Hii ni picha ya Karuta Primary School ambayo ilijengwa hapo na wamisionari wa enzi hizo na ilikuwa ikijulikana kama Ujiji White Father Central School ikiwa na darasa la tano mpaka la nane.Na hapa ndipo aliposoma nguli wa mpira tanzania Sunday Manara Computer.
Tuesday, September 4, 2012
Monday, September 3, 2012
BASI LA KAMPUNI YA SHAKILA LAPATA AJALI TABORA
Watu tisa wamejeruhiwa huku watatu wakiwa
katika hali mbaya na kupewa huduma ya kwanza katika kituo cha afya cha
Mtakatifu Philipo na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa Tabora
Kitete kwa matibabu zaidi,baada ya basi la kampuni ya Shakila lenye
namba za usajili T 539 AMY, lililokuwa likitoka wilayani Sikonge
kuelekea mjini Tabora na kuanguka eneo la Kizigo manispaa ya Tabora.
PICHA ZA DIAMONDS AKIWA MAREKANI
Friday, August 31, 2012
USAJILI SIKU YA MWISHO NA WALIO KAMILISHA USAJILI
![]() |
| Hatimaye Dimitar Berbatov amehamia rasmi Fulham kutoka Manchester United kwa ada ya £5million |
![]() |
| Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Douglas Maicon amesajiliwa kutoka Inter Milan kwenda Manchester City |
![]() |
| Charlie Adam amejiunga na Stoke City City akitokea Liverpool kwa ada ya £4MILLION |
![]() |
| Andy Carroll amejiunga na West Ham kwa mkopo wa mwaka mzima |
![]() |
| Rafael Van Der Vaart amejiunga na Schalke akitokea Tottenham Hotspur |
![]() |
| Pablo Hernandez amejiunga na Swansea City akitokea Valencia ya Spain |
![]() |
| Scott Sinclair amekamilisha uhamisho wake kutoka Swansea na kuhamia kwa mabingwa wa England Man City |
![]() |
| Nicklas Bendtner amehama Arsenal na kwenda kujiunga na Juventus ya Italia |
NI KWELI MICHAEL ESSIEN ANAENDA ARSENAL?
Kuna uvumi umezagaa ndani ya jiji la London kuwa Michael Essien anahitajika Arsenal kwa mkopo. Yamebaki masaa kadhaa ili kumalizika muda wa usajili. Tusubiri hadi mwisho tuone jembe hili litaenda kwa washika bunduki.
HATIMAE TFF WATOA RATIBA YA LIGI
LIGI KUU TANZANIA BARA 2012/2013
Michuano
ya Ligi Kuu kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013
itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja
tofauti.
Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).
Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.
WACHEZAJI 17 WAPINGWA KWENYE USAJILI
Klabu mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.
Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.
Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.
Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.
Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.
Vilevile Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.
Nayo Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.
Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.

Thursday, August 30, 2012
ANGALIA MAKUNDI YA UEFA HAPA
Angalia makundi ya UEFA (klabu bingwa barani ulaya) hapa.
| GROUP A |
GROUP B |
GROUP C |
GROUP D |
| Porto | Arsenal | AC Milan | Real Madrid |
| Dynamo Kiev | Schalke | Zenit St Petersburg | Manchester City |
| Paris Saint-Germain | Olympiakos | Anderlecht | Ajax |
| Dinamo Zagreb | Montpellier | Malaga | Borussia Dortmund |
| GROUP E |
GROUP F |
GROUP G |
GROUP H |
| Chelsea | Bayern Munich | Barcelona | Manchester United |
| Shakhtar Donetsk | Valencia | Benfica | Braga |
| Juventus | Lille | Spartak Moscow | Galatasaray |
| Nordsjaelland | BATE Borisov | Celtic | Cluj |
MBUYU TWITE ATUA DAR
![]() |
| Mbuyu Twite akiongozwa na viongozi wa Yanga kuelekea kwenye gari |
![]() |
| Hawa ni washabiki wa Yanga waliofika kumpokea Mbuyu Twite |
![]() |
| Mbuyu Twite akiwa amevaa Jezi namba 4 Iliyoandikwa Rage akihojiwa na waandishi wa habari |
![]() |
| Mmoja wa washabiki wa Yanga akiwa na jezi namba 4 iliyo andikwa Rage |
Amesema anavutiwa na mazingira yake ya kazi na ushirikiano anaopata kwa viongozi wa mabingwa hao wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati.
Subscribe to:
Posts (Atom)