Chama tawala nchini Uganda cha National Resisitance Movement-NRM-
kimewafukuza baadhi ya wanachama wake wanne, wote wakiwa ni wabunge, kwa
kile kilichoitwa utovu wa nidhamu.
Mbunge mwingine yeye amesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu kwa sababu za ulevi.
Katibu
mkuu wa chama hicho Amama Mbabazi anasema hii kwa tafsiri yake
inamaanisha kuwa wabunge hao wamepoteza viti vyao, jambo ambalo wahusika
wanapinga.
Katibu
mkuu wa chama tawala cha NRM na wakati huo waziri Mkuu wa Uganda, Amama
Mbabazi, ametangaza maamuuzi ya kamati kuu ya chama hicho kuhusu
majaliwa ya wabunge wanne waliopewa jina la ‘wabunge waasi’ kutokana na
misimamo yao dhidi ya masuala mbalimbali katika chama hicho.
Mbabazi
alitoa kauli hiyo na kusema, “Muhammad Nsereko afukuzwe kutoka NRM;kuwa
Theodor Sekikubo afukuzwe kutoka NRM; kuwa Barnabas Tinkasimire
afukuzwe kutoka NRM; kuwa Wilfred Nuwagaba wamefukuzwe kutoka NRM; na
kuwa Vicent Kyamadidi Muzuni asimamishwe uana chama wa NRM kwa muda wa
miezi mitatu.”
Wabunge
wanne waliofukuzwa kutoka chama: Nsereko; Sekikubo; Tinkasimire pamoja
na Niwagaba wamekuwa wakipinga na kukosoa saana uongozi wa sasa wa chama
hususan kutokana na madai ya ufisadi dhidi ya vigogo wa chama.
Na
wanasema hatua hii ni ya kuwaandama kisiasa kwa kusema ukweli dhidi ya
wanachoita uongozi mbaya. Hatua ya kuwafukuza wanachama hao , inasekena
ni kutokana na utovu wa nidhamu.
Wabunge hao walishtakiwa katika
kamati ya nidhamu ya chama na kukabiliwa mashataka saba: kuwapigia debe
wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mdogo; kupaka matope
wagombea rasmi wa chama cha NRM wakati wa uchaguzi mdogo; kutoa madai ya
uongo kwa vombo vya habari dhidi ya chama cha NRM; kutumia majukwaa
haramu, kama vile vyombo vya habari na mikutano ya hadhara ya vyama vya
upinzani kuzungumzia masuala yanayowakera;kujihusisha katika uundaji wa
genge ndani mwa NRM; matumizi ya lugha chafu;na mwisho kukaidi kamati ya
nidhamu ya chama.Wote licha ya kuwaita kufika mbele ya kamati hiyo
kujieleza walipinga.
Hii ndiyo mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi kuanza tena mwaka wa 2006, chama cha NRM kufukuza wanachama wake.
Na
hii imezusha tafsiri tofauti kwa wabunge wanaofukuzwa chama.Katibu mkuu
wa NRM anasema kuwa hii inamaanisha kuwa wamepoteza viti vyao vya
ubunge.
Mbabazi
aliongeza kusema kuwa ''Kulingana na sheria za Uganda, hususan kifungu
83 cha katiba ya taifa ni kuwa mtu anaweza kuwa mbunge pindi tu ikiwa
amechaguliwa kama mbunge wa kujitegemea,au ikiwa amechaguliwa baada ya
kuungwa mkono na chama Fulani,au ni waziri,au kama mwanajeshi.''
Hakuna
njia nyingje ile. Wabunge hao wanasema kuwa katiba haikubali mbunge
yeyote kubadili chama bungeni.Ikiwa mtu atapoteza uungwaji mkono wa
chama chake hii ina maana kuwa amepoteza kiti chake.
Lakini hilo limepingwa na mbunge muathiriwa na tena wakili, Wilfred Niwagaba.
Niwagaba
alisema ''Ikiwa anadhani kwa kutusimamisha au kutufukuza uanachama ina
maana kuwa tunapoteza viti vyetu,nasikitika sikubaliani na tafsiri
hiyo.Hakuna hata mmoja wetu ameondoka kutoka chama kwa hiari.''Hata
hivyo mwenzao Vincent Kyamadidi amesimamishwa uanachama kwa muda
kutokana na madai kuwa alilewa na kujaribu kupigana hadharani jambo
ambalo linakwenda kinyume na maadili ya chama.
Aidha yeye alipoita kujieleza alifika mbele ya kamati hiyo.
Bado kuna vuta ni kuvute kuhusu majaliwa ya wabunge wanne, ikisemekana wamekwenda mahakani kupinga kufukuzwa kwao.