![]() |
| Huu ni ushahidi wa picha ukimuonesha Luis Suarez akimng`ata Ivanovic leo kwenye mechi ya Liverpool dhidi ya Chelsea ambapo timu hizo zilitoka droo ya magoli mawili kwa mawili |
Sunday, April 21, 2013
HUU NDIO USHAHIDI WA SUAREZ KUMNG'ATA IVANOVIC UWANJANI LEO
Saturday, April 20, 2013
DARASA LA SABA SASA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU
| Jengo la Chuo Kikuu Dodoma(Udom) moja ya vyuo vitakavyo tumika katika utaratibu huo mpya |
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo
2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la
saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi
ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na
Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani
mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu
kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya
kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu,
lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha
mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama
‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa
vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya
Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk
Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa
habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo
bila tatizo.”
Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni
75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja
E ni 0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa
kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa
kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha
kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.
SOURSE: MWANANCHI
SOURSE: MWANANCHI
MWALIMU ATUHUMIWA KUMUAMBUKIZA VVU MWANAFUNZI
Na Gordon Kalulunga - Mbeya
IMEELEZWA kuwa mwanafunzi wa
Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Vanessa (jina
linahifadhiwa) iliyopo Mkoani Mbeya aliyekuwa na mahusiano ya kingono
mwalimu wake aitwaye John Mapunda ameambukizwa virusi vya UKIMWI
(VVU).
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka (17) wakati anahusiana kingono na mwalimu wake alikuwa anajiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2012 lakini hakuweza kufanya mtihani huo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, Mwalimu Mapunda alikuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi wake tangu mwaka 2011 akiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo na wakati mwingine mwanafunzi huyo alikuwa analala nyumbani kwa Mwalimu wake huyo kwa siku kadhaa, kama mkewe.
Vyanzo vya blogu ya Kalulunga vimeeleza kuwa mwalimu huyo ambaye anafundisha somo la jiografia alifanikiwa kumtongoza na kumrubuni mwanafunzi huyo tangu akiwa kidato cha kwanza kwa kumwongezea maksi kila mtihani unapofanyika.
Baada ya wazazi wa mtoto kufuatilia nyendo za mtoto baada ya kupotea kwa siku tatu mfululizo, wazazi walitoa taarifa Central Polisi Mbeya ambapo Polisi walianza kufuatilia.
Siku tatu baadaye, mwanafunzi huyo wa kike alirejea nyumbani kwao. Wazazi walimpeleka Polisi. Alipobanwa, aliwaambia Polisi kuwa ametoka kwa mwalimu Mapunda na kukiri kufanya naye ngono bila kinga.
Habari za kiuchunguzi zimeeleza kuwa Polisi na wazazi waliamua kwenda kumpima afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambapo majibu yalionesha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameambukizwa VVU.
Uchunguzi umebaini kuwa, jalada la uchunguzi wa polisi lipo chini ya askari anayefahamika kwa jina la Andrea Mwambembe na askari mwingine aliyefahamika kwa jina la Mwashiwuya.
Lakini katika hali ya kustaajabisha, inadaiwa askari hao walipokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa kumfuata mwalimu Mapunda kazini kwake, walipofika, Mkurungenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Shukran Mwasajobe alimshitua Mwl. Mapunda na kusababisha kutorokea wilayani Chunya.
Siku iliyofuata Shukran anadaiwa kumfuata Afande Justine Kayombe na Afande mwanaume lakini mwenye simu iliyosajiliwa kwa jina la Judith Juma, ili kumalizazana na tatizo hilo.
Katika hali ya kushangaza, Shukran baada ya kukutana na askari hao na kuweka mambo sawa, alionekana akimfokea askari Sponsor Millinga na kwenda kumlalamikia kuwa anatafuta rushwa kwake.
Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa mwalimu Mapunda hajakamatwa kwa kosa lolote na mwanafunzi aliyebakwa ameshindwa kufanya mtihani huku wazazi wakilalamika.
Kwa sasa mwalimu Mapunda, Shukran na Afande Justine Kayombe wanadaiwa kuwa maswahiba na mara kadhaa wanaonekana wakiwa pamoja katika hoteli ya Moon Dust iliyopo kata ya Ruanda eneo la Soweto Mkoani Mbeya.
Taarifa kutoka Ofisi za Ukaguzi kanda zinaonyesha kuwa mwalimu huyo amekuwa na kashfa ya ngono tanga akiwa katika Shule ya Montifot Sekondari iliyopo Usangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya, na alifukuzwa hapo kabla ya mwakza 2008 baada ya kutuhumiwa kosa kama hilo, la kufanya mapenzi na mwanafunzi.
Taarifa kutoka kwenye familia ya mwalimu huyo zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2007, muda mfupi kabla hajafukuzwa kazi katika Shule ya Montifot, mwalimu huyo alianza kukorofishana na mkewe katika suala la ufuska na walipohamia jijini Mbeya, mkewe alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kike ndani na hivyo ndoa yao kuvunjika papo hapo, huku mkewe akirejea nyumbani kwao mkoani Tanga.
Ili kuzima sakata hilo, Mkurugenzi wa shule hiyo anadaiwa kutaka kumfukuza Mkuu wa shule hiyo ambaye anaonekana kuhoji mara kadhaa juu ya sakata hilo ili hali yeye tayari anadhani amelimaliza polisi.

Friday, April 19, 2013
KESI YA PONDA YAZIDI KUPIGWA DANADANA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imeahirisha kutoa hukumu
ya kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. milioni
59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na wenzake 49
kwa maelezo kuwa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo,Victoria Nongwa
hayupo.
Hakimu Mkazi Alocye Katemana ndiye aliyeairisha kesi hiyo ambapo alianza kwa kusema kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kutolewa hukumu, lakini hukumu hiyo haitatolewa kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo na wala hajatuma hukumu ya kesi hiyo kwa uongozi wa mahakama.
“Kwa sababu hiyo naairisha kesi hii hadi Mei 2 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na Mei 9 mwaka huu, itakuja kwa ajili ya kutolewa hukumu...”
Alisema Hakimu Katemana na kuamuru mshitakiwa wa kwanza na watano (Ponda na Mukadam Swalehe) kurudishwa rumande kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Dk Elizer Feleshi hajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana.
Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika mahakamani hapo tangu saa moja asubuhi, alishuhudia kundi la watu zaidi ya mia moja wakiwa wamesimama nje ya uzio wa mahakama hiyo karibu na ofisi ya Maktaba ya Taifa tayari wakisubiri kuingia ndani ya lango la mahakama hiyo kwa ajili ya kukaguliwa kwa vifaa maalum na wanausalama.
Watu hao waliruhusiwa kuingia ndani ya viwanja vya mahakama, lakini ni wachache tu ndiyo walioruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha wazi Na.2 cha mahakama hiyo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.
Baada ya kuarishwa kwa kesi hiyo, askari magreza waliondoka na msafara wa magari yao ambao ulikuwa ukiongozwa na askari polisi waliokuwa wamevalia na wasiovalia sare za jeshi.
Wakati wakitoka ndani ya viwanja hivyo tayari kuelekea katika gereza la Segerea anapoishi Ponda na Mukadam kwa sasa, wafuasi hao walipaza sauti huku wakimpungia mkono Ponda wakisema ‘Takbir!’ na kuitikia ‘Allahu Akbar.’

HAWA NDIO WASHUKIWA WA ULIPUWAJI WA MABOMU YA BOSTON MAREKANI NA VIDEO YA HARAKATI ZAO
| Mwenye kofia nyeupe hapo ni mmoja wa hao washukiwa wawili. |
| Huyu ni mshukiwa mwingine na hapa ilikua kabla bomu halijalipuka, hii picha inawaonyesha wakielekea kwenye sehemu ambayo mbio ndio zinamalizikia ambako ndiko kulikolipuka. |
.
| Huyu ndio yule mshukiwa namba 1 anaeonekana kwenye picha ya kwanza hapo juu. |
| mshukiwa namba 1 |
.
| Hapa ilikua baada ya bomu kulipuka ambapo mshukiwa namba 1 mwenye kofia nyeupe hapo kushoto ndio alikua anaondoka mdogo mdogo |
Thursday, April 18, 2013
BI KIDUDE AZIKWA NA UMATI WA WATU ZANZIBAR
![]() |
| Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu bi Kidude, Zanzibar |
![]() |
| Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi) |
![]() |
| Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude |
![]() |
| Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude |
![]() |
| Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani |
Subscribe to:
Posts (Atom)