Macho
yote yalikuwa kwa Luis Suarez baada ya kurejea Liverpool kufuatia
kumaliza adhabu yake ya mechi 10, lakini Javier Hernandez akaiteka shoo
kwa bao lake pekee lililoipeleka Manchester United Raundi ya Nne ya
Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One.
Na
wakati mshambuliaji huyo wa Uruguay alizomewa na mashabiki Uwanja wa
Old Trafford, alikuwa ni Chicharito aliyepoza maumivu ya David Moyes
kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa wapinzani, Manchester City
katika Ligi Kuu Jumapili.Liverpool
ilitawala sehemu kubwa ya mchezo na Daniel Sturridge alipoteza nafasi
kadhaa za kufunga.
Wayne
Rooney, ambaye ndiye mchezaji bora zaidi kwa United hivi sasa, alipiga
kona nzuri baada ya mapumziko na Hernandez akaunganisha nyavuni.
Sasa Man United watamenyana na Norwich nyumbani baada ya kuwatoa Liverpool kwa bao moja hilo la Chicharito.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na Hernandez.
Liverpool: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Henderson, Suarez na Moses, Sturridge.
Javier Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao pekee la Manchester United Uwanja wa Old Trafford
Hernandez akienda hewani kuunganisha kona ya Wayne Rooney
David Moyes akishangilia bao la Hernandez
Luis Suarez akionekana mwenye furaha kuwa kikosini Liverpool tena
Suarez akipeana mkono na Wayne Rooney kabla ya mechi
Suarez alikaribia kufunga kipindi cha kwanza, lakini kipa wa United, David De Gea akaokoa
Suarez akipiga kichwa huku beki wa kushoto wa United, Alex Buttner akimuangalia
Beki wa United, Phil Jones akimchezea rafu Suarez
Gwiji wa United, Roy Keane alikuwa jukwaani akiangalia mechi
Rooney akipambana na Mamadou Sakho
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog