Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa |
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo |
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo |
Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kmuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake |
Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto |
Kama kawaida kmufa kmufaana hapa vibaka wakigombea sahani na masufuria kwenye box |
Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele |
Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo |
Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto |
Asubuhi hii moto ndiyo unaishia |
Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia |
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo |
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani |
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog