Wachezaji
waliozawadiwa kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho
kulia) na katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile
Osiah(mwisho kushoto).
Mkurugenzi
wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya
wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.
Tanzania
waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia
amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa
wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.
Katika
pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni
Shelda Boniface na mvulana ni Athanas Mdamu na pia amempongeza
mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .
Katika
mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande
wa wasichana magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne ,
mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa
wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na
kuondoka na mpira kila mmoja.
Kabla
ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya
michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili
kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.
Akiongea
kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua
mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa ,
amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve
na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na DRFA
Kocha
wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea
wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars.
Naodha
wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17
Stumai Abdalah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo nchini Leonard Thadeo.
Kaptain
ya timu ya wasichana Stumai Akikabidhi cheti cha kushinda kwa
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo.
Mchezaji
wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dolla 10,000
iliyokabithiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka
washindi wa michuano ya Airtel Rising stars Afrika.
Chanzo: Michuzi
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog