na uzazi wa mpango kwa lengo la kuwawezesha wazazi kuwa na uwezo na mbinu za kuzihudumia familia zao.

Rais Kikwete aliupongeza Umma, Washirika wa Maendeleo pamoja na Viongozi wa nyadhifa tofauti kwa juhudi zao zilizopelekea kufanikisha zoezi ya sense ya watu na makazi na kuviomba vyombo vya habari vilivyotoa mchango mkubwa katika zoezi hilo kuendelea kuelimisha ummamatumizi bora ya Takwimu za sense kwa kudumisha ustawi wa Jamii.

Akimkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa awali wa matokeo ya sense ya watu na makazi Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Taifa ya Sensa ambae pia ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda alisema asilimia 90% ya gharama za zoezi zima la sense limesimamiwa na Serikali yenyewe.

Mh. Pinda alisema Kiwango hicho kimepindukia asilimia 20% ya gharama za sensa ikilinganishwa na Sensa ya mwaka 2002 ambapo zaidi ya asilimia 70% zilitumika katika zoezi hilo.

Akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 mwenyekiti Mwenza wa kamati kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema matokea ya sense yatakuwa na maana katika Taifa pale Taarifa zake zitakapotumika kikamilifu katika kupanga maendeleo ya Nchi.

Balozi Seif aliwaomba washirika mbali mbali zikiwemo Taasisi za Serikali, Sekta binafsi, washirika wa maendeleo na Wananchi kuzifuatilia takwimu za sense kwa kuzitumia katika kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo yao ya kazi.
Alisema hatua hiyo itasaidia kufanikisha malengo ya mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Tanzania (MKUKUTA) na mpango wa kukukuza uchumi na kupunguza umaskini Zanzibar (MKUZA).

Mwenyekiti huyo mwenza wa Kamati Kuu ya Sensa Tanzania Balozi Seif amewashukuru Viongozi wote wa juu, kati, Wananchi pamoja na washirika wa maendeleo kwa kuitikia wito wa serikali zote mbili wa kuwataka washiriki katikamzoezi la sensa ya mwaka 2012.

Naye kwa upande wake mwakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bibi Maryam Khan alisema Taasisi za Umoja huo zitaendelea kusaidia kitaaluma na uwezeshaji katika kuona Mataifa wanachama yanafanikiwa katika utekelezaji wa Mipango yao ya Maendeleo.

Bibi Maryam Khan alisema sensa ndio msingi muhimu inayotoa mwanga wa mipango ya maendeleo kwa kuimarisha miundo mbinu na kuipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kujiletea maendeleo kwa kutambua umuhimu wa kujua idadi ya watu wake.

Mapema Kamishna wa Sensa Tanzania Hajat Amina Mrisho alisema watendaji wa kamati ya sensa watahakikisha machapisho yote ya sensa yatatolewa na kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Hajat Amina ameelezea faraja yake kutokana na watendaji wake kutimiza ahadi ya kutangaza matokeo ya sensa kama ilivyojipanga na inajivunia ufanisi mkubwa iliyoupata katika zoezi zima la sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.

“ Katika kipindi kifupi tumeweza kutoa matokeo ya awali ya sense ambapo inaonyesha umahiri mzuri walionao watendaji wa sense. Uzoefu wa Kitaifa na Kimataifa mara nyingi unaonyesha kuchelewa kwa matokeo ya takwimu za Sensa”. Alifafanua Hajat Amina Mrisho.
Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba leo Desemba 31, 2012 wakati wa kupiga picha baada ya kuzindua matokeo ya sensa ya watun na makazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (PICHA: IKULU)




Sunday, December 30, 2012

HIVI NDIVYO MOTO ULIVYOTEKETEZA MAGHALA YA KUHIFADHIA BIDHAA ZA WAFANYA BIASHARA WA MWANJELWA TAZAMA PICHA ZOTE HAPA,

Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo
Hakika kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo kubeba maji ya kuzimia moto
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo
Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kmuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake
Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto
Kama kawaida kmufa kmufaana hapa vibaka wakigombea sahani na masufuria kwenye box
Hakika jeshi la polisi linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kuokoa mali za wafanyabiashara ambao bidhaa zao zilikuwa katika maghala hayo hapa polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia
Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele
Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo
Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto
Asubuhi hii moto ndiyo unaishia
Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari leo amesema anawapongeza sana wakazi wa Mbeya hasa wale wa maendeo yanayozunguka maghala yalioteketea kwa mtoto kwa ushirikiano wao kuwezesha kuokoa baadhi ya bidha za wafayabiashara licha ya vijana wachache kutaka kuiba na kutupa mawe askari wake ili wafanye uhalifu wa kupora bidhaa zilizokuwa zinaokolewa hapo mpaka sasa vijana wawili wamekamatwa kwa kutupiaaskari mawe na kuiba bidhaa zilizokuwa zinaokolewa
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani 


PROF LIPUMBA: MADAI YA WANANCHI WA MTWARA YASIPUUZWE


Tarehe 27 Desemba maelfu ya wananchi wa Mtwara waliandamana kudai gesi ya Mnazi Bay itumiwe kuendeleza viwanda katika mkoa wa Mtwara kabla ha

ijasafirishwa kwenda kutumiwa maeneo mengine ya nchi. Kwa muda mrefu CUF Chama cha wananchi kimekuwa kikisisitiza kuwa na sera zitakazohakikisha kuwa maliasili na rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote kwa ujumla na hususani wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo maliasili hiyo imegunduliwa.

Katika nchi nyingi utajiri mkubwa wa gesi na mafuta umeleta balaa badala ya kuleta neema. Nchini Nigeria katika delta ya mto Niger ambako ndipo mafuta yanachimbwa kuna ghasia kubwa za kisiasa kwa madai kuwa wananchi wa eneo hilo hawanufaiki na rasilimali yao.

Wananchi wa mikoa ya kusini wana sababu za msingi za kulalamika kuwa  kwa muda wa miaka 51 ya uhuru wa
Tanzania Bara bado hawajatendewa haki. Serikali ya mkoloni wa Kiingereza ilijenga reli kuunganisha Nachingwea na Mtwara ilipoanzisha mradi wa kilimo cha karanga. Mradi huu haukufanukiwa. Badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo na kuendeleza uzalishaji wa mazao mengine kama vile korosho, ufuta, alizeti, kunde na mbaazi, Serikali ya TANU baada ya kupata uhuru ikaamua kun’goa reli ya Nachingwea – Mtwara na kuihamishia Kilosa Mikumi.

Zambia ilipokuwa inakabiliwa na tatizo la kusafirisha mizigo yake isipitie Rhodesia iliyokuwa inatawaliwa na wazungu wachache, walipendekeza kwa serikali ya Tanzania kujenga reli kwenda Mtwara kwani bandari ya Mtwara ni nzuri, ina kina kirefu na haina msongamano. Shaba ya Zambia ingepakuliwa kwa haraka na kusafirishwa kwenda nchi za nje. Vile vile mizigo inayoagizwa kutoka nje ingepakuliwa haraka na kusafirishwa kwenda Zambia. Serikali ya Tanzania haikuafiki pendekezo la Zambia na ikasisitiza reli ya TAZARA iende Dar es Salaam.

Gesi ya Songosongo ilikuwa itumiwe kama malighafi katika kiwanda cha mbolea cha Kilwa Ammonium Company. Prof Cleophace Migiro alienda kusomea PhD ya Chemical engineering kwa maandalizi ya kuja kufanya kazi KILAMCO. Ardhi ya kujenga kiwanda ilinunuliwa Kilwa Masoko, kiwanja cha ndege kikatengenezwa, mpango wa kuimarisha bandari ya masoko ukaandaliwa. Mgogoro wa uchumi wa miaka ya 1980 ikatibua mambo.

Dr. Shija waziri wa Nishati na Madini katika kipindi cha kwanza cha Rais Mkapa alizungumzia umuhimu wa kufufua mradi wa KILAMCO lakini hakuna kilichotendeka. Gesi ilipoanzwa kuchimbwa Songosongo likajengwa bomba dogo la nchi 12 kusafirisha gesi chini ya bahari toka Songosongo hadi Somanga. Bomba la nchi 14  lilijengwa toka Somanga hadi Dar es Salaam.

Uwezo wa mabomba haya ni mdogo ukilinganisha na gesi inayopatikana Songosongo na mahitaji yake kwa shughuli ya kufua umeme na kutumia viwandani. Mkopo wa kujengea bomba la Songosongo hadi Dar es Salaam ulighubikwa na tuhuma za ufisadi za ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha IPTL kinachotumia mafuta mazito ambacho gharama zake za kufua umeme ni za juu sana. Mkataba wa TANESCO na IPTL uliiwajibisha TANESCO kuilipa IPTL dola milioni moja kila mwezi hata kama haijazalisha umeme wowote. Mkataba huu ulidhoofisha sana hali ya fedha ya TANESCO.

Kampuni ya Artumas iligundua kuwepo kwa gas Mnazi Bay, Mtwara na kuanza utaratibu wa kuichimba mwaka 2006 na kuitumia kufua umeme wa Megawati 18. Kabla ya mtikisiko wa sekta ya fedha na uchumi wa dunia wa mwaka 2008, Artumas ilikuwa na mpango wa kuwekeza kwenye mtambo wa kufua umeme Mtwara wa Megawati 300 na kuunganisha Mtwara kwenye gridi ya taifa. Mpango huu ulikubaliwa na serikali na ukaingizwa katika Mpango Kabambe wa Taifa wa kufua na kusambaza umeme (National Power Development Master Plan). Mradi huu wa kufua umeme MW 300 Mtwara ulipangwa uwe umekamilika mwaka huu wa 2012.

Mtikisiko wa uchumi na fedha duniani wa 2008 uliikumba kampuni ya Artumas. Thamani ya hisa za Artumas iliporomoka katika soko la mitaji Canada na Norway. Artumas iliiomba serikali dola milioni 7 kunusuru Mradi wa Nishati wa Mtwara (Mtwara Energy Project). Uwezo wake wa kutekeleza mpango wa kufua umeme Mtwara ukatetereka pamoja na kuwa mradi huo una faida ya muda mrefu. Kampuni ya Artumas Group Inc. iliamua kubadilisha jina lake na kuwa Wentworth Resources Limited.

Wananchi wa Mtwara wanahitaji kujua kwa nini serikali haikutafuta njia mbadala ya kugharamia mpango wa kufua umeme na kuiunganisha Mtwara na gridi ya taifa?

Wentworth Resources wamefanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na kubaini kwamba njia nzuri ya kibiashara na kiuchumi ya kutumia gas wanayoweza kuzalisha Mnazi bay hivi sasa ni kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea na kemikali nyingine Mtwara. Hata hivyo serikali imewamrisha kupeleka gesi watakayozalisha kwenye bomba la gesi la kwenda Dar es Salaam. Gazeti la Financial Time la London la tarehe 6 Desemba 2012 linaeleza

“Bob McBean, executive chairman of Wentworth Resources, which explores in Mnazi Bay, had been planning to use any gas finds together with an existing discovery to power a petrochemical plant to make Africa’s first home-produced fertiliser. “We can supply 80[bcf] right away but we’d have made more money with the plant,” anasema Bw.Mc Bean ambaye kampuni yake imetakiwa kusafirisha  gesi kwenda Dar es Salaam.

Kampuni inayochimba gesi inaamini kuwa kujenga kiwanda cha kutengeneza mbolea Mtwara kitakuwa na faida kubwa kwa kampuni yake. Isitoshe kiwanda hicho kitaongeza ajira kwa vijana wa Mtwara. Kitaanza kuijenga Mtwara kama kituo cha sekta ya gesi na viwanda vyake. Upatikanaji wa mbolea ya bei inayotengenezwa hapa nchini utasaidia kuendeleza kilimo na kuifanya kaulimbiu ya Kilimo Kwanza kutekelezwa kwa vitendo. Hatua ya serikali kuilazimisha Wentworth Resources kuipeleka gas ya Mnazi Bay kwenye bomba la gesi ili isafirishwe Dar es Salaam kunaathiri maendeleo ya Mtwara na Tanzania kwa ujumla.

Ujenzi wa bomba la Mtwara umeanza bila kuwa na mipango ya kuhakikisha kuwa kutakuwepo na gesi ya kutosha kuisafirisha hadi Dar es Salaam. Bomba hili litakuwa na uwezo wa kusafirisha futi za ujazo bilioni 200. Uwezo wa gesi ya Mnazi Bay kwa hivi sasa ni futi za ujazo bilioni 80. Hakuna mpango unaoeleweka wa kupata futi za ujazo bilioni 120 ili bomba la gesi liweze kutumiwa kikamilifu. Mpaka hivi sasa gesi kiasi cha futi za ujazo trilioni 33 imegunduliwa hasa katika bahari yenye kina kirefu. Kuna uwezekano wa kugundua mafuta. Uchimbaji wa gesi hii bado haujaanza. Inaweza kuchukukua miaka 7 – 10 kabla ya shughuli ya uchimbaji wa gesi kukamilika na kuanza kuitumia ndani ya nchi au kuiuza nje ya nchi.

Upatikanaji wa mkopo wa masharti nafuu kutoka China wakujenga bomba la gesi ndiyo umeishawishi serikali kutekeleza mradi  huu haraka bila maandalizi ya uzalishaji wa gesi ya kutosha.Ni vyema serikali ingetekeleza mradi wa kufua umeme Mtwara na kuunganisha Mtwara na gridi ya taifa na kuruhusu kiwanda cha mbolea kuanzishwa Mtwara.

CUF Chama cha wananchi tunaitaka serikali kuzingatia kuwa, kwa kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi uko katika hatua za mwanzo ni vyema serikali ikatathmini upya mantiki na faida za mradi huo. Mradi unaweza kutekelezwa kwa awamu. Awamu ya kwanza iwe kujenga bomba la gesi had Somanga Kilwa ili kuongeza uwezo wa kusafirisha gesi ya Songosongo kuja Dar es Salaam.

Kama nchi bado tuna udhaifu mkubwa wa kuandaa mipango na kusimamia utekelezaji wake. Serikali itufahamishe utekelezaji wa National Power Development Master Plan umefikia wapi? Vipi Mtwara development Corridor bado ipo?

Katika kusimamia sekta ya gesi tujifunze toka nchi ya Norway, Ili kuendesha shughuli za mafuta kwa ufanisi, Norway iliamua mapema kuwa makao makuu ya shughuli za mafuta utakuwa Stavange na siyo mji mkuu wa Oslo. Uamuzi huu umeufanya mji wa Stavange kukua na kuwa kituo cha biashara ya mafuta. Mtwara uwe mji mkuu wa shughuli zote za mafuta na gesi kwa sababu ina bandari asilia yenye kina kirefu na gesi imeanza kugunduliwa kanda ya kusini ya bahari ya Tanzania.

CUF tunasisitiza kwamba, malalamiko ya wananchi wa Mtwara ni ya msingi na wala hayaathiri umoja wa kitaifa. Maoni yao ya kuwa na viwanda vinavyotumia gesi Mtwara na maeneo mengine ya kusini yana mantiki ya kiuchumi. Serikali iwasikilize isiwabeze. Msimamamo wa CUF wa Dira ya Mabadiliko ni kuhakikisha kuwa maliasili na raslimali za nchi zinatumiwa vizuri kuleta neema kwa wananchi wote. Wananchi wa Mtwara wana haki ya kunufaika na neema ya gesi ya Mnazi Bay.

Mwisho Watanzania wote heri ya mwaka mpya – Happy New Year.

Imetolewa na

Mwenyekiti wa CUF-Chama cha wanachi, Taifa
Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba


ALIYETANGAZA KUGOMBEA URAIS 2015 AJIONDOA CHADEMA

   

  Uamuzi huo wa Kisandu umekuja siku chache baada ya kutangaza maandamano kwa nchi nzima kupinga hatua ya Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbrod Slaa, kumiliki kadi mbili ikiwemo ya CCM.


Akizungumza jana na blog hii ya www.kitongoni.blogspot.com Jumapili kwa njia ya simu, Kisandu alisema hatua ya kujiondoa ndani ya CHADEMA imekuja baada ya viongozi wa Taifa wa chama hicho kumuandama kutokana na msimamo wake.
Kwa muda mrefu hasa baada ya kutangaza nami nitagombea nafasi ya urais nimeonekana kuwa ninatumiwa na CCM. Na hata nilipotoa tamko la kuitishwa maandamano kwa nchi nzima ya kutaka Dkt. Slaa, ajiuzulu kutokana na kumiliki kadi ya CCM, imekuwa ni chuki na uhasama baina yangu na viongozi.

Kwa hali hiyo nimetafakari kwa kina na leo hii (jana), ninatangaza rasmi kujivua nafasi zote za uongozi pamoja na unachama wa CHADEMA, huku bado nikibaki na dhamira yangu ya kuendelea kuwa mpigania haki. Nitabaki na msimamo wangu wa kugombea urais mwaka 2015 hata kwa kuwa mgombea binafsi bila kupitia chama chochote. Kwa sasa siwezi kusema nitaelekea chama gani ila baada ya muda ninaweza kusema ninaelekea chama gani ingawa si CCM.

Ninajua wazi sisi watu wa kanda ya ziwa ndani ya CHADEMA tumekuwa tukionekana kama virusi kwani alianza Shibuda, kutangaza nia ya kugombea urais, kila kona alipigwa vita na baadaye Zitto nchi nzima inajua hadi leo hii namna ambavyo anavyosakamwa ndani ya chama. Hata nami nilipotangaza hilo, viongozi wa kitaifa waliweza kuwatumia viongozi wa ngazi za chini katika mkoa huu na kwa muda mrefu sasa kumekuwa na hisia hasi juu yangu na Mkoa wa Tanga kwa ujumla, juu ya ushiriki wangu kwenye shughuli za chama.

Natambua kwamba wapo ambao tayari wameniona mnafiki, mamluki na msaliti kwasababu tu ya kutopenda kutambua ukweli juu ya mwenendo wa chama changu cha CHADEMA

alisema Kisandu.
Akizungumzia ziara za Vugu vugu la Mabadiliko (M4C) zimekuwa za kiupendeleo zaidi, bila kuzingatia maeneo ambayo hayakufikiwa na kampeni za Urais mwaka 2010.

Alisema Mkoa wa Tanga umekuwa ukitengwa sana na kutokuthaminiwa katika ujenzi wa chama, huku chama hicho kikijengwa kwa misingi ya kujitolea lakini kutokana na ubinafsi wa viongozi imekuwa ni kikwazo.

“Ninashindwa kuelewa vigezo vya M4C katika kuchagua viongozi wanaotakiwa kushiriki ziara za vuguvugu la mabadiliko (M4C). Inanishangaza kuona mwanachama aliyejiunga jana CHADEMA akitokea CCM, leo anapewa kipaumbele kuliko viongozi waliojenga chama kwa muda mrefu. Tumejenga chama kwa nguvu ya kujitolea hasa huku mikoani, wilayani na majimboni bila kulipwa chochote, leo hii tunaonekana hatufai hatuna maana,” alisema.



Friday, December 28, 2012

BASI LA ABIRIA USO KWA USO NA LORI LEO

Basi la Abiria limegongana uso kwa uso katika eneo lijulikanalo kwa jina la PIPE LINE INYALA Mbeya baada ya Dereva wa Lori kulipita gari lingine mlimani na ndipo alipokutana na Basi hilo uso kwa uso. Zaidi ya abiria 40 wamenusurika kufa katika ajali hiyo, Dereva wa Lori ambaye ndiye aliyetajwa kuwa na makosa alikimbia kusikojulikana baada ya ajali hiyo na bado anasakwa kwa udi na uvumba.

SAKATA LA ELIMU FEKI: MULUGO YUPO TAYARI KUTHIBITISHA

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema yupo tayari kumthibitishia Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Joseph Mbilinyi, maarufu 'Sugu', juu ya elimu aliyonayo kama alivyodai mbunge huyo. Bw. Mulugo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madai ya Bw. Mbilinyi ambayo ameyatoa katika vyombo vya habari kuwa, Waziri huyo ana elimu ya kuunga unga na jina lake kamili ni Amim. Alisema kauli ya Bw. Mbilinyi haina ukweli wowote bali yeye ni msomi na yupo tayari kuthibitisha ukweli huo kwa umma. “Mimi na Bw. Mbilinyi tuna vilema vingi, akitaka tuumbuane yatabainika mengi hasa katika upande wake, namfahamu muda mrefu kwa sababu nimesoma naye shule moja, nafahamu mambo yake mengi lakini kutokana na hekima zangu sihitaji malumbano na yeye,” alisema Bw. Mulugo. Alidai kumshangaa Bw. Mbilinyi, kuzungumzia jambo ambalo halifahamu lakini kwa kumsaidia ili asielendelee kuonekana mwanasiasa muongo, aitishe mkutano na waandishi wa habari na yeye atakuwa tayari kuthibitisha elimu yake kwa umma. Bw. Mulugo aliongeza kuwa, ni kweli wakati anasoma alikuwa akitumia jina la Amim na baada ya kufika elimu ya juu alianza kutumia jina la Philipo ambalo ni la ukoo ambapo Bw. Mbilinyi kama angekuwa makini, angefuatilia kwenye ukoo wake ili kujua jina hilo linamuhusu au la. Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo hivi sasa linashikiliwa na Bw. Mbilinyi, mwaka 2015 linarudi CCM na ukweli huo utathibitika katika uchaguzi. “Mimi ni Waziri kutoka CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC, hivyo Bw. Mbilinyi, asifikiri kuzua maneno hayo yatanitisha hadi nishindwe kutekeleza sera za chama changu,” alisema. Alisema ibara ya 5 ya Katiba ya CCM, inamwongoza kuhakikisha chama chake kinashinda uchaguzi wa dola wa ngazi zote pamoja na kulirudisha jimbo la Mbeya Mjini kutoka upinzani. “Katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitatumia nguvu zote kuhakikisha jimbo la Mbeya Mjini linarudi CCM, ninachoweza kumshauri Bw. Mbilinyi, ajifunze kutokana na makosa kwani ameanza kunitafuta siku nyingi lakini mimi sikuwa na muda wa kumjibu bali niliendelea kutekeleza majukumu niliyonayo,” alisema. Alisema Mbunge huyo na chama chake walijibiwa na wananchi wa Saza katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Wilaya ya Chunya na kusahau kilichowapeleka ni kampeni hatimaye wakaanza kunadi elimu ya Mulugo badala yake waliambulia kufukuzwa. Aliongeza kuwa, Bw. Mbilinyi alipaswa kulisema na hilo kama walifukuzwa na wananchi wa Saza ambao walimwambia wao, wanamfahamu vizuri Bw. Mulugo na wamemsomesha wenyewe kwa pesa zao baada ya kuthibitika ni yatima. Alisema wananchi hao walidai kuchoshwa na matusi ya Bw. Mbilinyi dhidi yake na kumtungia uongo lakini yeye hana muda wa kulumbana naye bali atamjibu kwa ushahidi. Kauli ya Bw. Mulugo imekuja siku chache baada ya Bw. Mbilinyi kudai kuwa, elimu ya Waziri huyo ni ya kuunga unga kwani alisoma naye Sekondari ya Mbeya Day, wakati huo akiitwa Amim si Philipo Mulugo hivyo kuanzia sasa ataendelea kumuita jina lake halisi na kusisitiza hana uwezo wa kumng'oa jimboni kwake.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU