Muandamanaji akidhibitiwa na mlinzi |
Muandamanaji huyu alimkaribia ila alidhibitiwa vilivyoRaisi wa Urusi bwana Putin alipata bonge la mshangao wakati wa ziara yake ya Ujerumani baada ya waandamanaji kujitokeza. katika waandamanaji hao kulikuwa na wanawake watatu ambao walikuwa vifua wazi ambao walijitokeza nao mbele na kutaka kwenda kumkumbatia rais huyo.Bwana Putin alikuwa ameenda katika uzinduzi wa Hanover Messe industrial trade show yeye na mwenyeji wake Chancellor Angela Merkel ndipo walipojitokeza waandamanaji hao wakipinga sera na sheria za nchi yake juu ya mambo mbalimbali ambayo wao wanaona sio sawaAkiliongelea hilo bwana Putin anasema alilitegemea ila anasema walinzi wa kijerumani walikuwa wakali sana kwa wamama hao kiasi cha kuwala wote chini kwa nguvu na muda mfupi kiasi kwamba hakusikia vizuri maneno waliyo yasema ila anasema alifurahishwa nao.Pamoja na hayo kulikuwa pia na mabango kwenye mitaa hiyo ya miji ya Ujerumani. |
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog