Mshambuliaji Romelu Lukaku amefunga
mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa Everton dhidi ya
Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja
wa Goodison Park.
Lukaku alifunga mabao hayo katika dakika
za tano na 37,wakati lingine lilifungwa na Barkley dakika ya 25 na
mabao ya Newcastle United yalifungwa na Cabaye dakika ya 51 na Remy dakika ya 89.
Mshambuliaji huyo anamuonyesha kocha wa Chelsea, Mreno Jose Mourinho kwamba alikosea kumruhusu kuondoka majira ya joto.
Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard, Baines, Distin, Jagielka, Coleman, Mirallas/Deulofeu dk73, McCarthy, Barry, Osman/Stones dk90, Barkley/Naismith dk88 na Lukaku.
Newcastle United: Krul, Debuchy,
Yanga-Mbiwa/Williamson dk45, Coloccini, Santon, Anita/Cisse dk69, Tiote,
Sissoko, Gouffran, Remy na Ben Arfa/Cabaye dk45.
Romelu Lukaku ameifungia mabao mawili Everton ikiilaza Newcastle 3-2 Uwanja wa Goodison Park
Dakika tano zilitosha kwa Lukaku kufunga bao la kwanza
Barkley akishangilia baada ya kufunga
Lukaku akifunga bao la kwanza
Lukaku akifunga bao lake la pili
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog