Saturday, July 13, 2013
KIIZA ATUA LEO JIONI KUSAINI YANGA MIAKA MIWILI
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego wa Kampala’ anatua
Alasiri ya leo Dar es Salaam na ndege ya KQ tayari kusaini Mkataba wa
kuendelea kuitumikia Yanga SC kwa miaka mingine miwili.
Hiyo
inafuatia mpachika mabao huyo kufikia makubaliano na Yanga juu ya dau
la usajili, baada ya awali kushindana hadi akarejea kwao, Kampala na
ikaripotiwa alikuwa karibuni kusaini URA ya kwao.
Mfanyabiashara
mwenye jina mjini, Mussa Katabaro alikwea pipa hadi Uganda wiki mbili
zilizopita kufanya mazungumzo ya kina na Kiiza ili abaki Yanga na
hatimaye akakubali kuendelea kuvaa jezi za kijani na njano kwa miaka
mingine miwili.
Katabaro
ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC na mmoja wa Wajumbe
wa Kamati ya Mashindano, chini ya Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb ameiambia
BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba Kiiza anatua na ndege ya shirika la
Kenya, KQ Alasiri.
Katabaro
alipokuwa Kampala katika mazungumzo yake na Diego walikubaliana
kumuongezea Mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola za Kimarekani 40,000
na mshahara wa dola 1,500 kwa mwezi.
Lakini
Katabaro akaomba Kiiza akubali kuchukua dola 20,000 kwa sasa na dola
20,000 nyingine atampa katika mwanzo wa mwaka wa pili wa Mkataba wake.
Kiiza akasema anataka dola 40,000 kamili kwa sababu ana kitu anataka
kufanya na ndiyo maana alikataa kupokea dola 35,000 na gari, ilia pate
fedha kamili.
URA ilikuwa tayari kumsaini Kiiza kwa mshahara wa dola 1,000 na dau la usajili dola 40,000 kama ambazo ameahidiwa Jangwani.
Awali, Kiiza aligoma kusaini Yanga kutokana na kulazimishwa achukue dola 35,000 na dola 5,000 nyingine apewe gari.
![]() |
| Anarudi; Hamisi Kiiza anatua leo |
HIVI NDIVYO CHADEMA WATAKAVYO TOA MSIMAMO WAO KUHUSU KATIBA MPYA LEO
Msimamo wetu kuhusu rasimu ya katiba mpya na mustakabali wa taifa
utatolewa leo Jumamosi ya Julai 13, 2013 kwenye mkutano wa hadhara
katika viwanja vya Shule ya Ukombozi-Manzese kuanzia saa 8 mchana.
Hotuba zitatolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Dk.W.Slaa, T.Lissu, M.Marando nk nathibitisha nami nitakuwapo kuwakaribisha Jimboni Ubungo.
Wananchi wote mnakaribishwa. Njoo wewe, njoo na yule!
Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli!
Muhimu:

- Shule ipo jirani na Manzese TipTop.
- Maelekezo wasiliana na M/Kiti wa Kata ya Manzese, Ali Makwilo 0784-691449 au 0715-691449 au 0769-658593
---
Taarifa hii imetolewa na:
John Mnyika (Mb)
Jumamosi, Julai 13, 2013
KIJANA WISEMAN LUVANDA ATEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR ES SALAAM
![]() |
| Wiseman Luvanda (23) akiwasili jijini Dar es Salaam alitokea Mbeya kwa miguu.Akiwa anaiunga mkono Timu ya Taifa |
![]() |
| Watu wakimpokea kwa shangwe kijana aliye onesha uzalendo wa hali ya juu |
Kijana Wiseman Luvanda(23) akikamilisha safari yake ya kutoka Mbeya hadi Dar kwa miguu! Kauli mbiu yake ni "Tanzania nchi yangu,Taifa Stars Timu yangu, Amka wakati wa Uzalendo ni Sasa". Tumefanya nn kuienzi nchi?
SIMBA YAMSAJILI HAMISI TAMBWE

Klabu
ya Simba ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajili mfungaji bora wa
michuano ya Kagame Cup 2013 Hamis Tambwe kutokea Vital O ya Burundi.
Tambwe ambaye pia alikuwa akiwania na mabingwa wa Tanzania bara Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba.

Tambwe amesaini mkataba huo mbele ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba.
Friday, July 12, 2013
OPRAH WINFREY KUJA TANZANIA KESHO
Inaelekea President Obama kaacha upepo mzuri Tanzania manake
taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita baada tu ya
bondia Evander kuthibitishwa na yeye kuja Tanzania, mtangazaji staa wa
dunia Oprah Winfrey nae anatarajiwa kufika Tanzania.
Staa huyu ambae amewahi kufanya interview na mastaa wengine kama marapper Jay Z na 50 Cent, unaambiwa usitegemee kumuona Dar es salaam au sehemu nyingine maarufu za town, anatua Serengeti kesho July 13 2013 kwa ajili ya mapumziko tu na kuondokea hukohuko.

TANGAZO LA AJIRA KUTOKA UTUMISHI
Sekretarieti
ya Ajira kwa niaba ya Tanzania Dairy Board, Tanzania Institute of
Accountancy, College of Business Education, National Institute of
Transport, Tanzania Broadcasting Cooporation, Tanzania Institute of
Education, Tanzania Library Services Board, Local Government training
Institute, Institute of Finance Management, National College of Tourism
Agency, Law school of Tanzania, Tanzania Metrological Agency, Moshi
Unoversity college of cooperative and business Studies, Dar es Salaam
Marine Institute, Kibaha Education Centre, Institute of Rural
Develepment Planning, Tanzania Public Service College, Tanzania Wildlife
Research institute, Institute of Accountancy Arusha na National
Examination Concil of Tanzania inawatangazia furasa mbalimbali za Ajira
Serikalini, Kwa maelezo zaidi fungua kwenye TOVUTI ya Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo ni www.ajira.go.tz.
POLISI WAFANYA UPELELEZI KUMPATA ALIE RUHUSU KILO 150 ZA MADAWA YA KULEVYA KUPITA AIR PORT
Akizungumza na gazeti la NIPASHE lililochapisha habari ya dawa za
kulevya kilo 150 zilizokamatwa kwa wasichana wa Kitanzania nchini Afrika
Kusini, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja wa Ndege Nchini, Deusdedit
Kato, amesema tukio hilo ni baya, limeifedhehesha Tanzania na kuiitia
dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu.
Hivyo amesema kuna haja ya kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi.
“Ni lazima tupambane kurudisha heshima kwa sababu watanzania watakuwa hawaaminiki tena katika nchi nyingine, ni mapema mno kuinyoshea kidole taasisi yeyote kwani uchunguzi bado unaendelea ili kubaini aliyeruhusu kupitisha mzigo huo, ”alisema alipoulizwa na gazeti hili kama wasichana hao walikaguliwa.
Alisema ni lazima kwa pamoja kufanya uchunguzi na kubaini ni taasisi gani ilipwaya katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuruhusu dawa hizo kupita.
Alisema mpaka sasa uchunguzi umefikia katika hatua nzuri na watatoa taarifa wakati wowote.
Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Polisi,Usalama wa Taifa,Uhamiaji na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA).
“Tukio hili ni baya limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu lakini sasa limetuchafua sana, tunahitaji kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi yetu iliyokuwapi hapo awaliaaaa,” alisema na kuongeza: "Wasichana hao inadaiwa kuwa walisafirisha dawa hizo kwa ndege ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini."
Hadi sasa wasichana hao bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa ajili ya upelelezi.

Thursday, July 11, 2013
VIDEO: MWANAMKE AKIMPIGA MUME WAKE HADHARANI
.
Ni ngumu kumuona mwanaume akitokwa machozi kama hivi…. hii
imetokana na mke wake kumpiga makofi hadharani kwenye mji wa Meru nchini
Kenya ambapo Mwanamke huyo alikua anadai jamaa kamkana, japo
anasisitiza kwamba ni mume wake na ndio baba wa watoto mapacha akiwemo
mmoja alienae mgongoni, Mwanaume alikataa kabisa na kusema hata watoto
sio wake.
Taarifa ambayo imerushwa na KTN Kenya, ni kwamba alichotaka
Mwanamke ni Mwanaume huyo akubali tu kwamba ni mume wake na pia ndio
baba watoto wa mapacha hao… lakini Mwanaume aliapa kabisa kwamba hausiki
kwenye upande wowote, hicho ndio kilichompa hasira Mwanamke na kuanza
kumpiga na baadae pia kusaidiwa kupiga na Mwanamke aliekua nae.
Kenya imekua kwenye mfululizo wa kesi za Wanawake kupiga
waume zao nyumbani na hadharani pale wanapokosana ambapo February 2012
Umoja wa Wanaume Kenya ulitangaza kususia kula majumbani kwa wiki moja
na kununua chakula hotelini mpaka Serikali itakapoingilia usawa wa
Wanaume na kuhakikisha tabia ya Wanawake kupiga Waume zao inamalizwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)