Sunday, June 29, 2014
TUKIO LILILOMSABABISHIA LUIS SHUAREZ AFUNGIWE MICHEZO TISA NA FAINI HILI HAPA
BRAZIL YAFANIKIWA KUINGIA ROBO FAINALI KWA KUITOA TIMU NGUMU YA CHILE HUKU COLOMBIA NAYO IKIIFUNGISHA VIRAGO URUGWAI.
Kikosi cha Brazil kimefanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali baada ya kuiondoa timu ngumu ya Chile kwa mikwaju ya penati 3-2. awali timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na hata zilipoongezwa dakika 30 bado mchezo huo ulikuwa na matokeo hayo hayo ndipo wakaingia kwenye mikwaju ya penati na ndipo Brazil wakaibuka kidedea.
Wachezaji wa Brazil kama wanavyoonekana wakishangilia ushindi wao baada ya kuitoa timu ngumu ya Chile kwa mikwaju ya penati 3-2.
David Luiz akishangila nyuma ya wachezaji wa Chile wakati wao wakiwa wameshika viuno hawaamini yaliyotokea.
Alexis Sanchez akiwa na maumivu ya kukosa penat kama anavyoonekana amejilaza chini.
Gonzalo Jara akitazama Penati yakeinavyokwenda kugonga mwamba na kutoka nje na ndiyo penati iliyowatoa Chile kwenye mashindano
Paulinho akiwapa wenzake mbinu za kupata ushindi kwenye mikwaju ya penati.
Colombia nayo imeifungasha virago Urugway kwa kichapo cha 2-0 na kutinga robo fainali.
Rodriguez akiunganisha mpira ambao aliutuliza kifuani kabla ya kuachia fataki na kuandika bao la kwanza kwa nchi yake ya Colombia.
Diego Godin na wenzake wa Urugway wakijaribu kumziwia muuwaji wao jana katika mechi kati ya Colombia na Urugway Rodriguez's.
Fernando Muslera akishindwa kabisa kuuziwia mpira ambao ulikuwa unaingia nyavuni na kuiandikia Colombia bao la kwanza kama unavyo jionea hapo pichani.
Rodriguez akiipatia Colombia bao la pili
Colombia nayo imeifungasha virago Urugway kwa kichapo cha 2-0 na kutinga robo fainali.
Chanzo:Daily Mail
Subscribe to:
Posts (Atom)