Monday, January 14, 2013
POLISI YAKAMATA VIROBA 202 VYA MADAWA YA KULEVYA LEO
TENGA KUTOGOMBEA TENA UONGOZI TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema hatagombea tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema wakati anaingia kwenye uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF kama taasisi kwa kuweka mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba na kanuni, jambo ambalo limefanyika.
“Wajumbe wamekuwa wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana. Nilishafika pale pa kufika. Tulipoanza wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo tumeifanya. Tulipoingia mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema Rais Tenga.
Amesema walitengeneza Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa wapiga kura ambapo hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea migogoro, hata ikitokea kuna mfumo wa kuidhibiti.
Rais Tenga ameishukuru Sekretarieti ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kamati za uchaguzi za wanachama wa TFF na vyama wanachama wa TFF kwa hatua iliyofikiwa katika uchaguzi ambapo mikoa yote imekamilisha uchaguzi na kubaki vyama shiriki pekee.
Ametoa mwito kwa wadau kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga taasisi ajenda iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini kifanyika ili mpira uchezwe katika maeneo mbalimbali.
“Tumeshatengeza mfumo, sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira. Changamoto ni tufanye nini ili mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo ajenda ili tuangalie tunakwendaje mbele,” amesema.
Pia amesema ushirikiano ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni wa ajabu. Vilevile ameishukuru vyombo vya habari, Serikali, klabu, wadhamini na wafadhili kwa mchango wao katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.
ANGALIA PICHA ZA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA IFM LEO
Ulinzi ukiwa umeimarishwa wizarani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha |
Hapa wanafunzi wakiwa safarini kwenda kumuona kamanda kova |
Kamanda Kova akimsikiliza Rais wa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) akimuelezea kadhia nzima. Baadae Kamanda Kova aliamuru wanafunzi hao waende wote Kigamboni kushughulikia kadhia hiyo |
Kamanda Kova akitoa taarifa kwa waandishi wa habari |
Hapa wanafunzi wakiimba "tunavuka bure , tunavuka bure" huku wakielekea kwenye kivuko |
Hapa wanafunzi wakigoma kushuka kwenye kivuko ilichukua saa zima ndio wakashuka na kuruhusu kivuko kiendelee na shughuli zake kama kawaida |
Wakati wengine wakikataa kushuka wengine walikuwa wakiongezeka |
WABABA WA BSS (2012) AKABILIWA NA KESI YA KUTEMBEA NA MWANAFUNZI
Mapenzi yao yalianza tangu binti akiwa kidaato cha tatu
lakini halikuwa penzi lenye mashamu shamu kwa kuwa wabababa alikuwa bado
hajamiliki pesa na heshima katika jamii inayomzunguka kama sasa mara tuu baada
ya kuchukua kifuta jasho cha bss na vijihela alivyopewa na mapapaa waliokubali
kazi aliioifanya bss hivyo kuwa na kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunz
ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na
mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo. Wababa aliwekwa ndani
kwa muda wa siku mbili na kesi bado ipo mahakamani na wazazi wa binti wameapa
kumweka ndani wababa na kumfanya kama Babu Sea huku binti akiwa hajaonekana
siku ya 4 sasa na kutokujulikana alipo kwa madai anampenda wababa na wakimfunga
tu nae anakunywa sumu.
Subscribe to:
Posts (Atom)