Facebook Comments Box

Monday, August 27, 2012

KITONGONI MNAIKUMBUKA BLACK FIGHTER FOOTBALL CLUB?

Mmoja wa wadau wa kitongoni blog Ramadhan Sendah kulia akiwa na wachezaji wa zamani wa Black Fighter Football Club katikati ni Mbayo Masoud ambaye alikuwa ni kiungo wa timu ya Black Fighter FC na Kapteni Mabo akijulikana enzi hizo kama Umeme. Wakati Mbayo alikuwa kiungo wa chini dimba la juu lilikuwa likishikwa na Kapteni Mabo (Umeme)
Mbayo Masoud watu hawana historia ya kumuona akikosa penati. Kila ikipatikana penati akishika mpira uwanja mzima wananyanyuka kushangilia goli kabla hajapiga.
Wadau mnawakumbuka hawa?

ZIARA YA YANGA IKULU RWANDA

Hapa akikabidhiwa kombe na nahodha wa timu ya Yanga Nadir Haroub Canavaro na kocha wa Yanga



Hapa Rais Kagame akiwahutubia na kuwapongeza

 Mwenyekiti wa Yanga Manji akimsikiliza kwa makini Mh Rais Kagame

Hapa Mwenyekiti wa Yanga akitoa risala yake kwa Rais

Hapa Rais akiwakaribisha

Bahanuzi mfungaji bora wa kombe la afrika mashariki na kati akigawa shughuli huko Rwanda
Hapa akikabidhiwa jezi




JEZI ZA YANGA ZAGOMBEWA RWANDA

Picha mbalimbali zikionesha wananchi wa Rwanda wakigombea jezi za Young Africans sports Club (Yanga). Yanga ndio mabigwa wa kombe la Africa mashariki na kati linalosimamiwa na CECAFA maarufu kwa jina la Kagame.








Sunday, August 26, 2012

ARSENAL WATOKA SULUHU NA STOKE CITY



S0-0A www.fasthighlights.com by fasthighlights-2012

SIMBA WAITAMBIA MATHARE UNITED

Simba  ikipambana na Mthare United katika uwanja wa Shekh Abeid huko Arusha. Imeibuka na ushindi wa gili 2 kwa 1.Mchezo huu ni wa kirafiki kati ya timu hizi, Simba ikijiandaa na ligi kuu ya Tanzania.
Simba inacheza mechi hiyo kutokana na maombi ya kocha wake Mkuu Milovan Cirkovic, kutaka kuona wachezaji wake ambao wamesajili hivi karibuni.
Simba inawakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kushika nafasi ya pili.

HASHEEM THABEET NA NYOTA WENZAKE WA NBA WATOA MAFUNZO YA KIKAPU DAR






NYOTA wa mpira wa kikapu kutoka Marekani, Hasheem Thabeet Mtanzania anayehezea Oklahoma City, Luol Deng Muingereza mwenye asili ya Sudan Kusini, anayechezea Chicago Bulls leo wameendesha programu ya kliniki kusaka vipaji vya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam kwenye viwanja vyta Don Bosco, Upanga.


Kliniki hiyo ilihudhuria na nyota wengine wa NBA, akiwemo Adam Andre, Masai Ujiri, mmiliiki na Meneja wa timu ya Denver Nuggets, Amadaou Gall Fall na Kocha J.


Alikuwepo pia Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Tanzania, Juliana Yassoda, Balozi Mdogo wa Marekani, Robert K Scott, Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu (TBF), Mussa Mziya na Makamu wake, Phares Magesa.

Zoezi lilianza saa nne asubuhi kwa hotuba ndefu, zilizowafanya watoto waungue juwa muda wa zaidi ya saa mbili, kabla ya kuanza kupewa mafunzo hayo. Pichani ni watoto waliohudhuria wakiteseka na jua kwa kusikiliaza hotuba ndefu.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU