Kikosi cha Yanga
Timu ya Yanga ya Dar es Salaam kama ilivyo kawaida yao wakifungwa au kutoka sare huwa hawakosi sababu tayari wameweka hadharani sababu ya wao kutoka sare na Ndanda Fc wana Kuchele kuwa eti Wachezaji wao walikuwa na mgomo baridi.
Na imedaiwa kuwa timu haikufanya mazoezi ya kwa siku tatu mfululizo kabla ya mchezo huo wa ligi kuu yaVodacom Tanzania Bara jambo ambalo hata hivyo, Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alilikana.
Imedaiwa wachezaji wa Yanga waligoma wakishinikiza kupewa mishahara yao ya mwezi Julai hadi walipokutana na Mwenyekiti, Yussuf Manji Jumatatu ambaye pia ni mfadhili ndipo wakasitisha mgomo wao.
Yanga ikasafiri Jumanne asubuhi kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo na Ndanda, uliomalizika kwa sare ya 0-0. Na waliingia kwenye mchezo wa huo baada ya mazoezi mepesi tu, tena ya siku moja Uwanja wa Nangwanda.
Yanga ilicheza kichovu ikilazimishwa sare na Ndanda kumbe kilichojificha nyuma ya hali hiyo ni timu kutofanya mazoezi kwa siku tatu.
Na inadaiwa huo ni mgomo wa pili ndani ya wiki mbili, baada ya awali wachezaji kugoma kuelekea mchezo wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
Inadaiwa waligoma kushinikiza kulipwa posho walizoahidiwa na Manji kwa kutwaa mataji matatu (Ligi Kuu, Kombe TFF na Ngao ya Jamii) msimu uliopita, kuwafunga mahasimu Simba mechi zote mbili na kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Hata hivyo, baadaye timu ilisafiri kwenda Lubumbashi, ambako ilichapwa mabao 3-1 na TP-MAZEMBE ya huko.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog