Facebook Comments Box

Tuesday, November 6, 2012

MUUWAJI WA KAMANDA BAROW ALIHUDHURIA MAZISHI YAKE

POLISI mjini Mwanza imebaini kuwa mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, alikwenda kuaga mwili wa Kamanda huyo katika uwanja wa Nyamagana sambamba na wananchi wengine. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Lily Matola jana alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Abdallah Petro ‘Ndayi’ (32) mkazi wa Mjimwema mjini hapa ambaye anashikiliwa Polisi. Kwa mujibu wa Kamanda Matola, Petro mbali na kutajwa kuhusika na mauaji hayo, pia anadaiwa kuwa na rekodi ya kufungwa miaka 30 jela katika gereza la Butimba kwa unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka 2006. Alitoka gerezani mwaka 2010 baada ya kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania. Petro pia imebainika pia kuwa ni mdogo wa mtuhumiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Muganyizi Peter. Vielelezo vyakamatwa Kamanda Matola alisema mbali na kuwa na uhusiano huo, Petro na mtuhumiwa mwingine, Abdurahim Ismail Athuman ‘Dula’ (28) mkazi wa Mkudi Ghana, pia mjini hapa, baada ya kukamatwa kwa nyakati tofauti Mjimwema na Kilimahewa mwishoni mwa wiki, waliwapeleka polisi mahali walikoficha baadhi ya mali za marehemu. Mali wanazodaiwa kuonesha polisi ni pamoja na redio ya mawasiliano ya Polisi na funguo za gari alilotumia kamanda Barlow siku ya tukio la mauaji yake. Kamanda Matola alisema watuhumiwa waliwapeleka polisi katika shimo la majitaka kwenye maeneo ya Nyanshana, jijini Mwanza walipokuwa wameficha vitu hivyo. Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Joseph Konyo alisema watuhumiwa baada ya kutimiza uhalifu, walitenganisha redio hiyo ya mawasiliano ili isipatikane. “Damu ya mtu haipotei bure, hayo yote ni pamoja na Mungu mwenyewe, kwani sisi peke yetu hatuwezi, wananchi mmetusaidia sana,” alisema Kamanda Konyo. Baada ya kuonesha polisi vitu hivyo ambavyo sasa vimechukuliwa kama vielelezo katika kesi ya mauaji ya Barlow, Kamanda Matola alisema watuhumiwa hao walipekuliwa na kukutwa pia na kadi tatu za simu za Vodacom na Airtel, simu ya mkononi, viatu vya ngozi na begi dogo. Pia walikutwa na kofia mbili za kijeshi aina ya bereti; moja ikiwa ya Polisi na nyingine ya kampuni ya binafsi ya ulinzi, sare za kampuni ya ulinzi, mtarimbo, bisibisi, mapanga, televisheni mbili, sub-hoofer na deki. Alisema walipohojiwa, walidai wamekuwa wakihifadhiwa na Ryoba Matiku ‘Mama Nyangi’ katika eneo la Nyakabungo Miembeni ambako mipango yote ya uhalifu imekuwa ikisukwa. Mama huyo anashikiliwa pia kwa mahojiano.

HATIMAYE SERIKALI YASEMA TPI WALITENGENEZA ARV FEKI

LICHA ya wamiliki wa kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) kukana kutengeneza na kusambaza dawa bandia za kupunguza makali ya UKIMWI, serikali imethibitisha kuwa kiwanda hicho ndicho kilitengeneza dawa hizo aina ya TT-VIR 30 yenye toleo Na OC.01.85. Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akisema kuwa serikali itawachukuliwa hatua za kisheria wote waliohusika katika suala hilo. Alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa suala hilo hatari linapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuzuia lisitokee tena, kabla ya kuchukua hatua hizo za kisheria uchunguzi unafanywa kupitia vyombo vya usalama. Dk. Rashid alikiri kuingia katika mzunguko kwa dawa hizo bandia lakini akawatoa hofu wagonjwa wote wanaotumia (ARV’s) kuwa dawa zinazopatikana kwenye vituo vya kutolea huduma hiyo kwa sasa ni salama na zenye viwango vinavyotakiwa. “Tunatoa wito kwamba waendelee kutumia dawa hizo kama wanavyoshauriwa na madaktari… kupitia Wizara ya Afya, serikali imehakikisha uwepo wa dawa za kutosha na kupunguza makali ya ukimwi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya,” alisema. Dk. Rashid alifafanua kuwa Wizara ya Afya hununua dawa hizo kupitia Bohari ya Dawa (MSD), ambayo imepewa jukumu la kununua, kuzitunza na kusambaza katika vituo vya kutolea huduma za afya. Alisema kwa hapa nchini kuna kiwanda kimoja tu cha TPI kinachotengeneza dawa hizo na kwamba zile za bandia zilibainika mwanzoni mwa Agosti mwaka huu katika ukaguzi wa kawaida wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika Hospitali ya Tarime. Alisema baada ya ukaguzi na uchunguzi kwenye vituo vyote vya huduma za afya katika mkoa wa Mara na nchi nzima ilibainika kuwa dawa yenye jina la biashara TT-VIR 30 toleo namba 0C.01.85 ni bandia. Alisema pia ilibainika kuwa nyaraka zilizokutwa katika Bohari ya Dawa (MSD) zinaonyesha kuwa TPI iliiuzia MSD dawa hiyo bandia toleo namba 0C.01.85. Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa uchunguzi ulibaini kuwa dawa hiyo bandia ilikuwa na dawa zenye rangi tatu tofauti, njano, nyeupe na vidonge vya rangi mbili tofauti za pinki na nyeupe. Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo wa Afya, dawa zilizokuwa na rangi ya njano, zilikuwa na kiambata cha Efaverenz badala ya viambata aina ya Nevirapine, Lamivudine na Stavudine vinavyopaswa kuwemo. Aidha vidonge vyenye rangi nyeupe na vile vyenye rangi ya pinki na nyeupe vilikuwa na viambata vinavyotakiwa kuwepo yaani Nevirapine, Lamivudine na Stavudine kama ilivyokuwa kwenye lebo. Akielezea kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya matokeo hayo ya uchunguzi alisema ni pamoja na kusimamisha mara moja matumizi ya dawa hizo aina ya TT-VIR 30 toleo Na 0C.01.85. Hatua nyingine ni pamoja na kusitisha uzalishaji wa dawa zote katika kiwanda cha TPI Ltd hadi uchunguzi wa suala hilo utakapokamilika ikiwa ni pamoja na kujiridhisha tena ubora wa dawa inazozalisha. Alisema pia vigogo wa MSD akiwamo mkurugenzi wake walisimamishwa na kwamba wizara imeunda timu ya wataalamu kwa lengo la kufuatilia mwendelezo wa tiba na matunzo kwa wagonjwa wa UKIMWI.

Sunday, November 4, 2012

YANGA NA AZAM KATIKA PICHA

Kiiza akijaribu bila mafanikio kufunga

Aggrey Morris akiruka juu ya Paul Ngalema kupiga mpira kichwa

Mbuyu Twite akimuacha chini Salum Abubakar

Kiiza akimtoka Hajjji Nuhu

Haruna Niyonzima 

Chuji akijadiliana na Niyonzima kabla ya kupigwa kwa mpira wa adhabu

Kiiza alivyomuenzi Mafisango

Mwadini akidaka mpira hewani 

Simon Msuva anateleza

Mwadini akiruka kupangua mpira

Msuva

Hatari kwenye lango la Yanga

Jabir Aziz akimdhibiti Chuji

Kiiza anapasua katikati ya Ibrahim Shikanda kulia na Sure Boy kushoto 

Nadir Haroub 'Cannavaro' akimdhibiti John Bocco

Hatari kwenye lango la Yanga

Stewart Hall alitia huruma

Frank Domayo kulia akipambana na Aggrey Morris

Niyonzima akipiga shuti mbele ya Shikanda

Twite anapasua

Sure Boy akimtoka Twite

Sure Boy na Twite

Chuji akipiga kisu mbele ya Sure Boy

Msuva anatafuta njia

Shughuli

Yanga wakipiga ndiki kabla ya mechi

Kikosi cha Azam leo

Kiiza anamtoka Erasto Nyoni

Kikosi cha Yanga leo

Hatari kwenye lango la Azam

Hatari kwenye lango la Yanga

Msuva akiwasalimia wenzake benchi baada ya kupumzishwa

Niyonzima kushoto, Nyoni kulia

Kiiza na Hajji Nuhu


Kiiza baada ya kufunga bao la pili


Kavumbangu wa pili kutoka kushoto, akishangilia bao lake na wenzake

Kavumbangu wa kwanza kushoto


LIVE SCORE : FT YANGA 2 - 0 AZAM, MTIBWA 2 - 0 SIMBA


Kutoka Taifa: Mpira umeisha Yanga wanatoka kifua mbele kwa Goli kwa sifuri

Kutoka Morogoro:  Mpira umeisha Mtibwa Inatoka kifua mbele kwa 2 kwa sifuri

Kutoka Morogoro: Gooooool Mtibwa wanapata goli la pili hapa. Nilisema huyu Javu ana historia ya kufunga katika uwanja huu. Ndio maana mara zote tunaandika mtibwa wanaongoza kwa goli la kwanza na hili ni la pili

Kutoka Mtibwa: Dk 88 Mtibwa bado wapo mbele kwa goli la kwanza

Kutoka Morogoro: Mwinyi kazimoto anaachia shuti kali linapanguliwa na kipa na kuwa kona. Simba wanalisakama lango la mtibwa

Kutoka Morogoro: Husein Javu anaingia kuchukua nafasi ya Muhamed Mkopi. Huyu Javu ana historia nzuri ya kufunga katika uwanja huu

Kutoka Morogoro: Dk 79 Okwi anawakosakosa mtibwa na inakuwa kona. Husein Sharrif anapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda. askari wameongezwa uwanjani

 Kutoka Taifa: Gooooooool Yanga wanaongeza goli la pili. Ni Hamis Kiiza "diego" anafunga goli safi sana hapa. Alivua jezi hapa kiiza anapewa kadi ya njano

Kutoka Taifa: Abdi Kassim anachukua nafasi ya Hamis Mcha.

Kutoka Taifa: Msuva anaenda nje anaingia Luhende.Yanga wanakosa goli baada ya Kavumbagu kuchelewa krosi ya Niyonzima

Kutoka Taifa: Dk 51 Erasto Nyoni anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumkanyaga Niyonzima wa Yanga.

Kutoka Taifa: Dk 48 Bocco anashindwa kuuwahi mpira aliopigiwa na Khamis Mcha lakini Chuji anautoa na kuwa kona. Azam inapata kona ambayo inakolewa na mabeki wa Yanga.

Kutoka Taifa: Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa kati ya Yanga na Azam

Kutoka Morogoro: Babu Ally anapewa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi emanuel Okwi. Na Mrisho Ngassa anaingia kuchukua nafasi ya Akuffor. Chollo anaingia nafasi ya Ochieng

Kutoka Morogoro: Mpira umeanza Jamal anatoka na anaingia Issa


Kutoka Morogoro: Washabiki wa Simba wamtupia chupa mwamuzi wa pambano hili, vile vile wamewarushia vilevile chupa wachezaji wao. mmoja wa washabiki hao wa simba amekamatwa na polisi. Ulinzi zaidi unahitajika katika mechi hii maana inaonekana washabiki wa simba hawana uvumilivu.

Taifa; Dk 45 HALF TIME..... AZAM 0-1 YANGA

 Kutoka Morogoro: Mtibwa wanapata kona tatu mfululizo, lakini, Kaseja anadaka, dakika ya 42 sasa

 Taifa: Dk 39 Yanga na Azam zinashambuliana kwa zamu na mpira unachezwa katikati sana.

Kutoka Morogoro: Mtibwa inaongoza kwa bao moja dhidi ya Simba, mfungaji Mohamed Mkopi. MTBWA 1-0 SIMBA


Taifa:  Dk 32 Azam inapata kona baada ya Mbuyu Twite kuutoa mpira nje
Khamis Mcha anapiga kona lakini Bocco anautoa mpira nje.
Dakika ya 28, Akuffor, anashindwa kutumia makosa ya mlinzi wa Mtibwa ambaye alipiga pasi fupi kwa mwenzake na kuiwahi. Lakini, akiwa ndani ya sita anashindwa kuamua kufunga au kutoa pasi, na kupiga pasi mkaa iliyonaswa na mlinzi wa Mtibwa. Dakika ya 30 sasa.
Kutoka Taifa: Dk 28 Bocco anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini kipa Ally Mustapha anadaka
 Dk 26 Athuman Idd Chuji anamchezea faulo Michael Bolou.
Kutoka Morogoro: Kwa dakika 20 za mwanzo, mechi bado imebalansi hakuna mashambulizi ya maana sana ambayo timu zinayaandaa. Kila timu inacheza kama haitafuti ushindi. Mara mbili, mshambuliaji, Said Mkopi wa Mtibwa amejaribu kumtoka Amir Maftah, lakini hakufanya cha maana. Emmanuel Okwi anajitahidi kuwakimbiza mabeki wa Mtibwa Sugar, lakini bado hapati, sapoti ya karibu kutoka Sunzu na Akuffor. Mtibwa, wamepiga kona nne hadi sasa, wakati,Simba, wamepata kona moja tu. Kiujumla, mchezo bado umepooza hadi sasa.
 
 Kutoka taifa: Dk 18 Niyonzima wa Yanga,anakosa bao la wazi kwa kupiga nje mpira aliopokea kutoka kwa Oscar Joshua.
Dk 15 Erasto Nyoni wa Azam anamchezea rafu Msuva 
Dk 14 Simon Msuva wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya kushindwa kuuwahi mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Dk 13 Mpira unachezwa kwa kasi sana na timu zote zinatawala kiungo
 
 Kutoka Morogoro - Kwa dakika hizi kumi za mwanzo, timu zote zinaonekana kucheza kwa kuogopana zaidi. Mtibwa, walianza kufika katika lango la Simba, kupitia kwa Shaaban Nditti. Walinzi wa Simba, Keita na Ochieng, wakamthibiti. Bado hakuna soka la kuvutia na la mipango, japo, Mtibwa, wanaonekana kucheza kitimu hadi sasa. Simba, wanapata kona ya kwanza, lakini haina madhara, dakika ya 12 
Dk 9 GOOO...... Didier Kavumbagu anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Azam. AZAM 0-1 YANGA
Kutoka taifa: DK 3 Hamis Kiiza anakosa bao la wazi kwa upande wa Yanga.
 Kutoka taifa: Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya
Azam Fc Vs Young Africans
Morogoro - Mpira umeanza hapa Morogoro - Simba wakianza kwa kasi.
Leo tunaendeza utamaduni wetu wa kuwaletea matukio muhimu yanayoendelea kwenye viwanja tofauti vya ligi kuu ya Tanzania bara - kwa siku ya leo tunawaletea matukio ya mechi mbili kubwa kati ya Azam na Yanga, na Simba dhidi ya Mtibwa.
Kutoka Morogoro - Hiki ndio kikosi cha kwanza cha Simba kinachoanza: Kaseja, Kapombe, Maftah, Keita, Ochieng, Mkude, Kiemba, Kazimoto, Sunzu, Okwi, Akuffor
Hiki ndio kikosi cha Yanga ambacho tumefanikiwa kukipata. 
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Yaw Berko
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Nizar Khalfani
6.Jeryson Tegete
7.Said Bahanunzi


MAALIM SEIF AZUNGUMZA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameelezea kuchukizwa kwake na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani vilivyotokea hivi karibuni visiwani Zanzibar.

Amesema vitendo hivyo vimeigharimu Zanzibar katika Nyanja mbali mbali zikiwemo za kiuchumi, kisiasa na kijamii, sambamba na kuitia doa katika jamii ya kimataifa.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho katika viwanja vya demokrasia Kibandamaiti mjini Zanzibar, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amevilaumu vyombo vya dola kwa kutochukuwa hatua zinazostahiki katika kudhibiti vitendo hivyo.

Amesema hatua zilizochukuliwa katika kurejesha amani baada ya kutokea kwa vurugu hizo hazikuwa muafaka, kwani zimekuwa zikiwadhalilisha na kuwanyanyasa wananchi wasiokuwa na hatia pamoja na kuhujumu mali zao.

Amesema yeye binafsi amechukizwa na kitendo cha kuuliwa kwa askari polisi katika eneo la Bububu, Koplo Said Abrahmani lakini bado serikali na vyombo vya dola vina jukumu la kulinda haki za raia kwa kuwasaka wanaohusika na tukio hilo, na sio kuwanyanyasa raia wasiokuwa na hatia.

“Nazungumza haya kwa unyonge sana leo, sikufikiria kuwa vitendo hivi vingetokea Zanzibar katika wakati huu tunaotekeleza maridhiano ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa”, alieleza Maalim Seif na kuongeza: “Sipendi kuisema serikali yangu na Rais wangu hadharani, lakini inanibidi niseme ‘Rais wangu Dkt Shein unatuangusha’ kwa kuwa wewe ndiye mwenye jukumu kubwa zaidi la kulinda amani ya nchi hii” alieleza.

Ametahadharisha kuwa huenda vitendo hivyo vimepangwa kuvuruga umoja wa Wazanzibari ambao umeiletea sifa kubwa Zanzibar, na kuwataka wananchi kutokubali kuingizwa katika mtego utakaopelekea kuvunjika kwa umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa wananchi.

Katibu Mkuu huyo wa CUF alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa vikundi vinavyolalamikiwa kufanya vurugu vikiwemo vya ‘Ubaya ubaya, Mbwa mwitu na Janjawid vilikuwepo kabla ya tukio hilo na kwamba vimetokana na kundi kubwa la vijana la JANJAWID lililoahidiwa kupewa ajira na Serikali.

Katika hatua nyengine Maalim Seif ameitaka Tume ya mabadiliko ya katiba kufanya kazi kwa uadilifu na kuheshimu mawazo ya wananchi wanayoyatoa bila ya kuonyesha upendeleo kwa baadhi ya watu au makundi fulani.

“Tume hii inaonekana kuanza kuwa na ‘bias’ kwa baadhi ya watu na makundi fulani, lakini tunamwambia Jaji Warioba tume yake iheshimu mawazo ya wananchi”, alitanabahisha.

Katika risala ya wanachama wa chama hicho kwa wilaya sita za Unguja iliyosomwa na Katibu Mtendaji wa vijana CUF taifa Khalifa Abdallah walitahadharisha juu ya uwezekano wa kuwepo kwa ajenda ya siri ya kuvuruga Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa bado inahitajika katika kupata ukombozi wa kweli wa Zanzibar, sambamba na kuendeleza umoja na mshikamano wa Wazanzibari.

Naye Kaimu wa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bw. Salim Bimani amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao juu ya mabadiliko ya katiba, na kuiomba Tume inayohusika na ukusanyaji wa maoni kuwapa fursa wananchi kutoa maoni yao kwa uwazi.

“Wananchi msikubali kuchokozeka, nendeni mkatoe maoni kwani hii ni fursa pekee ya kupata katiba tuitakayo” alisisitiza Bimani.




SHABAN KADO APATA AJALI

 Mchezaji wa simba Uhuru Selemani aandika katika wall yake ya Facebook kuwa mchezaji wa Mtibwa Sugar Golikipa Shaaban Kado amepata ajali Chalinze. Hii labda ndio inayofanya leo asiwepo uwanjani. Blog hii inafuatilia na habari kamili itakupa baada ya muda.
Ndugu zangu mliopo chalinze naomba mfatilie hapo hospitali kado kapata ajari nasim yake haipatikan pls naomba mfatilie atakae kuwa nataarifa aniinbox namba yake sory jaman


LORD EYES APATA DHAMANA

.
Stori za uhakika nilizozipata muda mfupi uliopita ni kwamba mkali wa Hiphop kutoka A Town ambae alikua anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz, Isack Waziri (Lord Eyes) hivi sasa yuko nje kwa dhamana.
Ametoka nje kwa dhamana toka ijumaa ya novemba 2 2012.
Oktoba 23 2012 Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alikaririwa na millardayo.com akisema “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia  kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”
.


Friday, November 2, 2012

TRENI YA DAR



ALI KIBA, DOGO ASLAY NA SAIDA KAROLI KUWANIA TUZO ZA HESHIMA ZA KORA 2012.



Baada ya miaka kadhaa kufanyika kwa tuzo za kora nchini South Africa,Nigeria na kisha Bukinafaso na hatimaye kusimama kwa muda kutokana na Post election Crisis iliy
otokea Ivory Coast, sasa tuzo hizi zimerudi tena na zitafanyika December 29 mwaka huu nchini Ivory coast.

ALI KIBA ametajwa kuwania kwenye kipengele cha 'Best male east afrika' kwa wimbo wa 'Single boy' aliomshirikisha Lady JayDee. Ali kiba atachuana na Jimmie gait ft Dk furi furi dance{Kenya}, Kidum ft sana mulika mwizi{Burundi}, Redsan-Ila wewe{Kenya},Chris D-Aisha{Burundi} na Malatu astatike{Ethiopia}.

DOGO ASLAY ametajwa kwenye kipengele cha 'Best male newcomer' na wimbo wa 'Niwe nawe' akipambana na Floby saanida{Burkina faso},Loyiso-Wrongo to u,Frique du sud, Aziz Azion-My oxyen{Uganda}, Davido Dami duro{Nigeria},John chit wapusuku{Zambia}.

SAIDA KAROLI anawania kipengele cha 'Best female East africa' kwa wimbo wa 'Sakina' ambapo anachuana na Juliana kanyomozi-Am gud ugandan,Marya shiki-Simu{Kenya},Helen berhelebe{Ethiopia},Asther aweke lu milli{Ethiopia} na Ikraam caraale gaarsiiya{Somalia}.



Monday, October 29, 2012

DR SLAA ACHEMKA TABORA

Habari ifuatayo imetumwa na Abunuwasi Alinacha (email: a...a...@gmail.com):
---

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya.

Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.

Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi.  Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka  kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi  alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote.  Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda



TFDA INAFAA KUSHITAKIWA

 
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imewekwa matatani ikielezwa kuwa nayo inastahiki kuchukuliwa hatua kutokana na kuzembea katika ukaguzi wa dawa na hivyo kusababisha dawa bandia za kupunguza makali ya ukimwi (ARV’s) kusambazwa.

Sakata hilo linakuja wiki chache tangu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Joseph Mgaya, na viongozi wengine kupisha uchunguzi wa tuhuma za kusambaza dawa hizo.

Wengine waliosimamishwa kazi ni mkuu wa kitengo cha udhibiti ubora na ofisa uthibiti ubora huku kiwanda cha dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kikisitishiwa uzalishaji na usambazaji wa dawa zilizokwishatengenezwa.

Taarifa za ndani ya TFDA ambazo Tanzania Daima imedokezwa na mmoja wa maofisa wake ambaye aliomba kuhifadhiwa jina kwa vile si msemaji, zilisema kuwa mamlaka hiyo nayo ilizembea katika sakata zima la dawa bandia za ARV’s kusambazwa.

Kiwanda chochote kabla ya kuzalisha dawa au chakula ni lazima kipate kibali cha TFDA baada ya kukaguliwa na kukidhi viwango husika.

“Hata dawa ingekuwa inaingizwa kutoka nje ya nchi, vilevile TFDA inapaswa kukikagua kiwanda husika kuona kama kina ubora wa kutengeneza dawa na kukidhi viwango,” kilisema chanzo chetu.

Gazeti hili pia limefanikiwa kupata nakala ya waraka wa TFDA kuhusu hali ya viwanda vya dawa nchini, ambayo inabainisha kuwa Tanzania ina viwanda saba vya dawa vilivyosajiliwa katika mwaka 2011/2012.

Viwanda hivyo ni Shelys Pharmaceuticals Ltd, Zenufa Laboratories Ltd, Mansoor Daya Chemicals Ltd, Keko Pharmaceuticals (1997) Ltd, Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd, A.A. Pharmaceuticals Ltd na Tanzansino United Pharmaceuticals (T) Ltd.

Waraka huo unabainisha kuwa kiwanda cha Tanzansino United Pharmaceuticals (T) Ltd, ambacho serikali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa ni mmbia mmojawapo kimesimamisha utengenezaji dawa tangu Agosti 2010 kutokana na mwekezaji wa nje kujiondoa.

“Ukaguzi uliofanywa na TFDA katika miaka ya fedha ya 2010/11 na 2011/12 umeonyesha kuwa hakuna kiwanda kilichokidhi viwango vya utengenezaji wa dawa,” alisema ripoti yao.

TFDA katika taarifa yake hiyo inakiri kuwa viwanda vya dawa hapa nchini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita vimeshindwa kukidhi vigezo vya usajili wa dawa.

Kutokana na hali hiyo dawa za viwanda hivyo zimekuwa zikiruhusiwa na mamlaka hiyo kuwepo sokoni kwa kuzingatia utaratibu maalumu ambao hauzingatii vigezo vyote vya usajili wa dawa.

“Utaratibu huu ulikuwa wa muda mfupi uliokuwa na nia ya kutoa muda kwa kiwanda husika kurekebisha mapungufu ili dawa zao zisajiliwe. Baadhi ya dawa zinazotengenezwa na viwanda vya ndani ni za tiba za ugonjwa wa malaria na vijiua sumu,” iliongeza taarifa.

Pia inafafanua kuwa katika siku za karibuni, sampuli za matoleo (batches) kadhaa za dawa za viwanda hivyo zilizochukuliwa katika soko na kuchunguzwa zimeonekana kuwa na ubora duni na hivyo kuondolewa.

Ni katika mtiririko huo, mtoa habari wetu anasema TFDA haijawahi kutoa kibali kwa kiwanda cha TPI kuzalisha dawa za ARV’s kinachoonyesha kuwa kiwanda hicho kimekidhi vigezo tajwa.

Lakini katika hali inayoonyesha kutokuwepo umakini, TFDA ilizisajili dawa hizo za ARV’s kutoka TPI wakati katika ripoti yake wanakiri kuwa kiwanda hicho hakina sifa za kuzizalisha.

“Dawa inaweza kuwa moja lakini ikawa na matoleo tofauti, hivyo hata toleo hilo la dawa bandia zinazolalamikiwa halikuletwa TFDA kwa ukaguzi maana ingebainika haraka kabla ya kuingia sokoni,” kiliongeza chanzo hicho.

Ofisa huyo anashauri kuwa TFDA ilipaswa kuwa na mkaguzi wake ndani ya MSD ambaye angekuwa anasaidia kukagua na kuhakikisha dawa hizo hazizalishwi na kusambazwa.

“Hapa utaona kuwa haikuwa sahihi kumwajibisha mkurugenzi wa MSD pekee na kutuacha TFDA ambao hatukutimiza wajibu wetu. MSD hawana utaalamu wa kuchunguza dawa bandia hiyo ni kazi ya TFDA,” alisisitiza ofisa huyo.

Dawa hiyo bandia aina ya TT-VIR 30 toleo namba OC.01.85 iliyotengenezwa Machi 2011 na kuisha matumizi Februari 2013, nyaraka zake zilionyesha kiwanda cha TPI kiliwauzia MSD.

Waziri Mwinyi alieleza kuwa vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikuwa vimesajiliwa na TFDA.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA jana alipotafutwa kwa njia ya simu, alisema atatoa ufafanuzi wake leo akiwa ofisini.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU