Facebook Comments Box

Friday, May 24, 2013

BREAKING NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI YANGA

 
WAKATI Haruna Niyonziam akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, habari zilizotufikia hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na mtandao huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema Kiemba amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao huu unaahidi kuwasiliana na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini katika kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake kwa Yanga.
Kiemba aliwahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA


M23 KUIVAMIA TANZANIA; WANANCHI WA KAGERA WATAHADHARISHWA

Serikali ya Mkoa wa Kagera imewatahadharisha wananchi wake kuepukana na wageni wasiowafahamu kwenye maeneo yao kutokana na tishio la kikosi chaM 23 cha nchini Congo DRC kinachotishia kuivamia Tanzania...
Kumekuwa na mapigano  makali  kati  ya waasi waM23  na  vikosi vya serikali  nchini  Congo ambako jeshi letu lipo huko...
Waasi  hao  wametishia  kuivamia  Tanzania  muda  wowote  ili  kulipiza  kisasi.Miongoni mwa mipaka ambayo iko wazi  ni Kagera, na hii ndo sababu iliyopelekea  serikali ya Mkoa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla....


HATIMAYE NIYONZIMA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI

Miaka miwili zaidi; Haruna  Niyonzima kushoto akiwa na mwanawe, ameongeza miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga. Hapa alikuwa anapokea Medali ya ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kutoka kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga
HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.
Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.
 Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
 Mwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb
SOURSE: BIN ZUBEIRY


Thursday, May 23, 2013

MAJAMBAZI WAMELIVAMIA HILI GARI NA KUPORA PESA LEO




Matundu matatu ya risasi katika kioo cha gari lililovamiwa na majambazi.

Wanausalama barabarani wakichukua taarifa eneo la tukio.

Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya VITZ N a kuwajeruhi watu wawili wenye asili ya asia na kupora kiasi cha fedha ambacho bado thamani yake haijafahamika mara moja.


KIBONZO: VURUGU ZA MTWARA

Picture


SHEHA AMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR

\
Sheha Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.

Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.


BUNGE LA AHIRISHWA TENA LEO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
BUNGE LAAHIRISHWA TENA LEO:Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee  kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.


Wednesday, May 22, 2013

MACHAFUKO YA MTWARA OFISI YA CCM YACHOMWA MOTO


clip_image001

MAPAMBANO kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara umefika katika hatua mbaya,kiasi cha mtu mmoja kudaiwa  kujeruhiwa vibaya baada ya kurushiwa bomu wakati wa mashambulizi hayo katika eneo la Magomeni.
Mbali na kujeruhiwa kwa mtu huyo aliyekuwa katika maandamano ya kupinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia imechomwa moto.
Taarifa zilizonaswa na Fahari ya Kusini hivi punde zinadai kwamba wananchi wa Mkoa wa Mtwara wamefungiwa majumbani tangu asubuhi, huku Jeshi la Polisi likifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwanasa watuhumiwa wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo kwa njia ya vipeperushi.
Shuhuda wa wa tukio hilo ameitaarifu Fahari ya kusini  kwamba waandamanaji hao wameapa kufa endepo serikali itaendelea na mipango yake ya kusafirisha gesi hiyo hadi Jijini Dar es Salaam. "Hali hapa ni mbaya, tangu asubuhi wananchi wote wamefungiwa ndani ya majumba yao, hakuna anayeruhusiwa kutoka nje, Polisi wanapiga mabomu ya machozi kila mtaa huku wakiwasaka watuhumiwa waliosambaza vipeperushi na kuwatawanya wandamanaji waliozagaa katika mitaa  mbalimbali, mpaka hivi sasa kuna mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya raia na Asakari Polisi wanaotumia mabomu ya machozi na silaha zigine za moto"alisema shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo imedaiwa kuwa hali hiyo imesababisha barabara zote kufungwa kiasi cha kuzuia mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU yametanda kila kona za mji, huku taarifa zidi ikifafanua kwamba hakuna mawasiliano, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi ya nyumba maeneno ya Shangani zimechoma moto.


Tuesday, May 21, 2013

HII NDIO RATIBA YA KAGAME CUP NA MAKUNDI WALIYOPANGWA SIMBA NA YANGA




















Droo ya makundi kwa ajili ya mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati al-maarufu kama (KAGAME CUP) imefanyika leo mchana mjini Khartoum nchini Sudan huku Mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Young Africans wakipangwa kundi C kwenye michuano hiyo itakayoanza 18 Juni - 2 Julai 2013.
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye imeonyesha mashindano ya mwaka huu itakua na jumla ya timu 13 kutoka katika nchi 10 wanachama ambapo droo hiyo imegawanyika katika makundi 3 ya A,B,C.
Timu zitakazo shiriki mashindano hayo na nchi zinazotokea kwenye mabano ni : Al-Hillal, El-Merreikh na Al Shandy (Sudan), Al Nasri (Sudan Kusini), Yanga & Simba (Tanzania), Express (Uganda), Tusker (Kenya), APR (Rwanda), Vitaloo (Burundi),  Ports (Djbouti), Elman (Somalia) na Falcon (Zanzibar)
Aidha mashindano ya mwaka huu yameongeza zawadi kwa washindi kutoka kitita cha dola za kimarekani 60,000 mpaka kufikia dolla 80,000 ikiwa kuna ongezeko la dola 20,000 ambapo zawadi kwa washindi zitapangwa na kamati ya utendaji kabla ya mashindano kuanza.
Mashindano ya CECAFA mwaka huu yatafanyika nchini Sudan katika miji ya El-Fashir na Kadugli ambayo ni miji iliyopo kusini mwa nchi ya Sudan yenye wakazi wapatao milioni 34 na eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 1,886,068.
Makundi ya michuano hiyo itakayoanza mwezi ujao ni kama ifuatavyo:

KUNDI A: El-Merrekh -(Sudan), APR (Rwanda), Simba SC (Tanzania), Elman (Somalia) - EL FASHER

KUNDI B: Al-Hillal (Sudan), Tusker (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar),  Al Shandy (Sudan) - KADUGLI

KUNDI C: Yanga SC (Tanzania), Express (Uganda), Ports (Djibout), Vitaloo (Burundi) - EL FASHIR

 KAGAME CUP FIXTURE 18th JUNE - 2nd JULY 2013 (EL-FASHIR & KADUGLI - SUDAN)
DATETEAMTEAMGROUP/TIMEVENUE
18.06.2013.TUSKER SUPER FALCON B - 2:00 PMKADUGLI
 AL HILLAL AL NASRI B - 4:00 PMKADUGLI
19.06.2013.VITALOOPORTS  C - 4:00 PMEL-FASHER
20.06.2013.YANGA SC EXPRESS C - 2:00 PMEL-FASHER
20.06.2013.ELMAN FC APR FC A - 4:00 PMEL-FASHER
20.06.2013.SUPER FALCON AL NASRI B -2:00 PMKADUGLI
20.06.2013.TUSKER AL-SHANDY B - 4:00 PMKADUGLI
21.06.2013.EL MERREIKH SIMBA SC A - 4:00 PMKADUGLI
22.06.2013.EXPRESS FC VITALOO C - 2:00 PMEL-FASHER
 PORTS YANGA SC C - 4:00 PMEL FASHER
22.06.2013.AL NASRITUSKER B - 2:00 PMKADUGLI
 AL SHANDY AL HILAL B - 4:00 PMKADUGLI
23.06.2013APR SIMBA SC A - 2:00 PMEL-FASHER
 EL MERREIKH  ELAM FC A - 4:00 PMEL-FASHER
24.06.2013AL NASRI AL SHANDY B - 2:00 PMKADUGLI
 SUPER FALCON AL HILLAL B - 4:00 PMKADUGLI
24.06.2013. PORTSEXPRESS FC C - 4:00 PMEL-FASHER
25.06.2013.VITALOO YANGA SC C - 4:00 PMEL-FASHER
26.06.2013.AL SHANDY SUPER FALCON B - 2:00 PMKADUGLI
 AL HILLAL TUSKER B - 4:00 PMKADUGLI
26.06.2012.SIMBA SC ELMAN FC A - 2:00 PMEL-FASHER
 APR FC EL MERREIK A - 4:00 PMEL-FASHER
27.06.2013.REST DAYREST DAYREST DAY  REST DAY
28.06.2013.(23) B2 VS C2(24) B1 VS BEST QTBDKADUGLI
28.06.2013.(25) C1 VS A2(26) A1 VS B3TBDEL-FASHER
30.06.2013.WNR 23 VS WNR 25WIN 24 VS WIN 26TBD 
01.07.2013.REST DAYREST DAYREST DAYREST DAY
02.07.2013.LOOSER LOOSER 283RD - TBDEL-FASHER
  WINNER 27 WINNER 28  FAINAL - TBDEL-FASHER




AZAM TV KUONESHA LIGI KUU YA TANZANIA BARA MSIMU UJAO WA 2013/2014



Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) inayomiliki klabu tajiri ya Azam FC ipo mbioni kumwaga zaidi ya 1.5 bilioni kwa timu zote za ligi kuu Bara msimu ujao na itarusha moja kwa moja (Live) zao kupitia televisheni yao mpya ya AZAM TV ambayo inatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni ambapo ujenzi wa kituo hicho unaendelea katika Jengo moja lililopo Barabara ya Mandela, Jijini Dar es Salaam.

Habari za uhakika zinasema Azam itauza Ving'amuzi na inakusudia kutoa kiasi cha shilingi Milioni 100 kwa kila timu kwa timu zote 14 zitakazo shiriki ligi kuu msimu ujao na Mkataba huo utakuwa ni wa miaka mitano (5). Kamati ya ligi chini ya Wallace Karia na viongozi wa TFF walikutana na klabu za ligi kuu kujadili mkataba huo ambao utazipunguzia mzigo klabu ndogo ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ukata kutokana na kutegemea udhamini wa Vodacom pekeyake ambao hautoshi.




RAIS OBAMA KUJA TANZANIA MWEZI WA SITA

Habari imetangazwa kwenye BBC NEWS WORLD ikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack Obama  kuja Tanzania itakuwa ni tarehe 1/06/2013




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU