Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Symbion, Ndugu. Peter Gathercole akifafanua jambo, leo
Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na Uongozi wa Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuelezea mikakati ya Maandalizi
ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya mchezo wa soka nchini (Soccer
Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts).
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Ndugu. Leonard Thadeo (kushoto) akielezea jambo, leo
Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, wakati uongozi wa Wizara
ulipokutana na Ujumbe wa Viongozi wa kampuni ya Symbion ya Marekani
Kujadili Maandalizi ya Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Mchezo wa soka nchini
(Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia
kwake ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Henry
Lihaya na Afisa Michezo Mkuu, Charles Yasse Mattoke.