Young
Africans Sports Club jana usiku imemuongezea mkataba wa miaka miwili
mshambuliaji Hamis Friday Kiiza kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.
Kiiza awali mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa mwezi mei mwaka huu
kabla ya jana kukutana na viongozi wa klabu ya Yanga na kukubaliana
kuongeza mkataba huo.
Kiiza anakua ni mchezaji wa nne wa
kimataifa atayeitumikia klabu ya Yanga akiwa pamoja na Didier Kavumbagu,
Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima.
Ni Majemedari
watatu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC inayohusika pia na masuala
ya usajili, Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb na Wajumbe wake, Isaac Chanji
na Mussa Katabaro wamemaliza kazi hiyo usiku huu.
Zoezi
lilifanya katika eneo la bwawa la kuogelea kwenye hoteli ya Protea, Dar
es Salaam na Kiiza Jumapili atavaa tena jezi ya Yanga kuichezea kwenye
mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.
 |
Hamis Friday Kiiza "mabao" |