Tetesi zilizopo mtaani zinasema hii ni helkopta ya mchungaji Ngwajima.
Wednesday, August 20, 2014
E-FM YAENDELEA KUIBOMOA ITV/R.ONE BAADA YA KITENGE, YAMCHUKUWA KATANGA
Omar Katanga
Katanga
Aliyekuwa
mtangazaji wa Radio One,OMARY KATANGA (mlinda mlango no.1) hatimaye leo
amejiunga na kituo kipya cha radio(E.FM) kinachorusha matangazo yake
toka mikocheni Jijini
Dar es salaam.
Katanga ametangaza kupitia katika ukurasa wake wa facebook kuwa amejiunga na E - fm.
Bila shaka wapenzi wa kipindi hicho watahama na watangazaji hao maana kipindi ndiyo kama kimevunjwa kabisa kwa kuwachukuwa waendeshaji wake maarufu ambao wamejizolea sifa hapa nchini.
"WAUNGWANA: WENGI
MMEKUWA MKINIULIZA MBONA HAMNISIKII KWENYE KIPINDI CHA SPOTI
LEO-NICHUKUE FURSA HII KUWAJULISHA KWAMBA HAMTANISIKIA TENA RADIO ONE
KUANZIA IJUMAA ILIYOPITA AGOSTI 15,2014.
KWA UWEZO WA MUNGU MTANISIKIA TENA.......POLENI KWA USUMBUFU LKN....ASANTENI KWA USHIRIKIANO WENU."
KWA UWEZO WA MUNGU MTANISIKIA TENA.......POLENI KWA USUMBUFU LKN....ASANTENI KWA USHIRIKIANO WENU."
Hayo ni maneno aliyo andika Omar Katanga kwenye ukurasa wake wa face book.
RAIA WA LIBERIA WAKATAZWA KUTOKA NJE ILI KUJIKINGA NA EBOLA
Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza amri ya kutotoka nje kwa wananchi wake nyakati za usiku kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi katika eneo la Kitongoji cha West Point viungani mwa Jiji la Monrovia.
Hali hiyo imetokana na tukio lililotokea hivi karibuni la watu kushambulia kituo cha afya katika eneo hilo na kusababisha wagonjwa 17 wa Ebola kutoroka.
Mgonjwa mmoja kati ya 17 waliotoroka katika kituo cha afya akiwa amebebwa na kijana.
Rais Sirleaf ameilaumu serikali yake kwa kutothibiti homa hiyo ya
Ebola, kwani haikufanya vya kutosha kuboresha hali ya maisha ya raia
walipopuuza ushauri wa wafanyakazi wa huduma za afya na kutotilia
maanani tahadhari rasmi za Ebola.
Hata baada ya Liberia kutangaza hali ya dharura
kufuatia mlipuko wa Ebola mapema mwezi huu, ugonjwa huo unazidi
kusababisha vifo nchini humo.
Ebola haina tiba lakini Shirika la Afya Duniani
(WHO) liliidhinisha matumizi ya dawa zilizokuwa zikifanyiwa utafiti
kufuatia mlipuko mkubwa wa Ebola Afrika Magharibi .
PICHA:MWALIMU MKUU AKIPEWA ZAWADI YA KUFELISHA
Mwalimu mkuu shule ya msingi kamanga Bw.Lucas Nicolaus(Pichani) iliyoko wilaya ya chato amekabidhiwa zawadi ya kinyago cha kutisha (kina sura ya mtu zoba /mburura) baada ya shule yake kuburuza mkia katika matokeo ya mtihani wa taifa (NECTA) wa darasa la saba 2013. Wilaya ya chato huwa na utaratibu wa kuwatunuku zawadi za ngao na fedha taslimu kwa shule zilizofanya vizuri na kinyago cha kuogofya kwa shule zilizofanya vibaya. Zawadi hizo zilizotolewa na afisa elimu wa wilaya ya chato Bw.Angasirin Obed Kweka mbele ya baraza la Madiwani wilaya ya chato hapo jana.
Mimi nimependa sana utaratibu huu wa kuwatunuku, rai yangu ni kuomba na halmashauri zingine nchini ziinge utaratibu huu katika mitihani yote kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha sita,pia na NECTA waige mfano huu.
Wadau mnaionaje huu mtindo kwani elimu hata ya zile shule kongwe nchini imekuwa ikizidi kushuka siku hadi siku. hii inaweza kuwa njia ya kurudisha hadhi ya elimu yetu kwa kiasi falani.
YANGA NA COASTAL ZAGONGANA PEMBA
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Coast Union
Picha Maktaba:
Katika kile kilichodaiwa kuwa ni maandalizi ya Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo inataraji kuanza hapo mwezi ujao wa Tisa ilitokea hali ya kushangaza pale timu mbili ambazo pia zinajiandaa na ligi hiyo YANGA
na COASTAL Ziligongana Pemba jana.
Baada ya timu ya Yanga kutua kisiwani kwa
mafungu (juzi)siku ya Jumatatu na timu ya Coastal union nayo ilitua kwa mafungu kisiwani humo jana (siku ya Jumanne).
Hali
hiyo ilileta mkanganyiko wa nani atautumia uwanja wa Gombani kabla ya
kukubaliana kuwa timu zote zitakuwa na vipindi viwili vya kufanya maoezi uwanjani hapo ambapo Coastal ndiyo wanaanza saa 12 asubuhi mpaka saa 2 mbili asubuhi na Yanga wanaanza
saa 2 asubuhi mpaka saa 4, na wanarudi tena saa 8 mchana mpaka saa 10
jioni, ndiyo Coastal wanaingia tena kumalizia awamu yao ya pili.
Awali
iliarifiwa kuwa ziara ya wana jangwani hao ilipangwa kuanza tarehe za
mwanzoni mwa mwezi huu hivyo kufikia tarehe 17 hadi 18 ndiyo wangekuwa
wanaondoka, lakini kwa kuwa jambo hilo limewekwa sawa ratiba ndiyo
itakuwa hiyo, kufatia timu 2 hizo za bara kugongana kisiwani humo na
wekundu wa msimbazi kuwa Unguja wadau wanahoji kuna ni visiwani??
Chanzo: kitongoni(Pemba)
Tuesday, August 19, 2014
PAPA AMRUHUSU PADRI MOSHA KUOA
![]() |
| Kiongozi wa kanisa katoliki duniani |
Moshi. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo. Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote.
Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi. Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.” Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.
CHANZO: TANZANIA CLASSIC
MWANAUME ALIEJIFANYA MWANAMKE NA KUPATA KAZI AKAMATWA UGANDA
Mwanaume mmoja huko nchini Uganda Amekamatwa baada ya Kujifanya ni Mwanamke ili apate kazi ya 'House Girl'.
Zoezi lake hilo lilifanikiwa na kuweza kupata hiyo kazi lakini siku zilivyozidi kwenda Boss wake ambae ni Mama Mwenye Nyumba alishtukia mchezo na kugundua ni Mwanaume, Baada ya kugundulika jamaa alichukua kipigo kutoka kwa Majirani , alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo alijitetea akasema Maisha ni magumu na kupata kazi kama mwanaume ni ngumu.
MIAKA 18 BILA KOMRED A M BABU (1924 - 1996): TAFAKURI JUU YA ATHARI ZA 'UTAJIRISHO WA UTAWALA'
![]() |
| Arrival Cabral, Abdulrahman Babu na Eduardo Mondlane |
"Kwa dhahiri Ken Saro-Wiwa alipaswa kuuawa, hiyo ni kwa sababu
alishirikiri kutenda kile kinachojulikana katika dunia ya tatu kama
'Dhambi ya Kiuchumi' - Kutishia muunganiko wa Kimaslahi kati ya
'Makampuni ya Kimataifa' na Viongozi Walarushwa wa Nchi za Dunia ya
Tatu. Wajumbe wa Genge la Watawala wa Kijeshi
wa Nigeria walikuwa Manyang'au kwa kuwa walihakikisha sehemu kubwa ya
mapato ya Mafuta ya Taifa hilo yanaelekezwa kwenye kukuza Utajiri wao
binafsi, na yeyote ambaye alionekana kupinga mpango huu maalum wa
'Utajirisho wa Watawala' alipaswa kushughulikiwa kwa njia yoyote iwayo,
halali ama haramu.
Sehemu kubwa ya Mafuta yaliyopelekea mauaji haya ya kila aliyeonekana ni kikwazo cha 'Utajirisho wa Viongozi' yalitokea katika eneo la Ken Saro-Wiwa la Ogoniland. Kampuni ya Mafuta ya 'Shell Oil' ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya Shirika la Mafuta la Nigeria, Mafuta ni chanzo kikuu cha 'Rushwa ya Kutisha' inayozunguka maisha ya Nigeria.
Saro-Wiwa hakuwahi kujaribu kukusanya nguvu ya wafuasi katika ngazi ya Kitaifa. Alizituamanisha harakati zake za kudai maslahi ya kiuchumi yatokanayo na Rasilimali kwa watu wake wa Ogoni tu, eneo ambalo lilikuwa na changamoto tofauti na sehemu nyengine za Nigeria. Nigeria bado haijaweza kuzalisha Kiongozi Mahiri mwenye maono na Karisma ya kuwaunganisha pamoja Mamilioni ya Wanaijeria wote ili wauondoe Utawala wa Rushwa na Kinyang'au. Kwahiyo basi Mafungamano ya 'Utajirisho wa Watawala' kati ya Serikali na Makampuni ya Kimataifa yataendelea kufaidi sehemu kubwa ya Rasilimali za Taifa hilo.
Kuthibitisha hilo (La kuendelea kwa mafungamano ya 'Utajirisho wa Watawala'), siku mbili tu baada ya Kunyongwa kwa Ken Saro-Wiwa pamoja na Wanaharakati wenzake nane wa Ogoni (Saturday Dobee, Nordu Eawo, Daniel Gbooko, Paul Levera, Felix Nuate, Baribor Bera, Barinem Kiobel na John Kpuine), Kampuni ya Mafuta ya Shell Oil ilisaini Mkataba wa Dola Bilioni 2.5 (Zaidi ya Trilioni 4 za Tanzania) kwaajili ya Gesi ya Taifa hilo".
Komredi Abdulrahman Mohamed Lain Babu (1924 - 1996), katika Makala yake 'WHY KEN SARO-WIWA HAD TO HANG?' iliyochapwa na Pacific News Service, San Francisco, Marekani - 1996.
Zaidi ya Miaka 18 iliyopita Makomredi wawili muhimu kwa Mapambano ya 'Ukombozi' wa pili wa Bara la Afrika waliiaga dunia, vifo vyao vikiwa na mafunzo makubwa mno kwa kizazi cha sasa cha Tanzania na Afrika kwa Ujumla, hasa kwa mazingira tuliyonayo ya Unyonywaji wa Rasilimali za nchi za Kiafrika unaofanywa kwa ushirikiano kati ya Watawala Mafisadi wanaoziongoza nchi zetu na Makampuni ya Kibepari ya Kimataifa yanayoletwa kwa wimbo wa 'Uwekezaji' usiowanufaisha wananchi wanyonge.
Makomredi hao ni Ndugu Kenule "Ken" Beeson Saro-Wiwa - Mwandishi, Mtayarishaji wa Vipindi vya Televisheni na Mwanaharakati wa Mazingira, na Rais wa Vuguvugu la Uhai wa watu wa Ogoni, MOSOP, aliyeuawa Novemba 10, 1995 kwa kunyongwa na Serikali Katili ya Kijeshi ya Dikteta Sani Abacha baada ya kuendesha Kampeni za kutokutumia nguvu kupinga Uharibifu wa Mazingira uliokuwa ukifanywa na Makampuni makubwa ya Mafuta yaliyokuwa yakichimba mafuta katika eneo la Ogoni, Niger Delta, Nigeria.
Mwengine ni Komredi Abdulrahman Mohammed Lain Babu, Kiongozi Mzalendo mwenye kufuata Itikadi ya Ukomunisti wa mrengo wa Kimarxi na mmoja wa waasisi wa Taifa hili. Babu alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kizalendo cha Kizanzibari cha ZNP, Mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la China, Mhariri wa Jarida la Kimapinduzi la ZANEWS, Muasisi na Rais wa Chama cha Mrengo wa Kushoto cha Umma Party kilichorikiana na Chama cha ASP kuunda Serikali ya kwanza ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Babu pia alikuwa Waziri wa Mambo ya nje wa SMZ chini ya Rais Karume na Waziri wa Kwanza wa Mipango na Uchumi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Nyerere.
Tarehe 5 mwezi kama huu mwaka 1996 Komredi Babu aliiga dunia jijini London mara baada ya kuumwa kwa muda mfupi, Alizikwa nyumbani kwao Ukutani katika Viunga vya Mji Mkongwe, Unguja Agosti 9, 1996 - Leo ikiwa ni miaka 18 na siku kadhaa tangu Mzalendo huyu atutoke.
Pichani ni Komredi Abdulrahaman Mohammed Babu akiwa pamoja na Komredi Amilcar Cabral (Kushoto), Mhandisi-Kilimo, Mwandishi na Mpigania Uhuru wa Nchi za Guinea-Bissau na Cape Verde na Katibu Mkuu wa Chama cha PAIGC na Komredi Eduardo Mondlane (Kulia), Rais wa Chama cha Ukombozi cha Msumbiji, FRELIMO. Picha husika ilipigwa Oktoba 1965, Jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Vyama vya Kupigania Uhuru wa nchi za Afrika zinazotawaliwa na Ureno - CONCP, Mkutano ambao Babu alikuwa Mgeni Rasmi.

Picha ni kwa hisani ya Hifadha ya Watanzania Mashuhuri .
Babu ni
Mchumi Mjamaiya
Komredi Mmarxiya
Mwafrika Mmajumiya
Mzalendo Mtanzaniya
Mwanamapinduzi Mzenjibiya
Ulale Pema Mahliya
Vijanao Twakuombeya
Subscribe to:
Posts (Atom)