Facebook Comments Box

Sunday, May 12, 2013

TAMKO LA WATETEZI WA HAKI ZA BINAADAMU DHIDI YA VURUGU NA KUTISHWA KWA WANAHABARI

TAMKO LA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU DHINI YA AGENDA ZA KUVURUGA AMANI YA NCHI NA VITISHO KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI TAREHE 11 MACHI, DOUBLE VIEW HOTEL SINZA, DAR ES SALAAM 
Watetezi kutoka mikoani ambao ni wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRD-Coalition), waliokutana kwa siku tatu jijini Dar es Salaam, pamoja na kupata mafunzo adhimu ya usalama kwa watetezi yatolewayo na THRD-Coalition, pia walifanya tathmini ya hali ya usalama kwa watetezi nchini; asasi za haki za binadamu, waandishi wa habari na watu wanaojitolea katika eneo la msaada wa kutetea wenzao yaani (volunteers). Tathmini imeonyesha kwamba yapo mambo kadhaa yanayosababisha kukosekana kwa usalama kwa watetezi nchini na kupotea kwa amani.

1. Utendaji wa Vyomba Serikali na Vuguvugu la Kisiasa

Serikali ndicho chombo chenye jukumu la kuwalinda watetezi wa haki za binadamu na watu wengine waliomo ndani ya mipaka ya nchi yetu, wao na mali zao. Vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi mwao, kuteka, kutesa, kung’oa meno, na macho, kukata vidole na hata kuwarushia bomu waamini wakiwa katika maeneo ya maombi ni ishara ya dhahiri ya serikali iliyoshindwa kutimiza majukumu yake. Vitendo vya baadhi ya viongozi nchini hasa katika ngazi za Serikali za Mitaa kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwafungulia kesi za kubambikiza vimefikia kiwango cha kutovumilika. Matamko mengi yanayotolewa na viongozi wa juu wakiwamo mawaziri dhidi ya watetezi na asasi za haki za binadamu nchini yanaonyesha kuwa ni viashiria vya vitisho vya kiusalama wazi wazi kwa watetezi nchini. Pia watetezi wamekuwa wakishutumiwa kuwa ni wapinzani kwa sababu kazi zao zimekuwa zikilinganishwa na kazi za vyama vya upinzani na za kiuchochezi.
Kuwa mtetezi ni kiungo muhimu katika kuibua na kufichua maovu ili kujenga utawala unaoheshimu haki za binadamu, lakini siku zote tumejikuta tukihatarisha maisha yetu. Katika mazingira ya aina hiyo watetezi hawawezi kujiweka katika kundi salama hata kidogo, bali kwamba usalama wao umo hatarini kwa sababu kazi nyingi wanazozifanya huwalazimisha kuikosoa serikali pale inapokuwa haitimizi wajibu wake kuhusiana na kulinda haki za msingi za binadamu na haki nyinginezo stahiki. Mifano halisi ya migongano kati ya asasi na serikali ni kesi za kugombea ardhi Pugu, Loliondo, Bagamoyo na migogoro isiyoisha katika migodi mkoani Mara.

2. Wamiliki wa vyombo vya habari

Katika kudadisi ni kwa nini wanahabari wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama iligundulika kwamba wamiliki wa vyombo hawana mikakati mizuri juu ya suala zima la usalama kwa waandishi wao. Pia malipo finyu kwa wanahabari ilionekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa sababu baadhi yao hawapati malipo ya uhakika wala mikataba. Hali hiyo husababisha waandishi waishi maisha ya kubahatisha na wakati mwingine hujikuta wakishawishika kuingia katika makundi ya kisiasa ili kuanza kuvitumikia ‘vyanzo vyao’ jambo ambalo husababisha wakiuke maadili ya kazi zao na mwisho hushambuliwa na wale wanaoguswa na habari za aina hiyo. Aidha watetezi wanawasihi wamiliki kuanza kuweka mikakati ya kiusalama kwa waandishi na kuboresha mishahara kwa waandishi ili wafanye kazi kwa uhakika zaidi.

3. Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi wawe makini na matumizi ya silaha za moto na nguvu za ziada ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na ulemavu wa kudumu. Katika purukashani nyingi za kisiasa jeshi hilo limeshindwa kabisa kuonyesha kwamba linafanya kazi ya kuutumia umma wa Watanzania wote na badala yake limekuwa likichukua mwelekeo wa kuwatumikia wanasiasa au chama fulani. Aidha askari polisi wanakumbushwa kwamba wao ni sehemu ya jamii na hao wanaowatesa ni ndugu zao wa karibu wadogo zao mama zao n.k. Jeshi la Polisi litambue kuwa kazi za watetezi wa haki za binadamu ni kazi halali zinazolindwa kisheria na wanajukumu la kuweka mazingira mazuri ya watetezi kufanya kazi zao bila kutekwa, kuteswa ama kungo’lewa macho, meno, kucha n.k. Mfano halisi wa mapungufu ya jeshi hilo ni kukamatwa kwa askari hivi karibuni waliokuwa na fuvu la kichwa cha mtu mkoani Morogoro kwa lengo la kumbambika mtu kesi ya jinai. Tunaisihi Serikali na Jeshi la Polisi kuanza kutekeleza Tamko la Umoja wa Mataifa la tarehe 15 Machi 2013 linalotaka mataifa yote kutambua umuhimu na uhalali wa majukumu ya watetezi wa haki za binadamu katika kutetea haki za binadamu demokrasia, utawala wa sheria, kama nyenzo la kuhakikisha usalama wao ikiwa ni pamoja na kuheshimu uhuru wa asasi zao na kuepuka kunyanyapaa shughuli za asasi za kiraia.

4. Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu

Wanaharakati wote na watetezi wa haki za binadamu wasichukue upande wowote katika masuala ya itikadi za kisiasa kwani wao ni watu wa kati. Pia wanaharakati wasijiingize katika matumizi ya nguvu au kupambana na Jeshi la Polisi. Aidha wanaharakati wametakiwa kuwa waelimishaji wa umma na kujizuia kujiingiza katika mambo yaliyopandikizwa na watu wasioitakia mema nchi yetu kama vile udini na migogoro isiyoisha ya kugombea ardhi, maeneo ya malisho, ukabila n.k.

5. Vurugu za Udini

Kwa miaka mingi Tanzania haikuwahi kupata misukosuko ya udini kama inayotokea sasa. Lakini kwa miaka ya hivi karibuni uhasama wa kidini umezidi kushamiri. Watetezi kwa umoja wetu tunaamini Tanzania hatuna udini bali kinachoendelea ni ajenda za watu fulani kwa maslahi binafsi ama ya kifedha, kidini au kisiasa. Kwa sasa nchi inaweza kutumbukia katika machafuko ya kidini endapo viongozi wa dini zote, wanasiasa na serikali hawatachukua hatua za makusudi kuwakomesha wachache hao ambao wanataka kuondoa amani ya nchi. Katika mazingira haya pia mtetezi wa haki za binadamu hawezi kubakia salama na ndio maana tunakemea kwa nguvu zote vitendo hivi viovu.

6. Watanzania Wote Kwa Ujumla

Watanzania katika ujumla wao wameaswa kuwa makini hususani wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Wapo watu wanaochomekea ajenda zao kwa malengo wanaoyafahamu wao wenyewe na hivyo kuligawa taifa katika misingi ya udini na mambo mengine kama hayo yasiyo na tija wala manufaa kwa nchi yetu. Aidha Watanzania wameshauriwa kuirejea kazi nzuri ya kuwaunganisha ambayo iliifanya nchi hii ifahamike kama kisiwa cha amani miongoni mwa Jumuiya ya Kimataifa.

Mwisho tunaungana na watanzania wengine kulaani kitendo cha kutupa mabomu katika mikusanyiko ya watu kama ilivyotekea kule Arusha. Tunawapa pole wafiwa na majeruhi wote. Na kutaka watanzania wote bila kujadili itikadi zao kuendelea kulaani vitendo hivi vya kinyama.

TAMKO HILI LIMEANDALIWA NA WATETEZI 30 WA HAKI ZA BINADAMU TOKA MIKOA MBALIMBALI KWA NIABA YA WENZAO KATIKA AZIMIO LA KUIREJESHA NCHI HII KATIKA HALI YA AMANI NA UTULIVU



MAJESHI YA TANZANIA YAFIKA DRC CONGO

 
Umoja wa Mataifa (UN) umearifu kwamba kundi la kwanza la wanajeshi (TANZBATT 1-DRC) 100 kutoka nchini Tanzania limewasili Jumamosi hii katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika mpango wa amani wa UN wa kukabiliana na makundi ya waasi.

Tanzania inatarajia kupeleka jumla ya wanajeshi wake 1,280 katika mpango huo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa azimio la Machi 28 lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UNSC wa kuunda brigedi maalumu ya kupambana na waasi katika eneo la mashariki mwa DRC.

Msemaji wa mpango huo Felix Basse amesema Tanzania imekuwa ni nchi ya kwanza kupeleka wanajeshi wake katika eneo hilo, wanajeshi zaidi toka Malawi na Afrika Kusini wanaarajiwa kujiunga na kikosi hicho wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Wanajeshi zaidi ya 3,000 watadhibiti makundi ya waasi zaidi ya 25 katika mkoa wa Kivu pekee. Tayari kundi la waasi la M23 limeripotiwa kujiandaa ili kujibu mashambulizi yatakayoelekezwa kwao na vikosi hivyo.

Jeshi la DRC kwa muda mrefu limeshindwa kutokomeza makundi la waasi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, hata hivyo mamlaka za nchi hiyo zinatarajia mpango wa sasa wa UN huenda ukazaa matunda mema kwa usalama wa nchi hiyo.



Saturday, May 11, 2013

PICHA ZA BONANZA LA VYUO VIKUU VYA MKOA WA KILIMANJARO


Mabingwa wa Netball VETA MOSHI wakiwa katika goli la Mwenge University


Mvua zilizonyesha kabla zilileta dosari na kuchelewesha mechi za Basketball





Mabingwa Kcmc kabla ya Fainali ya Mpira wa Kikapu


Vikombe vya washindi vilivyo tolewa


Washindi wa mpira wa Kikapu KCMC wakiwa na kikombe chao

Fred Maiko Leizer akiwa na kikombe cha mshindi wa kwanza
Waandaaji wa mashindano wakitoa maelezo kabla ya Fainali ya KCMC na Baptist


Kikundi cha kucheza mziki cha TIGO kikitoa burudani

Kikundi cha sarakasi cha TIGO kikitoa burudani baada ya mashindano kuisha




MSIKILIZE MRISHO MPOTO AKIMSEMA LADY JAY DEE HADHARANI

Msanii Mrisho Mpoto ambaye pia ametoa mada katika semina iliyo andaliwa na Clouds Media ambapo alimchamba Lady Jay Dee hadharani. Msikilize hapo chini
 




JESHI LA POLISI LAKANUSHA KANISA KUPIGWA BOMU

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limetoa taarifa baada ya kuwepo uvumi kuwa Kanisa la KKKT usharika wa Kunduchi Beach, lililopo Kunduchi, Dar es Salaam limelishambuliwa kwa kupuliwa kwa bomu na kurushiana risasi.

Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amesema ukweli ni kuwa hakuna ulipuaji bomu uliofanyika katika Kanisa la KKKT Kunduchi Beach ISIPOKUWA kikosi cha Polisi kilichokuwa kinapambana na wahalifu waliokuwa karibu na Kanisa hilo kililazimika kurusha bomu la machozi ili kupambana na kuwatia mbaroni wahalifu hao.

Kova ameongeza kwa kusema waumini waliokuwepo Kanisani walishituka kwa kudhani kuwa wamevamiwa, lakini baadaye walipofahamu kinachoendelea walijitokea ili kusaidia, "Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha. Siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kova.

---
Taarifa hii imekukuliwa kutoka ITV na Radio One Stereo.
Tusubiri taarifa iliyoahidiwa kutolewa ili kuondoa tashwishi.


NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI UGOMVI WA JIDE NA RUGE


IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka  anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.


SEMINA YA 'TWEN ZETU' YA CLOUDS MEDIA GROUP ILIVYOFANYIKA DODOMA



Mbunge wa Kigoma Kaskazini CHADEMA Ndugu Zitto Kabwe akizungumza na wasanii mabalimbali wakati akitoa mada katika semina ya kampeni maalum ya “Twen Zetu” iliyofanyika kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma leo , Kampeni hiyo inazungumzia na kuhamasisha vijana kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizopo ili kujikwamua kimaisha lakini pia kuleta maendeleo kwa wasanii wenyewe na taifa kwa ujumla Watu mbalimbali wametoa mada katika semina hiyo ambao ni Patrick Ngowi, Zeno Ngowi Msanii Mrisho Mpoto na Ndugu Zitto Kabwe mwenyewe.
MRISHO MPOTO AKITOA MADA KATIKA SEMINA HIYO DODOMA HII LEO


Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba akizungumza katika semina hiyo . Mkubwa Fella kutoka TMK akizungumza katika semina hiyoDJ Elly katikati Godzilla kushoto na Izo Busness wakiwa katika semina hiyo.Benny Kinyaiya akizungumza katika semina hiyo kulia ni Babu Tale na kushoto ni Said Bonge.Millad Ayo akizungumza Anold Kayanda akitoa mawazo yake.Ibrahim Masoud na washiriki wengine wakiwa katika semina hiyoDj fetty Afande sele akiwa na wenzie, kulia ni Shilole.
Khamis Mandi B12 akichangia Mada Gerlad Hando Shafii Dauda na Loveness Love 'Diva' wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo


Friday, May 10, 2013

TAARIFA MPYA YA WIZARA YA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo.

Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba

KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10/05/2013


HII NDIO BARUA YA FIFA ILIYOMLETEA MATATIZO SHAFFIH DAUDA

Mtandao wa shaffihdauda umeripoti kwa kuiweka barua halisi ya FIFA kwa TFF. Kitu ambacho TFF wamemjia juu Shaffih Dauda na kumpa siku saba aeleze ameipata wapi barua hii ya kiofisi.

MGOMO WA DALADALA WAITIKISA IRINGA LEO

Huko mjini Iringa, daladala za Manispaa hiyo zimegoma kufanya biashara leo kutokana na  kile  wamiliki na madereva  wanachodai ni kuchoshwa na manyanyaso ya Afisa mpya wa SUMATRA wa mkoa wa Iringa.

Francis Godwin katika blog yake anasema kiini cha mgomo huo ni kinatokana na kuchukizwa na uamuzi  wa SUMATRA mkoa wa Iringa kufuta stendi ya Posta pamoja na kuzuia daladala kukaa kwa muda katika eneo la stendi ya daladala ya Miyomboni maeneo ambayo walikuwa wakikaa siku zote, hivyo, madereva  hao wamesema hawatafanya kazi hadi hapo SUMATRA Iringa itakapofuta maagizo yake hayo.
Picture
Picture
Picture



KIBONZO: ANGALIA WACHEZAJI WA MAN U WAKIMLILIA FERGUSON NA BABA WA MWAKA

Kibonzo cha picha kinaco onesha wachezaji waMan U wakimlilia SAF
Huyu amepewa tuzo ya ubaba wa mwaka


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU