Facebook Comments Box

Saturday, November 8, 2014

HATIMAYE SITTI MTEMVU AACHIA TAJI

Katika hali isiyotarajiwa mlimbwende alichukua taji la urembo la Tanzania mwanadada Sitti Mtemvu ameachia taji hilo. Katika barua ambayo amewaandikia wandaaji wa shindano hilo ameeleza jinsi anavyo andamwa na watu mbalimbali juu ya umri wake.

Barua aliyo andika ni hiyo hapo chini


Friday, November 7, 2014

WHATSAPP YAWAUMBUA WAONGO

Kuanzia juzi longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika utakuwa unaongopa mchana kweupe.

Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa
Tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa
Tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea maelezo ya kina ya ujumbe huo  (Pressing and holding an individual message shows the Message Info option) Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa

Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa

Whatsapp haijatoa sababu za kufanya mabadiliko hayo ambayo yamewakera baadhi ya watumiaji.

Kuanzia juzi huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook- itakuwa ikionesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.

Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao.mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.


Thursday, November 6, 2014

RAIS AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU WA KUU WA WIZARA

Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja, uteuzi uliomuondoa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo.

Pallangyo sasa anakua Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, nafasi ambayo inatafsriwa kuwa adhabu, siku chache baada ya vyombo vya habari ikiwamo FikraPevu kuibua kashfa ya uhaba wa dawa katika hospitali kubwa za serikali. Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.

Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa ni pamoja na Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuchukua nafasi ya Pallangyo.

Katika uteuzi huo Dkt. Yohana Budeba anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.

Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje(EPZA).

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba amepanda na kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro anahamishiwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
wa Mwanza. Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA kuchukua nafasi ya Dkt. Meru.

Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam. Wakati huohuo, Rais Kikwete amefanya
uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine. Mabadiliko hayo yanampumzisha

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Fabian Massawe na kuwahamisha wakuu wa mikoa ya Arusha Magessa Mulongo na Fatma Mwasa wa Tabora. Taarifa ya Balozi Sefue inawataja Wakuu
wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John
Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho,
Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali
Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwavituo vya kazi ni Bwana  Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza
kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila
anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist
Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt.
Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa,
Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa. Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa
Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi. Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya
kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.


Wednesday, November 5, 2014

REAL MADRID YAINGIA HATUA YA 16 KWA KUIFUNGA LIVERPOOL

Timu ya R.Madrid jana usiku ilipata ushindi kiduchu kwa kuichapa Liverpool ya England katika michuano ya kuitafuta Klabu Bingwa wa Ulaya. Wenyeji walipata bao la kuongoza na la ushindi katika dakika ya 27 ya mchezo kupitia kwa Kareem Benzema.
 Uwanja wa Santiago Bernabeu ulipofanyika mchezo huo kati ya wenyeji R.Madrid vs Liverpool.
 Kareem Benzemaa akishangilia bao lake lililoipa ushindi Real Madrid dhidi ya Liverpool.
Wachezaji wa Real Madrid wakimpongeza mfungaji wa bao pekee la mchezo huo, Kareem Benzemaa.
 Kareem Benzemaa katikati ya Kolo Habib Toure na Martin Skrtel.



Tuesday, November 4, 2014

MRISHO NGASSA NDIO MFUNGAJI BORA AFRIKA

Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa amepata zali Afrika, baada ya kumaliza kinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake kuaga mashindano hayo katika mzunguko wa pili. Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.

Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya wakibebwa na bao la ugenini kutokana na matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa Algeria na sare mabao 2-2 mchezo uliochezwa Kinshasa.

Ngassa aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2. 

Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huwa haitoa zawadi.


HISTORIA FUPI YA MAREHEM JAFAR SIRAJ

Kabla ya kuwepo MuM alikuwa ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu cha Kiislamu Ubungo Islamic Teacher's College ambako alihitimu mwaka 2004 na kisha akasomesha Msamala Muslim Songea na baadae Matangini Islamic Dar, akajiunga na
Chuo cha Waislamu Morogoro wakiwa ndio Batch ya mwanzo 2005. Baada ya kuhitimu alichaguliwa kuwa Mhadhiri Msaidizi na mwaka mmoja baadae alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamili na kurejea MuM ambako amekuwa akifanya kazi mpaka mauti yalipomkuta.

Bro. Alianza kupata mtihani wa maradhi mwaka 2011 na 2012 au 13 aligundulika kuwa na Maji kwenye mapafu waislamu wakachukuwa  jukumu la kumpeleka India kwa matibabu akafanyiwa upasuaji na tatizo likapungua alirejea Alhamdulillaah ingawa alionekana wazi kuwa tayari amedhoofika, hakuwa Siraji yule handsome tuliyekuwa tukimjua.

Bro. Katika uhai wake ukiacha kwamba alikuwa superbright kitaaluma na kihoja na aliyekuwa na khofu ya dhati kwa Mola wake alikuwa role model, and very inspiring, fasaha na mtulivu sana asiye na papara katika mambo yake na huu ni sehemu ya urithi aliyotuachia.

Bro. Siraji alikuwa mtu huru na anayenyoosha maneno alipokuwa akisimamia haki, Kipindi cha mwangaza wa jamii Radio Iman na wasikizaji wake watashuhudia kwa hili na watasikitika sana kipindi hiki kumkosa huyu Akhy.

"Hao ni umma umekwishapita, wao wana malipo yao nanyi mna malipo yenu wala hamtoulizwa wao wamefanya nini (Bali mtaulizwa ninyi mmefanya nini) 2:141

Bro. Siraji ameacha mke na  watoto wawili wa kiume. Tunaamini wajibu wake kwa jamii ya waislamu na watanzania kwa jumla ameutekeleza kikamilifu na hivyo anastahiki akapumzike.

Sisi sote ni wa Allaah na kwake ndio Marejeo. Allaah amsamehe madhambi yake amrehemu na ampe makazi mazuuri peponi.


Sunday, November 2, 2014

MLIPUKO WA KITU KINACHODHANIWA KUWA BOMU WAUA MMOJA KISHAPU



Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45 hrs katika center ya Muhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu.

Gari no T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, Muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) msukuma wa Muhunze.

Wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid 21-23, mwangaza wa Ngara ambaye ni
familia ya mwenye gari.

Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.

Pia mfanyabiashara Donard s/o Nzugala Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.

Wengine ni Maganga s/o Piusi (14 ), msukuma,mkulima wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto, mgongoni na mkono wa kushoto.

Seni s/o Edward (25 ), msukuma mkulima wa Lubaga Kishapu amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa.



SIMBA YAENDELEZA SARE: PHIRI ABAKIZA MECHI MOJA KUTIMULIWA


SIMBA SC imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya jana.

Hii inakuwa ni mechi ya 12 kwa Simba bila ushindi ukijumlisha na mechi sita za mwisho za msimu uliopita. Swala hili la kutoa suluhu limepelekea Simba kumpa kocha wa Phiri mechi tatu za mwisho na akihitajika kushinda mechi mbili. Jana wametoa suluhu mechi ya kwanza na zimebaki mbili, Hii ina maana akitoa suluhu yoyote au kufungwa ndio utakuwa mwisho wa Kocha huyo ambae ana historia ya kuja Simba na kufundisha mara kwa mara nusu msimu ikifika  msimu mwingine anaaga kuwa ana matatizo ya kifamilia na harudi tena.

Suluhu hiyo inawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC imefikisha pointi 6 jana.Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki wa kimataifa wa Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi.
 
Hali hiyo iliwafanya vinara wa hao wa Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika ya 58, mfungaji Mussa Hassan Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia, William Lucian ‘Gallas’ kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.

VIKOSI VILIKUWA HIVI:
 
Mtibwa Sugar: Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka na Ally Shomary.

Simba SC: Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Awadh Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla na Emmanuel Okwi/Uhuru Suleiman dk75.


Saturday, November 1, 2014

PICHA YA LEO: KIONGOZI WA YANGA AKIKAGUA UDONGO WA UWANJA

Yanga leo inapambana na timu ya Kagera Sugar chini ni picha ya mmoja wa viongozi wa Yanga akifukia kitu katika uwanja wa kaitaba jana.



Friday, October 31, 2014

SHEIKH SORAGA UNAJICHANGANYA NA UNAPOTOSHA

Sheikh Fadhil S. Soraga
Hivi karibuni kumekuwa na barua ya katibu wa mufti wa zanzibar Sheikh Fadhil S. Soraga kilichonichanganya ni Katibu huyo kuto ikanusha barua hiyo ambayo haina kichwa cha juu cha barua na anuani (Headed letter). Ukiiangalia utaiona imekaa kama tangazo na chini ina saini ya sheikh huyo.Nadhani wengi wetu hatuuijui saini ya Sheikh Soraga na huenda watu wameitumia vibaya ili kumdhalilisha. Kingine kinacho nichanganya ni kuwa kikao kilifanyika tarehe 18 mwezi wa 8 kwanini leo ndio iwekwe kwenye mitandao ya kijamii na iwe gumzo?

Nahisi kuna watu wanataka kuwavuruga waislam wa Zanzibar au kuanzisha mjadala huu ili baadae walipitishe maana ni dhahiri kuwa ile kuswali kufuata uislam na idadi ya waislam wa Zanzibar ina waumiza.

Labda tuzungumze upande wa pili huenda ni kweli Sheikh Soraga ameandika maana hawa BAKWATA kutumiwa ni raisi sana (Naomba wanisamehe kwa kauli hii lakini ndio ukweli) watakuwa wameambiwa na mtu mmoja mwenye hela ambae huwapa vijisenti sasa wamelileta hili. Wakasahau kuwa ikiishakuhusu swala atawaambia hata adhana na kwenda msikitini pia inamkera maana inaonesha haridhiki na uislam kabisa. Inakuwaje asichukizwe na adhana ambayo hutolewa kwa nguvu na kuna wakati mtu hugeuka kulia na kushoto ili kutawanya sauti. Aje achukizwe na nyiradi ambazo husemwa na imam mara moja tu na wengine kufuatiliza kwa mdomo.

Naomba BAKWATA wawe wanafikiria kidogo kabla ya kuamua jambo. Kwani huko kuna matamasha ya filamu na mziki ambayo yanakesha usiku kucha na sijasikia malalamiko. Mi nina uhakika wameanza hapo ila watakuja mpaka kwenye adhana.

Tangazo/Barua ya katibu wa mufti Zanzibar



DAR ES SALAAM MPAKA ZANZIBAR SASA KWA BARABARA


Picha(maktaba)

BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.

Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara na Unguja, kwa upande wa Zanzibar.

Umbali kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni kilometa 73.43, sawa na maili 45.62 hivyo kuwapo kwa mradi huo ni jambo linalowezekana, kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.

Kwa sasa, daraja refu kabisa duniani ni lile la Danyang–Kunshan lililopo China ambalo lina umbali wa kilometa 165, sawa na maili 102.4. Daraja hilo lilifunguliwa Juni mwaka 2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau wakati alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda ambaye alitaka kufahamu kama kuna matarajio ya kujenga daraja kubwa zaidi, ikiwezekana la kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema wapo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ambapo mazungumzo hayo yakienda sawa, ujenzi wa daraja hilo huenda isiwe ndoto, bali ukweli.

"Hilo wazo lipo mheshimiwa na tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali, kwa hiyo hilo wazo lipo na sisi tulilifikiria," alisema Dk Dau.

Kamati hiyo ilifanya ziara katika miradi mikubwa mitatu ya shirika hilo ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi na 'Dege Eco village' ambao una nyumba zaidi ya 7,000.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mtanda alisema, kamati yake imeridhishwa na miradi hiyo ya NSSF ambayo inaendelea huku akitaka kuongezwa kwa kasi ili watanzania waanze kunufaika na miradi hiyo.

"Muangalie na hilo la ujenzi wa daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na mradi wa makazi bora na salama ambao utaweza kubadili taswira ya Jiji la Dar es salaam," alisema.

Alisema kamati yake isingependa kuona changamoto zozote ambazo zinaweza kukwamisha miradi hiyo na kwamba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaangalia namna ya kuunganisha miundombinu karibu na miradi hiyo.

"Lakini pia tumesikia kuwa serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi, tunashauri serikali kuilipa mifuko hii ili kuifanya kuwa na nguvu na kuweza kuleta maendeleo," alisisitiza Mtanda.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU