Kutoka Taifa: Mpira umeisha Yanga wanatoka kifua mbele kwa Goli kwa sifuri
Kutoka Morogoro: Mpira umeisha Mtibwa Inatoka kifua mbele kwa 2 kwa sifuri
Kutoka Morogoro: Gooooool Mtibwa wanapata goli la pili hapa. Nilisema huyu Javu ana historia ya kufunga katika uwanja huu. Ndio maana mara zote tunaandika mtibwa wanaongoza kwa goli la kwanza na hili ni la pili
Kutoka Mtibwa: Dk 88 Mtibwa bado wapo mbele kwa goli la kwanza
Kutoka Morogoro: Mwinyi kazimoto anaachia shuti kali linapanguliwa na kipa na kuwa kona. Simba wanalisakama lango la mtibwa
Kutoka Morogoro: Husein Javu anaingia kuchukua nafasi ya Muhamed Mkopi. Huyu Javu ana historia nzuri ya kufunga katika uwanja huu
Kutoka Morogoro: Dk 79 Okwi anawakosakosa mtibwa na inakuwa kona. Husein Sharrif anapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda. askari wameongezwa uwanjani
Kutoka Taifa: Gooooooool Yanga wanaongeza goli la pili. Ni Hamis Kiiza "diego" anafunga goli safi sana hapa. Alivua jezi hapa kiiza anapewa kadi ya njano
Kutoka Taifa: Abdi Kassim anachukua nafasi ya Hamis Mcha.
Kutoka Taifa: Msuva anaenda nje anaingia Luhende.Yanga wanakosa goli baada ya Kavumbagu kuchelewa krosi ya Niyonzima
Kutoka Taifa: Dk 51 Erasto Nyoni anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumkanyaga Niyonzima wa Yanga.
Kutoka Taifa: Dk 48 Bocco anashindwa kuuwahi mpira aliopigiwa na Khamis Mcha lakini Chuji anautoa na kuwa kona. Azam inapata kona ambayo inakolewa na mabeki wa Yanga.
Kutoka Taifa: Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa kati ya Yanga na Azam
Kutoka Morogoro: Babu Ally anapewa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi emanuel Okwi. Na Mrisho Ngassa anaingia kuchukua nafasi ya Akuffor. Chollo anaingia nafasi ya Ochieng
Kutoka Morogoro: Mpira umeanza Jamal anatoka na anaingia Issa
Kutoka Morogoro: Washabiki wa Simba wamtupia chupa mwamuzi wa pambano hili, vile vile wamewarushia vilevile chupa wachezaji wao. mmoja wa washabiki hao wa simba amekamatwa na polisi. Ulinzi zaidi unahitajika katika mechi hii maana inaonekana washabiki wa simba hawana uvumilivu.

Taifa; Dk 45 HALF TIME..... AZAM 0-1 YANGA
Kutoka Morogoro: Mtibwa wanapata kona tatu mfululizo, lakini, Kaseja anadaka, dakika ya 42 sasa
Taifa: Dk 39 Yanga na Azam zinashambuliana kwa zamu na mpira unachezwa katikati sana.
Kutoka Morogoro: Mtibwa inaongoza kwa bao moja dhidi ya Simba, mfungaji Mohamed Mkopi. MTBWA 1-0 SIMBA
Taifa: Dk 32 Azam inapata kona baada ya Mbuyu Twite kuutoa mpira nje
Khamis Mcha anapiga kona lakini Bocco anautoa mpira nje.
Dakika ya 28, Akuffor, anashindwa kutumia makosa ya mlinzi wa Mtibwa ambaye alipiga pasi fupi kwa mwenzake na kuiwahi. Lakini, akiwa ndani ya sita anashindwa kuamua kufunga au kutoa pasi, na kupiga pasi mkaa iliyonaswa na mlinzi wa Mtibwa. Dakika ya 30 sasa.
Kutoka Taifa: Dk 28 Bocco anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini kipa Ally Mustapha anadaka
Dk 26 Athuman Idd Chuji anamchezea faulo Michael Bolou.
Kutoka Morogoro: Kwa dakika 20 za mwanzo, mechi bado imebalansi hakuna mashambulizi ya maana sana ambayo timu zinayaandaa. Kila timu inacheza kama haitafuti ushindi. Mara mbili, mshambuliaji, Said Mkopi wa Mtibwa amejaribu kumtoka Amir Maftah, lakini hakufanya cha maana. Emmanuel Okwi anajitahidi kuwakimbiza mabeki wa Mtibwa Sugar, lakini bado hapati, sapoti ya karibu kutoka Sunzu na Akuffor. Mtibwa, wamepiga kona nne hadi sasa, wakati,Simba, wamepata kona moja tu. Kiujumla, mchezo bado umepooza hadi sasa.
Kutoka taifa: Dk 18 Niyonzima wa Yanga,anakosa bao la wazi kwa kupiga nje mpira aliopokea kutoka kwa Oscar Joshua.
Dk 15 Erasto Nyoni wa Azam anamchezea rafu Msuva
Dk 14 Simon Msuva wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya kushindwa kuuwahi mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Dk 13 Mpira unachezwa kwa kasi sana na timu zote zinatawala kiungo
Kutoka MorogoroKwa dakika hizi kumi za mwanzo, timu zote zinaonekana kucheza kwa kuogopana zaidi. Mtibwa, walianza kufika katika lango la Simba, kupitia kwa Shaaban Nditti. Walinzi wa Simba, Keita na Ochieng, wakamthibiti. Bado hakuna soka la kuvutia na la mipango, japo, Mtibwa, wanaonekana kucheza kitimu hadi sasa. Simba, wanapata kona ya kwanza, lakini haina madhara, dakika ya 12
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog