Facebook Comments Box

Monday, July 15, 2013

THIAGO ALCANTARA AITOSA MAN UNITED NA KUJIUNGA NA BAYERN MUNICH



Hatimaye kiungo wa kimataifa wa Spain na FC Barcelona Thiago Alcantara ameuzwa rasmi kwenda kujiunga na mabingwa wa ulaya na Ujerumani Bayern Munich.

Thiago ambaye alikuwa akihusishwa mno na kujiunga na Manchester United ingawa juzi kocha David Moyes alisema hawakuwahi kusema wanamhitaji mchezaji, amejiunga rasmi ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa 25 million euros.

Mapema wiki iliyopita kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alikaririwa akisema kwamba anamhitaji Thiago kwenye timu yake na amewaomba viongozi wake kumsajili mchezaji huyo tu msimu huu.

Thiago amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Bayern Munich.


PICHA: HALI ILIVYOKUWA JANA KATIKA UPIGAJI KURA ARUSHA

 Polisi wakimsihi Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari  aondoke nje ya kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu,pamoja na makada wa CCM hawako pichani ambapo walitakiwa kukaa mita 200 badala ya mita 100.
 Polisi wakimsihi Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari  aondoke nje ya kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu,pamoja na makada wa CCM hawako pichani ambapo walitakiwa kukaa mita 200 badala ya mita 100.
 Makarani wa uchaguzi wakiingiza masanduku ya kura katika ofisi ya kata ya Kimandolu kutoka  kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi kimandolu. 
Makarani wa uchaguzi wakiingiza masanduku ya kura katika ofisi ya kata ya Kimandolu kutoka  kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi kimandolu. 
 Polisi wakiimarisha ulinzi katika lango kuu la kuingilia  kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu katika uchaguzi ulifanyika leo mjini Arusha. 
 Mkazi wa kata ya kimandolu akichomvya wino mara baada ya kukamilisha zoezi  la kumchagua diwani wa kata hiyo liliofanyika jana katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata.
 Mkazi wa Kata ya Kimandolu akitumbukiza kura yake wakati wa uchaguzi wa madiwani uliofanyika mjini Arusha.
 Mkazi wa kimandolu,Juliana Mosha akitumbukiza kura yake katika sanduku la kura katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika jana kuziba nafasi  ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo,zoezi hili lilifanyika katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
 Dina Naftal Mkazi wa kata ya kimandolu akitumbukiza kura yake katika sanduku la kura katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika jana kuziba nafasi  ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo,zoezi hili lilifanyika katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata.
 Wakala wa chama cha siasa akihakiki kitambulisho cha mpiga kura kabla ya kuruhusiwa kupiga kura ya kumchagua diwani wa kata hiyo ya Kimandolu,zoezi hili lilifanyika katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
 Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini ili kufahamu vyumba husika vya kupigia kura ya kumchagua diwani wa kata hiyo liliofanyika jana katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
 Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini ili kufahamu vyumba husika vya kupigia kura ya kumchagua diwani wa kata hiyo liliofanyika jana katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini ili kufahamu vyumba husika vya kupigia kura ya kumchagua diwani wa kata hiyo liliofanyika jana katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata 
 Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini ili kufahamu vyumba husika vya kupigia kura ya kumchagua diwani wa kata hiyo liliofanyika jana katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
Polisi akiwasogeza wananchi waliokuwa karibu na kituo cha kupigia kura cha Shule ya msingi Kimandolu ambapo walitakiwa kukaa umbali wa mita 200 na sio mia 100 kama ilivyozoeleka.(Picha zote na Ferdinand Shayo)


Sunday, July 14, 2013

MAWAIDHA: SHEIKH RASHID AL-SHUKERY - MOYONI HADI MOYONI




SHEIKH WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI

  
 
Sheikh Said Juma Makamba akiwa hospitali
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.

Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.

Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.

Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.

Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.

Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu

 huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.

‘’Wakati natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa  akilia.

Pamoja na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na  mgongoni, pia ana majeraha  kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.

Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.

Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.

Kwa upande wake,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna  mtu anayeshikiliwa hadi sasa.



FREEMAN MBOWE AVAMIWA NA POLISI USIKU WA MANANE

 
Freeman Mbowe
KUNDI la polisi wenye silaha za moto jana usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata.

Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.

Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.

Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.

Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza 
kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.

Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.

“Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo,” alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.

“Kwa kweli ndiyo napata taarifa hizo kutoka kwako, kuwa kiongozi huyo alifuatwa na polisi, maana silijui suala hilo hata kidogo,” alisema Wambura, naye kama alivyofanya Kimola akakata simu.

Lakini wakati Kimola akikataa kusema chochote, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Kimola kuhusiana na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo wa juu wa kisiasa, na kudai kupewa majibu ya kushangaza.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Wilaya ya Kinondoni, Dk. Slaa alisema Kimola alijitetea akidai kwanza kukana kufika nyumbani kwa Mbowe usiku wa manane. Pili, alisema kuwa hawakwenda kumkamata Mbowe, isipokuwa kufanya naye mazungumzo na kisha wangemwacha.

Slaa alisema kitendo hicho kimewashitua na ni cha kinyama na kilichokiuka sheria za nchi na haki za binadamu. Aliongeza kwamba, daima wamekuwa wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kutumika vibaya kukandamiza wapinzani, lakini mara zote CHADEMA kimepuuzwa na sasa jeshi hilo limeamua kuvamia makazi ya viongozi wa kisiasa kwa madhumuni yasiyoeleweka.

Alisema haijulikani nini kingetokea ikiwa Mbowe angekuwa ndani, ikiwa walinzi wangeamua kugoma kumwachia kiongozi wao. “Tuna hofu kubwa na usalama wetu, maana pale wangeweza kufanya lolote, hata kumuua na kisha kutoa matamshi kuwa walikuwa wanajibishana kwa risasi, kama ambavyo imekuwa jadi ya askari polisi kutoa taarifa za uongo na upotoshaji wanapoua watu,” alisema Slaa.

Alisema ikiwa polisi walikuwa na shida ya kweli, wangemwita kwa njia sahihi na si kumvamia na kuingilia uhuru wake na wa familia yake kama wanakamata gaidi ama jambazi hatari.

Dk. Slaa alisema Mbowe anayo ofisi inayojulikana, na kama kweli hakukuwa na jambo baya lililopangwa na polisi hao wasingeweza kufanya uhuni kama walioufanya.

“Kama wanaweza kuvamia nyumbani kwa kiongozi mkubwa kama Mbowe wakiwa na silaha nzito, itakuwaje kwa viongozi wa kawaida na raia?” alihoji Slaa.

Kutokana na tukio hilo la kuogofya, CHADEMA imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania maana ya matukio haya ambayo yamedhamiria kuleta vurugu kubwa nchini. Kadhalika, wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuueleza umma kile kilichokusudiwa na askari wake kuvamia nyumbani kwa Mbowe mithiri ya jambazi.

Itakumbukwa pia kuwa hivi karibuni askari polisi wa Mkoa wa Arusha walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakiwa na silaha nzito na mbwa, na kumkamata, kisha kumtupa rumande kwa siku nzima.


---Imenukuliwa kutoka TANZANIA DAIMA


Saturday, July 13, 2013

VIDEO ZA UKUMBUSHO KWA WAISLAM WOTE WALIO FUNGA








VIDEO: VIDOKEZO VYA KATIBA MPYA KIKIWEMO CHA SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU






KIIZA ATUA LEO JIONI KUSAINI YANGA MIAKA MIWILI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego wa Kampala’ anatua Alasiri ya leo Dar es Salaam na ndege ya KQ tayari kusaini Mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga SC kwa miaka mingine miwili.  Hiyo inafuatia mpachika mabao huyo kufikia makubaliano na Yanga juu ya dau la usajili, baada ya awali kushindana hadi akarejea kwao, Kampala na ikaripotiwa alikuwa karibuni kusaini URA ya kwao. Mfanyabiashara mwenye jina mjini, Mussa Katabaro alikwea pipa hadi Uganda wiki mbili zilizopita kufanya mazungumzo ya kina na Kiiza ili abaki Yanga na hatimaye akakubali kuendelea kuvaa jezi za kijani na njano kwa miaka mingine miwili.
Anarudi; Hamisi Kiiza anatua leo
Katabaro ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC na mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Mashindano, chini ya Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba Kiiza anatua na ndege ya shirika la Kenya, KQ Alasiri. Katabaro alipokuwa Kampala katika mazungumzo yake na Diego walikubaliana kumuongezea Mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola za Kimarekani 40,000 na mshahara wa dola 1,500 kwa mwezi. Lakini Katabaro akaomba Kiiza akubali kuchukua dola 20,000 kwa sasa na dola 20,000 nyingine atampa katika mwanzo wa mwaka wa pili wa Mkataba wake. Kiiza akasema anataka dola 40,000 kamili kwa sababu ana kitu anataka kufanya na ndiyo maana alikataa kupokea dola 35,000 na gari, ilia pate fedha kamili. URA  ilikuwa tayari kumsaini Kiiza kwa mshahara wa dola 1,000 na dau la usajili dola 40,000 kama ambazo ameahidiwa Jangwani. Awali, Kiiza aligoma kusaini Yanga kutokana na kulazimishwa achukue dola 35,000 na dola 5,000 nyingine apewe gari.



HIVI NDIVYO CHADEMA WATAKAVYO TOA MSIMAMO WAO KUHUSU KATIBA MPYA LEO

Msimamo wetu kuhusu rasimu ya katiba mpya na mustakabali wa taifa utatolewa leo Jumamosi ya Julai 13, 2013 kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Ukombozi-Manzese kuanzia saa 8 mchana.

Hotuba zitatolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Dk.W.Slaa, T.Lissu, M.Marando nk nathibitisha nami nitakuwapo kuwakaribisha Jimboni Ubungo.

Wananchi wote mnakaribishwa. Njoo wewe, njoo na yule!

Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli!

Muhimu: 
  • Shule ipo jirani na Manzese TipTop. 
  • Maelekezo wasiliana na M/Kiti wa Kata ya Manzese, Ali Makwilo 0784-691449 au 0715-691449 au 0769-658593

---
Taarifa hii imetolewa na:
John Mnyika (Mb)
Jumamosi, Julai 13, 2013



KIJANA WISEMAN LUVANDA ATEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR ES SALAAM

Wiseman Luvanda (23) akiwasili jijini Dar es Salaam alitokea Mbeya kwa miguu.Akiwa anaiunga mkono Timu ya Taifa


Watu wakimpokea kwa shangwe kijana aliye onesha uzalendo wa hali ya juu

Kijana Wiseman Luvanda(23) akikamilisha safari yake ya kutoka Mbeya hadi Dar kwa miguu! Kauli mbiu yake ni "Tanzania nchi yangu,Taifa Stars Timu yangu, Amka wakati wa Uzalendo ni Sasa". Tumefanya nn kuienzi nchi?

SIMBA YAMSAJILI HAMISI TAMBWE

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajili mfungaji bora wa michuano ya Kagame Cup 2013 Hamis Tambwe kutokea Vital O ya Burundi.

Tambwe ambaye pia alikuwa akiwania na mabingwa wa Tanzania bara Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba.
Tambwe amesaini mkataba huo mbele ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU