Facebook Comments Box

Monday, May 13, 2013

PICHA YA BASI LA SPORT LILIVYOPATA AJALI LEO


KONDAKTA WA GARI HILO AKIANGALIA JINSI GARI LILIVYOHARIBIKA 
BASI LA SPORT LENYE NAMBARI ZA USAJILI T 157 ASZ LINALOFANYA SAFARI ZAKE KUTOKA DAR KWENDA DODOMA LIMEANGUKA ENEO LA MWIDU MKOANI MOROGORO JANA  NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO MMOJA NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA.
MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI NA DEREVA ALIKUWA ANATAKA KUMKWEPA MTU MMOJA ALIYEKUWA ANATENGENEZA BAISKELI KANDO KANDO YA BARA BARA HIYO

BASI LA SPORT LENYE NAMBA ZA USAJILI T157 ASZ MARA BAADA YA KUANGUKA ENEO LA MWIDU MKOANI MOROGORO 




BAADHI YA MASHUHUDA ENEO LA TUKIO




MASHUHUDA WAKIANGALIA ENEO LA AJALI

ENEO LA CHASES LINAVYOONEKANA

BAADA YA KUPINDUKA

GARI HILI LILIANZA KUPOTEZA MWELEKEO HAPA KABLA HALIJAPINDUKA 


HIZI NDIO SABABU ZITAKAZO CHELEWESHA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA

Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi  huu yatachelewa  ili kutoa nafasi kwa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA),  kurekebisha matokeo mabaya ya mitihani  kidato cha nne ya mwaka jana yaliyofutwa na serikali  mwezi huu.

Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni  mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa  na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.

Alipoulizwa  juu ya suala hilo, Naibu Waziri   wa Elimu na  Mfunzo ya Ufundi  Philipo Mulugo alisema ingawa wakati huu ndio unaopaswa yatangazwe matokeo ya kidato cha sita haitafanyika hivyo hadi yatangazwe matokeo mapya ya kidato cha nne baada ya kufutwa.

Hata hivyo, akasema huenda yakatolewa  pamoja au yakafuata wakati mwingine lakini mara baada ya  kukamilisha kazi ya kurejea na kusahihisha matokeo ya kidato cha nne.

"Siyo kwamba yamechelewa kwani muda wa kujiunga na chuo ni Septemba hivyo haitawaathiri kwa hilo," alisema Mulugo.

Kuhusu hatma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo mashuleni wanaendelea na masomo ya kidato cha sita, alisema  kama kutakuwa na wanafunzi ambao wapo madarasani  shule zilizowasajili  zitakuwa hazijafuata mfumo wa elimu unavyoelekeza.

Alifafanua kuwa mfumo wa elimu kwa kidato cha nne ulibadilishwa na kwamba endapo mwanafunzi akifaulu anatakiwa kujiunga rasmi kidato cha tano  Julai na si vinginevyo.

Alisema licha ya  ucheleweshaji  wa matokeo  hali hiyo haikuwaathiri wanafunzi hao kwa kuwa ratiba ya kwenda masomoni  haijaanza kwa mujibu wa kalenda  ya shule ya serikali.

Serikali ilifuta matokeo ya kidato cha nne ya 2012 na kuiagiza Necta kuyaandaa upya kwa kutumia utaratibu wa usahihishaji na upangaji madaraja uliotumiwa mwaka  2011

Taarifa ilisema mfumo uliotumika  mwaka jana na kusababisha wanafunzi kushindwa vibaya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika.

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  mwezi  Februari mwaka huu yalionyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi walishindwa mtihani.



WAARABU WALIOKAMATWA KWA KUSHUTUMIWA KULIPUWA KANISA ARUSHA HAWANA HATIA POLISI YAWAACHIA HURU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA
 logo_tpf
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.
Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)
Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen.  Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo. Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao. Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenye na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.
Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.
Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.


Sunday, May 12, 2013

MANCIN ATIMULIWA KAZI MANCHESTER CITY



Roberto Mancini sasa si kocha mkuu tena wa Manchester City, imeelezwa.
Nafasi ya Muitaliano huyo itachukuliwa na kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini.

Bado haijajulikana rasmi ataondoka leo usiku, kesho au keshokutwa lakini inaonekana hakuna uhakika kama atakuwepo kwenye benchi kesho wakati City watakapokuwa wakiivaa Reading.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Man City zinaeleza, uamuzi wa kumtimua Mancini ulichukuliwa katika kikao cha pamoja kilichowajumuisha mabosi wawili Ferran Soriano, Txiki Begiristain na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Khaldoon Al Mubarak ikiwa ni siku moja tu baada ya City kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA.


 The Sun la Uingereza lilifanya juhudi za kumnasa Mancini ili azungumzie suala hilo lakini haikuwezekana lakini kumekuwa na taarifa amebanwa kwa kuwa anashughulikia suala la malipo ya fedha zake baada ya mkataba wake kusitishwa.
 
Ingawa yeye alisema jana amebakiza miaka minne na City, lakini taarifa zinaeleza ana miaka mitatu iliyosalia na alisaini baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England.

Jana, Mancini aliushambulia uongozi wa City kwa madai haukuonyesha juhudi za kukanusha kwamba ulikutana na wakala wa Pellegrin na aliyehusishwa kufanya naye mazungumzo ni Txiki.

Taarifa za Txiki kukutana na wakala wa Pellegrini zilianza kuchukua nafasi tokea wiki iliyopita na uongozi wa City ulionekana kuwa kimya kabisa kuhusiana na suala hilo.

Pamoja na kuipa City ubingwa wa Ligi Kuu England, Mancini aliibebesha Kombe la FA msimu huu.

Kwa kifupi, msimu huu pamoja na kushika nafasi ya pili, wamevulikuwa makombe yote waliyokuwa nayo msimu huu na uliopita.



TAMKO LA WATETEZI WA HAKI ZA BINAADAMU DHIDI YA VURUGU NA KUTISHWA KWA WANAHABARI

TAMKO LA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU DHINI YA AGENDA ZA KUVURUGA AMANI YA NCHI NA VITISHO KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI TAREHE 11 MACHI, DOUBLE VIEW HOTEL SINZA, DAR ES SALAAM 
Watetezi kutoka mikoani ambao ni wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRD-Coalition), waliokutana kwa siku tatu jijini Dar es Salaam, pamoja na kupata mafunzo adhimu ya usalama kwa watetezi yatolewayo na THRD-Coalition, pia walifanya tathmini ya hali ya usalama kwa watetezi nchini; asasi za haki za binadamu, waandishi wa habari na watu wanaojitolea katika eneo la msaada wa kutetea wenzao yaani (volunteers). Tathmini imeonyesha kwamba yapo mambo kadhaa yanayosababisha kukosekana kwa usalama kwa watetezi nchini na kupotea kwa amani.

1. Utendaji wa Vyomba Serikali na Vuguvugu la Kisiasa

Serikali ndicho chombo chenye jukumu la kuwalinda watetezi wa haki za binadamu na watu wengine waliomo ndani ya mipaka ya nchi yetu, wao na mali zao. Vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi mwao, kuteka, kutesa, kung’oa meno, na macho, kukata vidole na hata kuwarushia bomu waamini wakiwa katika maeneo ya maombi ni ishara ya dhahiri ya serikali iliyoshindwa kutimiza majukumu yake. Vitendo vya baadhi ya viongozi nchini hasa katika ngazi za Serikali za Mitaa kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwafungulia kesi za kubambikiza vimefikia kiwango cha kutovumilika. Matamko mengi yanayotolewa na viongozi wa juu wakiwamo mawaziri dhidi ya watetezi na asasi za haki za binadamu nchini yanaonyesha kuwa ni viashiria vya vitisho vya kiusalama wazi wazi kwa watetezi nchini. Pia watetezi wamekuwa wakishutumiwa kuwa ni wapinzani kwa sababu kazi zao zimekuwa zikilinganishwa na kazi za vyama vya upinzani na za kiuchochezi.
Kuwa mtetezi ni kiungo muhimu katika kuibua na kufichua maovu ili kujenga utawala unaoheshimu haki za binadamu, lakini siku zote tumejikuta tukihatarisha maisha yetu. Katika mazingira ya aina hiyo watetezi hawawezi kujiweka katika kundi salama hata kidogo, bali kwamba usalama wao umo hatarini kwa sababu kazi nyingi wanazozifanya huwalazimisha kuikosoa serikali pale inapokuwa haitimizi wajibu wake kuhusiana na kulinda haki za msingi za binadamu na haki nyinginezo stahiki. Mifano halisi ya migongano kati ya asasi na serikali ni kesi za kugombea ardhi Pugu, Loliondo, Bagamoyo na migogoro isiyoisha katika migodi mkoani Mara.

2. Wamiliki wa vyombo vya habari

Katika kudadisi ni kwa nini wanahabari wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama iligundulika kwamba wamiliki wa vyombo hawana mikakati mizuri juu ya suala zima la usalama kwa waandishi wao. Pia malipo finyu kwa wanahabari ilionekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa sababu baadhi yao hawapati malipo ya uhakika wala mikataba. Hali hiyo husababisha waandishi waishi maisha ya kubahatisha na wakati mwingine hujikuta wakishawishika kuingia katika makundi ya kisiasa ili kuanza kuvitumikia ‘vyanzo vyao’ jambo ambalo husababisha wakiuke maadili ya kazi zao na mwisho hushambuliwa na wale wanaoguswa na habari za aina hiyo. Aidha watetezi wanawasihi wamiliki kuanza kuweka mikakati ya kiusalama kwa waandishi na kuboresha mishahara kwa waandishi ili wafanye kazi kwa uhakika zaidi.

3. Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi wawe makini na matumizi ya silaha za moto na nguvu za ziada ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na ulemavu wa kudumu. Katika purukashani nyingi za kisiasa jeshi hilo limeshindwa kabisa kuonyesha kwamba linafanya kazi ya kuutumia umma wa Watanzania wote na badala yake limekuwa likichukua mwelekeo wa kuwatumikia wanasiasa au chama fulani. Aidha askari polisi wanakumbushwa kwamba wao ni sehemu ya jamii na hao wanaowatesa ni ndugu zao wa karibu wadogo zao mama zao n.k. Jeshi la Polisi litambue kuwa kazi za watetezi wa haki za binadamu ni kazi halali zinazolindwa kisheria na wanajukumu la kuweka mazingira mazuri ya watetezi kufanya kazi zao bila kutekwa, kuteswa ama kungo’lewa macho, meno, kucha n.k. Mfano halisi wa mapungufu ya jeshi hilo ni kukamatwa kwa askari hivi karibuni waliokuwa na fuvu la kichwa cha mtu mkoani Morogoro kwa lengo la kumbambika mtu kesi ya jinai. Tunaisihi Serikali na Jeshi la Polisi kuanza kutekeleza Tamko la Umoja wa Mataifa la tarehe 15 Machi 2013 linalotaka mataifa yote kutambua umuhimu na uhalali wa majukumu ya watetezi wa haki za binadamu katika kutetea haki za binadamu demokrasia, utawala wa sheria, kama nyenzo la kuhakikisha usalama wao ikiwa ni pamoja na kuheshimu uhuru wa asasi zao na kuepuka kunyanyapaa shughuli za asasi za kiraia.

4. Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu

Wanaharakati wote na watetezi wa haki za binadamu wasichukue upande wowote katika masuala ya itikadi za kisiasa kwani wao ni watu wa kati. Pia wanaharakati wasijiingize katika matumizi ya nguvu au kupambana na Jeshi la Polisi. Aidha wanaharakati wametakiwa kuwa waelimishaji wa umma na kujizuia kujiingiza katika mambo yaliyopandikizwa na watu wasioitakia mema nchi yetu kama vile udini na migogoro isiyoisha ya kugombea ardhi, maeneo ya malisho, ukabila n.k.

5. Vurugu za Udini

Kwa miaka mingi Tanzania haikuwahi kupata misukosuko ya udini kama inayotokea sasa. Lakini kwa miaka ya hivi karibuni uhasama wa kidini umezidi kushamiri. Watetezi kwa umoja wetu tunaamini Tanzania hatuna udini bali kinachoendelea ni ajenda za watu fulani kwa maslahi binafsi ama ya kifedha, kidini au kisiasa. Kwa sasa nchi inaweza kutumbukia katika machafuko ya kidini endapo viongozi wa dini zote, wanasiasa na serikali hawatachukua hatua za makusudi kuwakomesha wachache hao ambao wanataka kuondoa amani ya nchi. Katika mazingira haya pia mtetezi wa haki za binadamu hawezi kubakia salama na ndio maana tunakemea kwa nguvu zote vitendo hivi viovu.

6. Watanzania Wote Kwa Ujumla

Watanzania katika ujumla wao wameaswa kuwa makini hususani wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Wapo watu wanaochomekea ajenda zao kwa malengo wanaoyafahamu wao wenyewe na hivyo kuligawa taifa katika misingi ya udini na mambo mengine kama hayo yasiyo na tija wala manufaa kwa nchi yetu. Aidha Watanzania wameshauriwa kuirejea kazi nzuri ya kuwaunganisha ambayo iliifanya nchi hii ifahamike kama kisiwa cha amani miongoni mwa Jumuiya ya Kimataifa.

Mwisho tunaungana na watanzania wengine kulaani kitendo cha kutupa mabomu katika mikusanyiko ya watu kama ilivyotekea kule Arusha. Tunawapa pole wafiwa na majeruhi wote. Na kutaka watanzania wote bila kujadili itikadi zao kuendelea kulaani vitendo hivi vya kinyama.

TAMKO HILI LIMEANDALIWA NA WATETEZI 30 WA HAKI ZA BINADAMU TOKA MIKOA MBALIMBALI KWA NIABA YA WENZAO KATIKA AZIMIO LA KUIREJESHA NCHI HII KATIKA HALI YA AMANI NA UTULIVU



MAJESHI YA TANZANIA YAFIKA DRC CONGO

 
Umoja wa Mataifa (UN) umearifu kwamba kundi la kwanza la wanajeshi (TANZBATT 1-DRC) 100 kutoka nchini Tanzania limewasili Jumamosi hii katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika mpango wa amani wa UN wa kukabiliana na makundi ya waasi.

Tanzania inatarajia kupeleka jumla ya wanajeshi wake 1,280 katika mpango huo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa azimio la Machi 28 lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UNSC wa kuunda brigedi maalumu ya kupambana na waasi katika eneo la mashariki mwa DRC.

Msemaji wa mpango huo Felix Basse amesema Tanzania imekuwa ni nchi ya kwanza kupeleka wanajeshi wake katika eneo hilo, wanajeshi zaidi toka Malawi na Afrika Kusini wanaarajiwa kujiunga na kikosi hicho wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Wanajeshi zaidi ya 3,000 watadhibiti makundi ya waasi zaidi ya 25 katika mkoa wa Kivu pekee. Tayari kundi la waasi la M23 limeripotiwa kujiandaa ili kujibu mashambulizi yatakayoelekezwa kwao na vikosi hivyo.

Jeshi la DRC kwa muda mrefu limeshindwa kutokomeza makundi la waasi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, hata hivyo mamlaka za nchi hiyo zinatarajia mpango wa sasa wa UN huenda ukazaa matunda mema kwa usalama wa nchi hiyo.



Saturday, May 11, 2013

PICHA ZA BONANZA LA VYUO VIKUU VYA MKOA WA KILIMANJARO


Mabingwa wa Netball VETA MOSHI wakiwa katika goli la Mwenge University


Mvua zilizonyesha kabla zilileta dosari na kuchelewesha mechi za Basketball





Mabingwa Kcmc kabla ya Fainali ya Mpira wa Kikapu


Vikombe vya washindi vilivyo tolewa


Washindi wa mpira wa Kikapu KCMC wakiwa na kikombe chao

Fred Maiko Leizer akiwa na kikombe cha mshindi wa kwanza
Waandaaji wa mashindano wakitoa maelezo kabla ya Fainali ya KCMC na Baptist


Kikundi cha kucheza mziki cha TIGO kikitoa burudani

Kikundi cha sarakasi cha TIGO kikitoa burudani baada ya mashindano kuisha




MSIKILIZE MRISHO MPOTO AKIMSEMA LADY JAY DEE HADHARANI

Msanii Mrisho Mpoto ambaye pia ametoa mada katika semina iliyo andaliwa na Clouds Media ambapo alimchamba Lady Jay Dee hadharani. Msikilize hapo chini
 




JESHI LA POLISI LAKANUSHA KANISA KUPIGWA BOMU

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limetoa taarifa baada ya kuwepo uvumi kuwa Kanisa la KKKT usharika wa Kunduchi Beach, lililopo Kunduchi, Dar es Salaam limelishambuliwa kwa kupuliwa kwa bomu na kurushiana risasi.

Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amesema ukweli ni kuwa hakuna ulipuaji bomu uliofanyika katika Kanisa la KKKT Kunduchi Beach ISIPOKUWA kikosi cha Polisi kilichokuwa kinapambana na wahalifu waliokuwa karibu na Kanisa hilo kililazimika kurusha bomu la machozi ili kupambana na kuwatia mbaroni wahalifu hao.

Kova ameongeza kwa kusema waumini waliokuwepo Kanisani walishituka kwa kudhani kuwa wamevamiwa, lakini baadaye walipofahamu kinachoendelea walijitokea ili kusaidia, "Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha. Siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kova.

---
Taarifa hii imekukuliwa kutoka ITV na Radio One Stereo.
Tusubiri taarifa iliyoahidiwa kutolewa ili kuondoa tashwishi.


NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI UGOMVI WA JIDE NA RUGE


IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka  anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.


SEMINA YA 'TWEN ZETU' YA CLOUDS MEDIA GROUP ILIVYOFANYIKA DODOMA



Mbunge wa Kigoma Kaskazini CHADEMA Ndugu Zitto Kabwe akizungumza na wasanii mabalimbali wakati akitoa mada katika semina ya kampeni maalum ya “Twen Zetu” iliyofanyika kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma leo , Kampeni hiyo inazungumzia na kuhamasisha vijana kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizopo ili kujikwamua kimaisha lakini pia kuleta maendeleo kwa wasanii wenyewe na taifa kwa ujumla Watu mbalimbali wametoa mada katika semina hiyo ambao ni Patrick Ngowi, Zeno Ngowi Msanii Mrisho Mpoto na Ndugu Zitto Kabwe mwenyewe.
MRISHO MPOTO AKITOA MADA KATIKA SEMINA HIYO DODOMA HII LEO


Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba akizungumza katika semina hiyo . Mkubwa Fella kutoka TMK akizungumza katika semina hiyoDJ Elly katikati Godzilla kushoto na Izo Busness wakiwa katika semina hiyo.Benny Kinyaiya akizungumza katika semina hiyo kulia ni Babu Tale na kushoto ni Said Bonge.Millad Ayo akizungumza Anold Kayanda akitoa mawazo yake.Ibrahim Masoud na washiriki wengine wakiwa katika semina hiyoDj fetty Afande sele akiwa na wenzie, kulia ni Shilole.
Khamis Mandi B12 akichangia Mada Gerlad Hando Shafii Dauda na Loveness Love 'Diva' wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU