Facebook Comments Box

Wednesday, June 12, 2013

HII NDIO VIDEO YA MCHUNGAJI ALIENASWA AKIMTOMASA MUUMINI WAKE

clip_image002KATIKA  hali ya kushangaza , mchungaji mmoja huko nchini Nigeria amejikuta akiaibika baada ya video yake aliyokuwa  akimtomasa  mwanamke  wakati wa  maombi  kuvuja na kusambaa kitika mitandao mbali mbali ya kijamii.
Video hiyo ilirekodiwa kwa kutumia kamera zilizokuwa zimetegeshwa kitika ofisi ya mchungaji huyo bila yeye kujua.

Tazama video ya mchungaji huyo hapa
 

AMPIGA MUMEWE BAADA YA KUKUTA AKIANGALIA TV KABLA YA KUMALIZA KAZI ZA NYUMBANI

MWANAMUME mmoja katika mtaa wa Mwanzo, Eldoret anauguza majeraha baada ya kupigwa na mkewe kufuatia mzozo uliotokana na yeye kupatikana akitazama runinga kabla ya kumaliza kazi ya nyumbani.

Kwa mujibu wa majirani mkewe mwanamume huyo, alirejea nyumbani jioni kutoka kazini mnamo Jumatatu na kumkuta akitazama televisheni. Mara moja, alimrukia na kumpiga vibaya.

Mwanaume huyo aliokolewa na majirani waliofika kuitika kilio chake na kumkuta akigaragara sebuleni kutokana na maumivu. Walimpeleka katika zahanati ya kibinafsi alikotibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Majirani walisema wawili hao wamekuwa wakigombana mara kwa mara baada ya mwanamume huyo
kufutwa kazi miezi michache iliyopita.

Wakazi wa Mwanzo sasa wanalitaka Shirika la Maendeleo ya Wanaume kuingilia kati na kuokoa wanaume ambao wanadai wanadhulumiwa na kuchapwa na wake zao kila siku. Wanasema visa hivyo vimeongezeka mtaani humo. Aidha, wanataka wanaume hao wapewe ushauri wa kisheria kuwasaidia kutafuta usaidizi.

Mmoja wa wakazi, Justus Mwaniki, alisema wanaume wengi wanapigwa na wake zao kwa kuonekana kama mzigo nyumbani hasa wanapokosa kazi: “Sisi huwatunza wake zetu, na kukidhi mahitaji hao hata wakiwa hawana kazi na huleta nyumbani mapato yetu kwa matumizi ya familia. Mbona wadhulumu wanaume ambao hawana kazi?” alishangaa.

Majuzi, kiongozi wa Maendeleo ya Wanaume Nderitu Njoka alijipata taabani baada ya kukaripiwa na mwanamke mwenye nyumba kaunti ya Kiambu alipokuwa ameenda kumwoka mwanamume aliyedai alikuwa akizuiliwa na kudhulumiwa nyumbani.


KIBONZO: KUSIGANA KWA MAONI YA CUF TANGANYIKA NA CUF ZANZIBAR

Picture


CCM YAPATA UGENI KUTOKA PALESTINA


Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO,
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat (Kushoto). Wapili kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini  Dk. Nasri Abujasir.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizingumza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuanzia saa 3.30 asubuhi hii, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam


WIMBO MPYA WA CHRISTIAN BELLA




Tuesday, June 11, 2013

WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AACHIWA KWA DHAMANA NA MAHAKAMA LEO

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Wilfred Lwakatare 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  imekubali kumwachia Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare kwa dhamana ya Sh10Milioni.

VIDEO YA WIMBO JIKUBALI WA BEN POL AMBAO NDANI AMEMUIMBA LADY JAY DEE




VIDEO: BALOZI WA MAREKANI AKIELEZEA UJIO WA RAIS OBAMA TANZANIA




STAR TV WAGOMA KURUDISHA MATANGAZO YAO STAR TIMES

Siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuagiza matangazo ya Star TV yarejeshwe kwenye kisimbuzi cha Star Times ifikapo saa 10 jioni jana, televisheni hiyo imegomea agizo hilo na imetishia kwenda mahakamani ikiwa italazimishwa kurejea humo.

Taarifa ya kugoma agizo hilo, ilitolewa jana na Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group Ltd, Kampuni inayomiliki Star TV, Nathan Lwehabura.

Ilieleza kuwa kinachofanywa na TCRA, kuwalazimisha kurejesha matangazo Star Times ni ukiukwaji wa Sheria ya Hatimiliki na  Sheria ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.

"Serikali ya Tanzania ni mwanachama wa WTO na pia WIPO (World Intellectual Property Rights Organization) na hivyo kwa kulazimisha uvunjaji wa sheria za hati miliki ina maana inavunja haki zetu zilizopo kikatiba! Tutakwenda mahakamani kupata haki yetu hii muhimu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pamoja na kutoweka bayana lini watakwenda mahakamani, Lwehabura alisema sheria ya hati miliki inaweka 
kinga kwa vipindi vya redio, televisheni, nyimbo na sanaa. Alisema kulazimisha Star Times kupora vipindi vya Star TV, inadhihirisha kilio cha wasanii wa Tanzania, wasivyolindwa na Serikali yake.

Taarifa hiyo ilieleza Mei 23 mwaka huu, Star TV kupitia mwanasheria wake iliwataka Star Times kuiondoa kwenye kisumbuzi chao ifikapo saa sita usiku wa Mei 31, mwaka huu kutokana na kurusha na kuuza maudhui na vipindi vyake bila idhini na kukiuka sheria za haki miliki (Copyright laws).

"Katika barua hiyo, Star TV iliwakumbusha Star Times kwamba hawakuwa na mkataba wa kurusha kituo hicho kwa mujibu wa sheria ya EPOCA, pia hawana haki ya kutumia maudhui yake bila idhini chini ya Sheria ya Haki miliki ya Tanzania na kimataifa," ilieleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, Mei 31 Star Times/Star Media walijibu kwamba hawajakiuka sheria yoyote. Walisisitiza wataendelea kuirusha Star TV, kutekeleza matakwa ya sheria ya EPOCA na kanuni zake. Lakini, Star TV iliwaandikia tena na kuwaeleza itachukua hatua zaidi kwa kukiuka ;na kuwataka iwaondoe saa sita usiku wa Juni 8, mwaka huu.

Tarehe 6 Juni mwaka huu, Star TV iliwaandikia tena Star Times ikisisitiza nia yake ya kuchukua hatua zaidi, kutokana na wao kuendelea kukaidi ombi hilo na kuainisha mapungufu kadhaa ya kisheria kwa upande wao, yanayoifanya Star TV ijiondoe kwenye king'amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 8 Juni, mwaka huu na kufanya hivyo.

Jana, TCRA, kupitia Mkurugenzi Mkuu, Profesa John Nkoma, iliagiza chaneli hiyo irejeshwe mara moja jana ifikapo saa 10 jioni na kuzitaka pande hizo mbili, kukutana na mamlaka Juni 17 mwaka huu kwa majadiliano zaidi.

Hata hivyo, mpaka jana saa 11.20 jioni, Star TV haikuwa inaonekana kwenye Star Times huku TCRA ikidai Star TV inakiuka sheria ya EPOCA na ikikaidi, itachukuliwa hatua kwa kuwa si yenyewe wala Star Times walioko sawa katika maamuzi hayo.

TCRA iliwataka watoa huduma hao kufuata Sheria, inapotokea kutokuafikiana katika jambo fulani badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA), kwani kufanya hivyo ni kuwakosea haki wananchi.

Hata hivyo, Star TV imesema haipo tayari kuona maudhui yake yakiuzwa nje ya nchi bila makubaliano.  Star Times jana hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo. Lakini, awali, Msaidizi wa Meneja wa Star Times, Hellen Elisa alithibitisha kujitoa kwa Star TV. Alisema waliwaandikia barua na kudai wamejitoa kwa matakwa yao.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 


“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 06. 2013.

WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA VIFO.

 MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO VWAWA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.840 BKD AINA YA TOYOTA HARRIER LIKIENDESHWA NA DEREVA BROWN S/O MWAKIBAMBO,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O HALINGA,MIAKA 27,MKULIMA MKAZI WA ILOLO AKIWA  AMEMBEBA MTOTO WAKE AITWAE HELENA D/O SAMSON,UMRI  WA MWAKA MMOJA NA NUSU, KYUSA  NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI . TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

 
WILAYA YA KYELA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.


MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO GWAKISA ENEO LA KYELA - KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. LUKINDO S/O JOHN,MIAKA 45 NA 2. MSEMAKWELI S/O JOHN, MIAKA 27 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI RWANDA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA ZA KISHERIA  DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.

 
Signed By,

 [DIWANI ATHUMANI - ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Monday, June 10, 2013

TAIFA STARS YAWASILI LEO KUTOKA MOROCCO

 

IMG_5878
 Wachezaji wa Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Jumatatu alfajiri wakitokea Morocco.
IMG_5874
IMG_5825
-Asema adhabu ya kadi nyekundu haikuwa na ulazima
-Asema wangecheza 11 ushindi ulikuwa wazi
Kocha wa Timu bali matokeo ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa wa mechi ya Taifa Stars na Morocco iliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la  Dunia Brazil mwakani aliuwa mchezo kwa kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.
Akitoa maoni ya mchezo huo, Poulsen alisema alisikitishwa na jinsi refa huyo alitoa adhabu kali ambayo haiendani na kanuni za FIFA.
Aggrey Morris alioneshwa kadi nyekundu baada ya kugongana na Abderazak Hemed Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katika dakika ya 37.
“Hakuwa na sababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa Morocco penalti, alisema Poulsen huku akiongeza, “FIFA imeshawaonya marefa mara kadhaa dhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu kali kupita kiasi.”

Poulsen alisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana uwanjani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kyemba. Morocco walishinda kwa 2-1.
“Kama tungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii lakini refa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama hii,” alisema Poulsen.
Kocha huyo alisema kupata goli la ugenini unapochez na timu ngumu kama Morocco ni jambo la kujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitiza kuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast Jumapili ijayo. “Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya kushinda mechi ya Jumapili.
Tanzania iko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6, Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa Stars imerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na itaendelea na kambi ya wiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory Coast.
Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa na walifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
“Tulipata faraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameisha sasa tuangalie Ivory Coast,” alisema.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema wacezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa walicheza pungufu na hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
“Katika hali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja linaonesha kuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi,” alisema Bw Kavishe.
Alisema wao kama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini hii ni safari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita
 
SOURSE: MO blog


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU